EPA na mambo yake

EPA na mambo yake

Macho yote kwa Feleshi sasa...

Huyu ndo wa kumtolea macho ili asituuze watanzania kwa sababu za kiufundi(most likely scenario according to MKJJ).

Maana niliwahi kusoma sehemu(hapahapa JF) wakati jamaa alipoteuliwa, kuwa ana hulka ya ufisadi na kuuza kesi, kama alivyowahi kufanya alipokua kanda ya ziwa na kesi ya mtoto wa mwarabu tajiri(refer thread ya Feleshi's appointment as New DPP)...

Tuwe nae macho huyu mtu hatari lakini anamamlaka makubwa sana. Kama vipi tumpigie makelele mpaka ang'oke pale akileta usanii wake kwenye hili.
 
Mkuu Halisi asante kutuhabarisha, pamoja na usanii hili la kuwafikisha mahakamani ni hutua kubwa sana kwa serikali ya Muungwana, wengi hatukutegemea

Ushi

Wakuu tuwe tunaosma habari humu JF na kuzikumbuka, haya ya kwenda mahakamani nimeyasema toka last two weeks kwamba inasubiriwa okay Muuungwana tu, lakini kesi zote ziko tayari kwa kufika kwenye sheria,

Muungwana amekua akisua sua sana na hili deal, akijaribu kila attempt kuwasukumia wabunge hii, lakini Sitta akamkatalia kata kata kwamba hii sio Richimonduli, na ndio maana nikasema kwamba habari iliyoletwa na Ibrah hapa last week kwamba Mramba na Mgonja waliokolewa mahakamani na Luhanjo, ilikuwa correct kwa 100%,

According to the dataz, hili ni kundi la kwanza tu kuna la pili linakuja kupelekwa huko kwenye sheria, sasa wananchi tuwe na busara pia na tuyaangalie haya matendo ya Muungwana, kwa macho mawili, knowing who muungwana is, na mazingara ya kisasa na kisheria ya nchi yetu pia, lakini tusisite kuukubali ukweli hata ukiwa kidogo.

Mkuu Ushi Wa Rombo, ahsante sana kwa huu ujumbe wako ambao ni solid unao onyesha understnding of our political realities, otherwise sisi tuko huku underground tunaendelea na project OIC, huku mtandao ni limited lakini tutarudi tena in full kuanzia tarehe 8, tutaanza na kui-monitor NEC session ya tarehe 8 & 9.

Respect kwa Wote!
 
Niliwaambia Rais wetu atachukua hatua juu ya suala hili la EPA baadhi yenu mkabeza.

Hatua Zipi?
Kuwasamehe waloiba hela wakafanyia biashara na kurudisha? Umeona wapi

Duniani Rais anayesamehe Wezi!?!?!

Labda na yeye awe "mwizi" ndo anaweza samehe wezi
 
Kuna kitu serikali ya JK ilikuwa inavizia...Matokeo ya uchaguzi wa USA nk....Ila hapa bado sitokurupuka na kusema everything cool. Ila ni hatua nzuri ya mwanzo.
Lukaza na Malegesi ni mashahidi muhimu sana na kama kweli kesi hii inaunguruma..Basi na wao kama maisha yao yanaweza kuwa hatarini kwani wanaweza kumwaga mchele mwingi kwenye kuku wengi, on the ither hand kesi either imepangwa ama serikali inaweza ikawa imeamua iwe mbaya.
Malegesi Law chamber(Advocates) kwa kushirikiana na FAMILIA YA KINA lUKAZA ndio walifanikisha uchotwaji wa pesa za EPA kwa kupitia amri ya ccm wazazi ambapo mwenyekiti alikuwa Idi Simba.
Kama alivyosema Halisi tunawapa muda...Ila muda unazidi kuwatupa mkono kwani hapa USA change tayari imekubali na swahiba wa JK ni Bush.
Huyu rwekaza bado anakumbuka kujiramba kama fiesta vile, hapo ni mahakamani dogo!

----------------
Sema na watu upate kiatu.
 
Mtuhumiwa wa wizi wa fedha za EPA Bwana Bahati John Mayenga (Mahenge?) amepandishwa kizimbani na ni kaka yake Janeth John Mayenga (Mahenge?) ambaye alipandishwa kizimbani mwezi Septemba kwa kosa la kughushi vyeti vya kidato cha nne kujipatia kazi BoT.
 
Hatua Zipi?
Kuwasamehe waloiba hela wakafanyia biashara na kurudisha? Umeona wapi

Duniani Rais anayesamehe Wezi!?!?!

Labda na yeye awe "mwizi" ndo anaweza samehe wezi

Unaambiwa Jeetu karudisha hiyo mihela lakini jana kasimamishwa kizimbani. Hebu rudisha mawazo nyuma kidogo kama miaka 18 iliyopita uone kama hatua hii ya jana ingeweza kufanyika chini ya Mzee Ruksa.
 
Sasa biashara ya magazeti itauzika balaaa.
Mpandishe bei kidogo jamani muwakumbuke hata waandishi angalau kipindi hiki cha x-mass watoke jamani.
Hii ishu ya EPA magazeti yatafanya biashara sana.
Tunaomba list ya walio pandishwa leo.
 
