EPA na mambo yake

Mimi nilianza kufurahia mafisadi kushughulikiwa lakini baada ya ile namba kubaki pale pale 20, naona hapa tunafungwa goli lingine.

Hivi kuna haja gani ya usiri kwenye jambo ambalo liko wazi kama hili?

Sasa inabidi tumpe changamoto DPP, kufuatana na hayo maneno kwenye field yake, ya sheria, sio wanatupiga chenga za mwili, wakati nia ya kufunga magoli hawana
 
Sasa inabidi tumpe changamoto DPP, kufuatana na hayo maneno kwenye field yake, ya sheria, sio wanatupiga chenga za mwili, wakati nia ya kufunga magoli hawana

That is very true in this EPA-blah.....blah thing.
 

hapa Mkuu justice imekwua delayed kutekelezwa. yaani watu wameachwa wanatumbua mihela yetu huku sisi tunaguguna kwa umasikini hadi wenzetu wamekufa ndio leo wanafikishwa mahakamani!
Pia, kwangu mimi, ukichukulia malalamiko ya mahakimu wanaondesha kesi hizo, sioni kama justice seems to be done here
 
Siri nzito EPA (Tanzania Daima)




na Salehe Mohamed



SIRI ya kufichuka kwa wizi uliokuwa ukifanyika kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeanza kubainika.

Habari ambazo Tanzania Daima Jumapili limezipata kutoka vyanzo vya kuaminika ndani na nje ya serikali, zinaeleza kuwa kubainika kwa siri hiyo kulitokana na hatua ya mfanyabiashara mmoja Mtanzania mwenye asili ya Kiasia, kuamua kulipiza kwa kutoa siri za wizi huo uliofanywa na mfanyabiashara mwenzake mwenye asili ya Kiasia, ambaye alimdhulumu kiasi kikubwa cha fedha.

Habari hizo zinaeleza kuwa wafanyabiashara hao, ambao (majina yao tunayo) walikuwa marafiki wa karibu na walikuwa wakifanya udanganyifu huo kwa pamoja huku wakishirikiana na wafanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Mmoja wa wafanyabiashara hao ambaye hivi sasa yuko rumande baada ya kupewa masharti magumu ya dhamana katika kesi inayowakabili, ndiye anayetajwa kumdhulumu mwenzake baada ya kuona amekamilisha nyaraka zote muhimu zilizokuwa zikitakiwa katika kuiba fedha kutoka EPA.

Taarifa zaidi kutoka kwa baadhi ya maofisa wa BoT zinaeleza kuwa mpango wa wizi huo uliowafanya wafanyabiashara hao kutengana ulikuwa ni wa zaidi ya sh bilioni 20, ulioandaliwa kwa muda mrefu na kwa umakini wa hali ya juu na wafanyabiashara hao kabla hawajadhulumiana, kama wafanyavyo majasusi mbalimbali duniani.

Mfanyabiashara anayesota rumande hivi sasa ndiye aliyedakia ‘dili' ya mwenzake ambaye alikuwa katika hatua za mwisho za kuzungumza na wafanyakazi wa BoT ili wamsaidie kufanikisha wizi huo.

Inaelezwa kwamba, katika hali isiyo ya kawaida, Mfanyabiashara huyo aliye rumande alipata nyaraka hizo na kuwakalisha kitako wafanyakazi wa BoT ambao waliingia katika mtego wake na kuidhinisha kiasi hicho cha fedha.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa hasira za mfanyabiashara aliyezungukwa na kudhulumiwa na mwenzake zilikuwa kubwa baada ya kubaini kuwa amezungukwa na fedha alizokuwa akitegemea kuzipata kutoka BoT zimekwisha kuchukuliwa na kuingizwa katika akaunti za kampuni za aliyemdhulumu zilizo ndani na nje ya nchi.

Baadhi ya watu walio karibu na wafanyabiashara hao, wameleeza kuwa njama za wizi huo zilifichuka kutokana na hasira ya kuzungukwa aliyokuwa nayo mfanyabiashara aliyedhulumiwa.

Kwa mara ya kwanza mpango wa wizi huo uliwasilishwa kwa mbunge mmoja ambaye anasifika ndani na nje ya Bunge kwa kulipua hoja nzito, anapokuwa akichangia mijadala mbalimbali katika vikao vya Bunge.

Walieleza kuwa tofauti na matarajio ya mfanyabiashara huyo, mbunge huyo aliwasiliana na watendaji wa juu wa BoT na anadaiwa kuwa ili kuhahakisha suala hilo halilipuliwi bungeni, yalifanyika mazungumzo ambayo mpaka sasa yamekuwa siri.

Mmoja wa maofisa wa BoT aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la jina lake kutotajwa gazetini, alieleza kuwa baadaye taarifa za wizi huo zilisambazwa na mfanyabiashara huyo katika mtandao wa ‘internet' na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Benki ya Dunia (WB) pamoja na wahisani mbalimbali nao walitaarifiwa kuhusu wizi huo.

