EPA na mambo yake

EPA na mambo yake

Yeah kundi jinginee linapelekwa kesho (watu kama nane hivi); watu wangesoma makala yangu ya Tanzania Daima mapema leo asubuhi wangepata clue kidogo of what is happening. It is more dramatic.. lakini hili limeandaliwa kuendelea hadi around early 2010...

Kitu ambacho ni lazima tukikatae ni "uchunguzi bado haujakamilika". Kwa vile uchunguzi wote uko tayari na ushahidi hii kesi ingefanywa kwa mfululizo ili ndani ya miezi sita kesi ya msingi iamuliwe, na kabla ya mwisho wa mwaka ujao rufaa ziwe zimefikia kikomo chake.

Vinginevyo, pesa zinachukuliwa, jamaa wanarudishiwa vittu vyao, wana counter suit kwa sababu hii kesi imeandaliwa kushindwa si kwa sababu ya kukosa ushahidi bali kwa masuala ya kiufundi.
 
hivi haiwezekani jf iwe na wakili wa kuwatetea hawa mafisadi lakini kwa maslahi yetu kuwa aweze ku spin kesi ili wafungwe kitakatifu, yaani wakili wa kuwauwa akina patel! wataalam wa sheria tusaidieni hapo, ile inaitwa kuuwa wakati unatibu mwenyewe!

This is possible, but its too good to be true. Cha msingi kukumbuka ni kwamba, hawa mawakili wanapenda kujenga reputation by winning "unwinnable" cases. The likes of OJ Simpson cases. Hapo ndipo wakili anajenga jina na kujiongezea umaarufu. Kama huku Kamara atashinda hii kesi, that means atapata mafisadi wengi zaidi wenye kesi za aina hiyo na nyingine nyingi. Kama wangekuwa wazalendo, basi wangefanya kazi kwa manufaa ya taifa zima.
 
Hawana Hatia kwa kuwa wana mbinu za ushindi?
Hawana hatia sababu hawa ni bangusilo?
hawana hatia sabnabu hawa ni CCM?
HAwana hatia kwa kuwa RAis ni rafiki yao?

Wenye hatia ni wale waliochukua pesa za Kagoda Agriclutrure.
Wenye HATIa ni pamoja na wale waliorudisha pesa
Wenye hatia ni ile kambi ya mtandao ambayo ilikuwa na pesa nyingi
Wenye hatia wapo wamelala na wanastarehe?

Yes hawa mie ndiyo nataka wafikishwe mahakamani fasta
Yes Tuwaombee Mungu awalaani
Yes Pongezi ziende kwa Hoseah?
Yes Tumshukuru RAis Kafanya kazi ipasavyo?

Ukiwa makini utagundua Jeetu patel Mjanja sana
Ukiwa makini utagangalia kwani hao watu wa BOT walikuw aawajinga kiasi gani mpaka wakatapeliwa navyojua mimi kwa BOT kulipa billioni zaidi ya moja kwa acccount kama hiyo lazima zipite sahihi zisizop[unguza 10 na mojawapo ni ya Gavana(Masikini Balali wanayesema amekufa?)

Mie nadhani bado hatujapata Mchawi,CCM walisema PESA za EPA siyo za Serikali sasa kwanini wanawafungulia Mashtaka?yaani huu ni usaniiii mwingine na as usual tunashabikia upinzani?yaani tunashabiki kufungwa bao lingine la Kisigino.

Mwanakijiji kama utakumbuak akuna mtu alisema maneno haya Last week kwamba hawa watu watafunguliwa mashatka.Kama sikosei RAia Mwema na thena tutaendelea kuzugwa mpaka basi.Unafikiri kwa mali alizonazo Lukaza watakosa Dhamana ??Jeetu patel na pesa za wahindi wenzake wa jhamatini watashindwa kumtoa.

There is "something"wrong somewhere.Kuna kitu mkului anashindwa kutambua watanzani wanataka nini,Yes kuna haja sasa atambue watanzania wanamtaka yeye abadili khali ya uchumi wa nchi yetu kwanza kwa kuandaa kampeni maalum.SAfisha serikali kwa kutoa watendaji wabadhirifu na Mafisadi.