Mtuhumiwa wa wizi wa fedha za EPA Bwana Bahati John Mayenga amepandishwa kizimbani na ni kaka yake Janeth John Mayenga ambaye alipandishwa kizimbani mwezi Septemba kwa kosa la kughushi vyeti vya kidato cha nne kujipatia kazi BoT.

Utafutaji wa MAISHA na hasa fedha katika FAMILIA nyingi hapa Tanzania unafanana sana. Familia ya matapeli wote wanakuwa hivyo; sasa hivi familia za wanasiasa wote wanajitahidi kuwa wanasiasa!
 
Utafutaji wa MAISHA na hasa fedha katika FAMILIA nyingi hapa Tanzania unafanana sana. Familia ya matapeli wote wanakuwa hivyo; sasa hivi familia za wanasiasa wote wanajitahidi kuwa wanasiasa!

Mwana wa Msana husana asiposana?............................
 
JK sasa ameonyesha anaweza...

Haya bandugu, kura za Kikwete 2010 hizo hapo zinaanza.

Never underestimate that man. One of the most shrewd politicians Tanzania has ever seen. Anajua jinsi ya kuwashika vichwa Watanzania.

Unaachia wakina Ndullu na Mgonja na Chenge na Mramba waliokuwa viongozi wakati wa huu ufisadi unaenda kukamata Wahindi kafara wawili watatu halafu Watanzania wanakuwa taken in!! Daaah!

Kikwete ndugu yetu umetukamata sehemu muhimu, you got us by the balls, wanasema Wamarekani. Hatuwezi kufurukuta. Tusali.
 
Mtuhumiwa wa wizi wa fedha za EPA Bwana Bahati John Mayenga (Mahenge?) amepandishwa kizimbani na ni kaka yake Janeth John Mayenga (Mahenge?) ambaye alipandishwa kizimbani mwezi Septemba kwa kosa la kughushi vyeti vya kidato cha nne kujipatia kazi BoT.

Hao ni ukoo wa akina Mahenge siyo Mayenga kama ulivyoandika rekebisha taarifa zako umekosea mheshimiwa.
 
jamani hakuna update mpya yahao jamaa wa epa?hakuna ingizo jipya leo pale kisutu?hakuna aliepata dhamana?
 
And the Winner is?................................
.........................................................
.........................................................
.........................................................
JK, I guess
 
habariiliyoingia hivi punde toka redio one ni kua jamaa wa mibale farms kwenye ile sakata ya EPA nao wamepandishwa pale kwa mweshimiwa chusi wa kisutu
 
Ivi hawa jamaa sawa wameiba but nahisi bado kunawengine walikokuwa wanawapa hawa jamaa ushirikiano wa kribu katika zoezi zima,hawa wasingekua na Guts kwenda kichwa kichwa kujichotea mihela....isije kuwa danganya toto tu hapa!!!
 
habariiliyoingia hivi punde toka redio one ni kua jamaa wa mibale farms kwenye ile sakata ya EPA nao wamepandishwa pale kwa mweshimiwa chusi wa kisutu

Ni kina nani wanahusika na Mibale Farms. Hivi Kagoda wanahusika na EPA, au dawa yao bado iko jikoni.
 
Haya bandugu, kura za Kikwete 2010 hizo hapo zinaanza.

Never underestimate that man. One of the most shrewd politicians Tanzania has ever seen. Anajua jinsi ya kuwashika vichwa Watanzania.

Unaachia wakina Ndullu na Mgonja na Chenge na Mramba waliokuwa viongozi wakati wa huu ufisadi unaenda kukamata Wahindi kafara wawili watatu halafu Watanzania wanakuwa taken in!! Daaah!

Kikwete ndugu yetu umetukamata sehemu muhimu, you got us by the balls, wanasema Wamarekani. Hatuwezi kufurukuta. Tusali.

Hahahaa....Siasa ndivyo ilivyo ndugu yangu; Timing is everything.
 
Haya bandugu, kura za Kikwete 2010 hizo hapo zinaanza.

Never underestimate that man. One of the most shrewd politicians Tanzania has ever seen. Anajua jinsi ya kuwashika vichwa Watanzania.

Unaachia wakina Ndullu na Mgonja na Chenge na Mramba waliokuwa viongozi wakati wa huu ufisadi unaenda kukamata Wahindi kafara wawili watatu halafu Watanzania wanakuwa taken in!! Daaah!

Kikwete ndugu yetu umetukamata sehemu muhimu, you got us by the balls, wanasema Wamarekani. Hatuwezi kufurukuta. Tusali.

Kuhani,
Unapomnukuu mtu chukua maandishi yote kama yalivyo kuliko kuchukua yale tu unayoona yanakidhi nia yako kwa wakati huo. Hivi kweli JK hana jema analolifanya kwa NCHI hii kama Rais wetu?
 
kuna tetesi kuwa mahakimu wote leo wameketishwa chini na wakuu wao juu za hili sakata, vi inzi vya hapo vijitume watupatie hiyo nyeti.
 
Back
Top Bottom