Kusambazwa kwa taarifa hizo, mtandaoni, kuliwafanya baadhi ya wabunge akiwamo Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa (CHADEMA), kuzidaka na kutinga nazo bungeni, ambako alilivalia njuga suala hilo na kutaka ufafanuzi kuhusiana na taarifa hizo huku akilitaka Bunge liunde kamati teule kuchunguza.

Uchunguzi zaidi wa gazeti hili umebaini kuwa hakuna taarifa sahihi za moja kwa moja mwanzoni mwa sakata hilo, na ndiyo maana alipotaka kiasi cha fedha kilichoibwa katika akaunti hiyo alisema ni sh bilioni 800, lakini baadaye ilielezwa na mbunge mmoja anayedaiwa kulijua kwa undani sakata hilo kuwa kiasi kilichoibwa ni sh bilioni 133.

Aliyekuwa Waziri wa Fedha, Zakhia Meghji, alisema taarifa hizo za Dk. Slaa, si sahihi na analidanganya Bunge.

Aliongeza kuwa serikali haifanyi kazi kupitia taarifa za kwenye mitandao ambazo hazina ukweli wowote.

Dk. Slaa, alionyesha nia ya kutaka kutoa hoja binafsi lakini hakufanikiwa, kwani alizimwa na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, aliyemwambia nchi haiwezi kuendeshwa kwa kutegemea taarifa za kwenye mtandao.

Fukuto la EPA lilizidi kushika kasi hasa pale wafadhili walipotishia kufunga misaada yao kwa Tanzania mpaka ufanyike uchunguzi katika akaunti ya EPA na hatimaye serikali ilisalimu amri na kuipa jukumu Kampuni ya Ernst & Young kufanya ukaguzi.

Kampuni hiyo iligundua kampuni 22 zilijichotea kiasi cha sh bilioni 133 na kuwasilisha ripoti yake serikalini ambapo Rais Jakaya Kikwete aliamua kutengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa BoT, marehemu Daudi Balali, aliyekuwa nchini Marekani kwa matibabu.

Pamoja na kutengua uteuzi wa Balali, Rais Kikwete, aliunda timu ya kufuatilia suala hilo iliyokuwa ikiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Johnson Mwanyika, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hoseah, ambayo ilitoa taarifa na kupendekeza wote waliohusika katika wizi warejeshe fedha.

Aidha, timu hiyo iliomba iongezewe muda kutafuta taarifa za kampuni tisa ambazo mpaka sasa hazijaweza kujulikana zilipo.

Rais Kikwete, alikubalina na mapendekezo hayo ya timu hiyo na kutoa muda mpaka Novemba mosi kwa wezi wa EPA wawe wamerejesha fedha hizo la sivyo atawaburuza mahakamani.

Muda alioutoa Rais Kikwete, ulimalizika na baadhi ya wezi walishindwa kurejesha fedha. Hivyo, Rais Kikwete, alimwagiza Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) Elieza Feleshi, kuwafikisha mahakamani watu wote waliohusika kwenye wizi huo.

Feleshi, alianza kulitekeleza jukumu hilo, ambapo mpaka sasa watuhumiwa 20 wameshafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Kampuni 22 zilizovuna mabilioni ya EPA ni Bencon International Ltd of Tanzania, VB & Associates Ltd, Bina Resorts Ltd, Venus Hotels Ltd, Njake Hotels Ltd and Tours Ltd, Maltan Mining Company na Money Planers and Consult, Bora Hotels and Apartment Ltd na BV holdings Ltd.

Nyingine ni Ndovu Soaps Ltd, Navy Cuts Tobaco Ltd, Changanyikeni Residential Complex, Kagoda Agriculture Ltd, G&T International Ltd, Mibale Farm Liquidity Sevices Ltd, Clyton Marketing Ltt, M/s Rastash, Malegesi Law Chambers, Kiloloma and Bothers na Karnel Ltd.

Hadi sasa jumla ya washitakiwa 20 wa EPA wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma zinazowakabili kuhusiana na wizi huo.
 
Nafikiri hapo mbunge anayesemwa ni Mzindakaya ambaye baada ya kumegewa na Ballali
mabilioni kwa ajili ya kiwanda chake cha nyama, akaamua kuwauza Watanzania.

Nahisi urafiki wa Mkapa, Ballali na Mzindakaya unaunganishwa na mapesa ya BOT.

Mtu kama Mzindakaya ana haki gani hata ya kuendelea kuwa mbunge?
 
Wanabodi,
Ebu turudi nyuma kidogo.. Hivi ni mashirika mangapi kati ya yote yaliyohusika yamefikishwa mahakamani isije kuwa focus nzima ya serikali imelenga WATU badala ya mashirika yaliyohusika..
Kati ya hao watuhumiwa 20 waliokwisha fikishwa mahakamani wanawakilisha mashirika mangapi?
 