Tatizo liko Kwa wafanyakazi wa serikali wala Rushwa na Vihiyo.
Taatizo ni hawa kina Mgonja wenye kiburi.
Tatizo ni Hii CCM ambayo inawalea Mafisadi.

Kama Serikali ni Tatizo na CCM ni tatizo,YEs We can kama tukijipanga na kuamua kuweka nguvu zetu kwenye CHamama kimoja kisicho na sura ya Ukabila,Udini na tuwe nguvu moja na nitakuwa tayari kujiunga na chama hicho.

Natamani Chama ambacho kitawaweka wale wote waliohusika na EPA ndani
Natamani chama ambacho kitawafunga wale wote waliohosika na dili ya RDC
Natamani Chama ambacho kitawashtaki wei wa import Support
Natamani Chama ambacho kitakemea Mafisadi

Je mko tayari kuniunga Mkono kwa ajili ya Kuanzisha Chama kipya?
 
Jeetu Patel ni nani? Naona wachangia wengi wanasifu "UWEZO and UKUBWA" wake? Kama kuna mjumbe anafahamu u-TAJIRI, u-KUBWA, e.t.c, basi na atupe habari!
 
Tumepigwa changa la macho, hao wahindi waliopelekwa na Jeetu Patel mahakamani wote wachovu, kwa kuwaangalia tu unawaona, Watanzania fumbueni macho na muone mbele...... kwa jana tumepigwa mchanga wa macho kwa kweli, hata huyo Jeetu Patel kwa sababu tu ya umarufu wake ndio maana wamempeleka pale la sivyo na yeye tungeletewa mdosi yoyote tu.

Hii ndio Tanzania zaidi ya uijuavyo.
 
YES! hii habari kubwa sana...Kwa wanaomfahamu Jeetu nadhani mtakubaliana nami kwamba sasa Kikwete kaamua kufanya mambo!..
Kwanza fedha kisha kusanya, halafu imefuatia mahakama na kesho nasikia kundi jingine linavutwa ndani!.. Jamani sii haya ndio tulikuwa tunayaomba JF toka kitambo!
Wangechukuliwa mahakamani mwanzo tusingepata hata ndululu...Sii haba jamani sii haba hata kidogo.
Mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Hivi ndivyo WADANGANYIKA tunavyo danganyika kiurahisiiiii " eti KIKWETE kaamua kufanya kweli"
 
Jeetu mbona niko nae Dhubai wee Halisi wacha dangnanya watu sasa bana
 
Kuwakamata haina shida....
Kuviita vyombo vya habari na kutoa statement kuwa wamewakamata haina shida...
Kuonekana kwenye viunga vya mahakama wakiwa na nyuso za huzuni haina shida pia.....
kusema wamenyimwa dhamana nako hakuna shida.......
Kunza kesi na kusomewa mashataka hakuna shida........
Kikwete kupongezwa na watu wasiofikiri mbali nalo halina shida.....
Jumuiya za kimataifa kumsifia Kikwete kuwa anafanya kazi vizuri hakuna shida pia,,,,,,,
Luwa watahukumiwa kwenda jela, ilo nalo halina shida....

kuwa wataenda jele gani, watakaa vipi , hili nalo lina shida na maswali yake!

Tatizo ni pale wanaposhindwa kujibu maswali yetu.

1. Kuwa kulikuwa na wahusika wangapi katika wizi huu?
2. Wahusika hao ni akina nani?
3.Kwa nini majina yao yalifichwa?
4.Kuwa CCM na serikali yake kwanini wamechukua muda mrefu kulishugulikia swala hili:
5.Kuwa wezi hao wana nguvu kuliko serikali kama alivyokwisha wahi kusema Pinda?
6.kuwa watu wanaoichangia CCM , CCM inawajua au mtu yeyote yule hata kama anauza ngozi za watu? wanachukua tu pesa?

siamini bado swala zima hili, mpaka hap nitakapomwona jeetu patel, kwe

waberoya


Wakuu mimi siamini kabisa haya mazingaombwe. Tunachezewa kikweli kweli! Kama kweli hatuchezewi basi waletwe wezi wote wa EPA na hata wale wa account nyingine za BOT. Kwani watu wanaolia kwenye sinema huwa wanalia kweli?? Natamani kubadili jina niitwe Tomaso!
 
Tunadanganywa tu. Mbona wakina RA waliyorudisha hela hawakamatwi!! Basi wezi wawe wanaiba hela nyingi ili wasishitakiwe.
 
i8_IMG0087.jpg



Kuna mtu anamjua huyu DADA?

nauliza tuuu si ugomvi

Huyo mwanamke anaitwa EDA ni mtu wa mambo ya urembo.Kuna mwanamke analalamika kuwa huyo dada ni kibaka mzoefu wa kutupwa kwani alimpora huyo mume Mwakale ambaye wanashistakiwa wote kwa kuiba hela za EPA.Alimpora huyo mume na kumfanya mumewe halafu wakaenda kushirikiana kupora hela za EPA.Sasa wote wako kizimbani.
 
Huyo mwanamke anaitwa EDA ni mtu wa mambo ya urembo.Kuna mwanamke analalamika kuwa huyo dada ni kibaka mzoefu wa kutupwa kwani alimpora huyo mume Mwakale ambaye wanashistakiwa wote kwa kuiba hela za EPA.Alimpora huyo mume na kumfanya mumewe halafu wakaenda kushirikiana kupora hela za EPA.Sasa wote wako kizimbani.


Je ni kweli huyu Eda anahuhusiano na Rita Mlaki?? mtueleze jamani...
 
Tunadanganywa tu. Mbona wakina RA waliyorudisha hela hawakamatwi!! Basi wezi wawe wanaiba hela nyingi ili wasishitakiwe.

Hilo shinikizo la kuwapeleka mahakamani ni ushindi kwa umma.Wangeweza kuamua hata wasiwafikishe lakini kila kukicha kelele za umma zinawasuta.
Sasa nguvu pia itaelekezwa mahakamani na umma utaendelea kuwapigia kelele kwa kuwa hili sakata linajulikana na sheria ichukue mkondo wake.
Hii sinema bado iko mwanzo,tuendelee kutazama tusichoke
 

Mkuu Halisi asante kutuhabarisha, pamoja na usanii hili la kuwafikisha mahakamani ni hutua kubwa sana kwa serikali ya Muungwana, wengi hatukutegemea

Ushi

Haa Haaaa Hah! uwe na vogue ukishachutama kisutu wewe ni mwizi tuu, hata watoke ishajulikana ni wezi ...
 
JK sasa ameonyesha anaweza. Kwa kuwa wengi tumeshamhukumu siku nyingi kwamba hawezi, inatuwia vigumu kubadili misimamo hiyo dhaifu.
 
Nadhani huu ni usani tu,muungwana anapangilia karata zake vizuri kwa ajili ya kuwazuga wadanganyika.Wakuu hii kesi itaendelea mpaka mwaka 2011,muungwana anajua atapata kitu cha kuwadanganya wadanganyika kwenye kampeni mwaka 2010.
 
jamani..
inawezekana ukawa ni usanii kama mnavyosema,lakini siamini ya kwamba hamuoni tumepiga hatua....hebu tuacheni kupinga kwa sababu tunapinga tu,kama ni kwa mashinikizo ama vinginevyo,hii ni hatua na ni sahihi kwenye suala zima la vita dhidi ya huu ufisadi...tupunguze munkari kidogo wana JF
 
jk sasa ameonyesha anaweza. Kwa kuwa wengi tumeshamhukumu siku nyingi kwamba hawezi, inatuwia vigumu kubadili misimamo hiyo dhaifu.

wenye fikra kama hizi poleni. Hii ni "epa remix part ii with an added verse"
 
Je ni kweli huyu Eda anahuhusiano na Rita Mlaki?? mtueleze jamani...


Huyu dada miaka ya mwanzo ya 90 alikuwa anafanya kazi SUKITA.Kwa hio sidhani kama anaweza kuwa mtoto wa Rita Mlaki.
Fununu za mitaani zinasema kuwa Jeetu Patel bail yake itakuwa shs 6b! Na akitoka tu,ndio moto! Tanil Somaiya,alipata habari hizi wakati yuko Mozambique,na inasemekana amekodi ndege kurudi haraka kuja kumsevu Godfather wake.Hao wengine,ngoma naona itakuwa nzito kidogo,lakini kuna kila dalili za kiini macho.
 
Back
Top Bottom