Malegesi, Kagoda bado
 
CCM: Hatumo katika wizi EPA
Faraja Mgwabati
Daily News; Sunday,November 16, 2008 @20:10

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakihusiki na wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kama kuna wanachama walihusika, hawajatumwa na chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi, John Chiligati alisema madai kwamba CCM iliiba fedha kwa ajili ya uchaguzi wa 2005, yamethibitika kuwa ni uongo.

“Nasikitika kwa jinsi viongozi wa upinzani walivyokipaka matope chama chetu kupitia sakata la EPA, lakini kwenye ukweli uongo hujitenga… ukweli ni kwamba CCM haikuchukua fedha hizo ndiyo maana hata kwenye ripoti ya Kamati ya Wanasheria CCM haipo,” alisema Katibu huyo.

Alisema kama CCM ingehusika, basi ingetajwa miongoni mwa watuhumiwa waliohusika na wizi huo ambao sasa wanafikishwa mahakamani kujibu mashitaka.Alisema kama kuna mwanachama au kiongozi yeyote wa chama hicho tawala yumo kati ya watuhumiwa wa wizi wa EPA, basi yupo kama yeye na CCM haijamtuma mtu kushiriki kwenye wizi huo.

Aliwataka wananchi waache kuishinikiza serikali kuhusu suala hilo badala yake sasa aachiwe kazi hiyo Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), afanye kazi yake kwa mujibu wa sheria.Chiligati alimpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa hatua zote alizochukua kushughulikia suala la wizi wa fedha za EPA akisema ametimiza ahadi yake aliyotoa kwamba atawashughulikia wahusika.

“Kuna watu walibeza kwamba Rais hatawachukulia hatua wahusika, lakini kama tunavyojua mwanzoni mwa mwezi huu, watu wamefikishwa mahakamani,” alisema Chiligati ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Alisema Rais ndiye aliyeagiza uchunguzi ufanyike, akamfuta kazi Gavana wa BoT wakati huo, Dk. Daudi Balali na akaunda kamati ambayo ilitoa taarifa ambayo ilibainisha mambo mbalimbali.“Baada ya kupata orodha ya kampuni na watu waliohusika Rais aliwapa ilani wote waliohusika warudishe fedha hizo. Baadhi ya watu waliulaumu uamuzi huu wa kutaka warudishe fedha hizo, na uamuzi huu umezaa matunda,” alisema Chiligati.

Katibu huyo pia amewataka wananchi kutambua kuwa wizi wa fedha za EPA hauhusiani na Serikali ya Awamu ya Nne, bali Rais Kikwete anashughulikia matatizo yaliyofanywa zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Kwa mujibu wa hotuba ya Rais mwishoni mwa Oktoba mwaka huu, Sh bilioni 69.3 zilikuwa zimerudishwa kiasi ambacho sawa na asilimia 76 ya fedha zilizotakiwa kurudishwa. Jumla ya fedha zilizoibwa ni Sh bilioni 133.
 

Ni nani aliyethibitisha kwamba CCM haikuhusika na wizi wa EPA? Alifanya uchunguzi huo tangu lini mpaka lini? Na ripoti ya uchunguzi wake alikabidhiwa nani na lini?

Tunafahamu kwamba makampuni matatu ya Kagoda, Deep green na Mwananchi ambayo inasemekana baadhi ya mabilioni waliyochota toka EPA yalielekezwa CCM. Na makampuni hayo bado yanachunguzwa na DPP na timu yake, je, Chiligati uthibitisho huo kwamba CCM haikuhusika na wizi wa EPA kautoa wapi wakati uchunguzi bado unaendelea!?
 
Bubu,

Nilimiambieni mapema, EPA haihusiani na CCM ndio maana wamewafikisha mahakamani kina Lukaza na Jeetu Patel baada ya kujikagua kwa miezi sita kuhakikisha hakuna hata senti moja ya EPA ilikwenda CCM!

Jiulize kwa nini uchunguzi ulichukua muda mrefu kiasi hicho! Sababu kuu haikuwa ni kutafuta ushahidi wa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa, bali ni kutafuta kama kuna ka-ushahidi wa mikono ya CCM na wakubwa wake kuwa ndani ya chungu!
 

Mkuu Kishoka, wote tunajua kuwa hela za EPA zilihusika kwenye uchaguzi 2005 na ndio sababu ambayo utaona wazee wa kagoda mahakamani, na wakitokea ndio kweli nitajua JK kiboko.

Hawa waliofikishwa mahakamani sasa hivi hata kama walitoa hela kusaidia kwenye kampeni, walitoa kama michango tu ya matajiri wanaotoa hela kukisaidia chama tawala.
 
Yeah, right! and the Pope is not Catholic either.
 
Mafisadi wa EPA waitisha Serikali


*Wajipanga kuanika siri zote hadharani
*Vocha za malipo kwa CCM kuanikwa
*Kapt. Chiligati awakana, naye awatisha
*Asisitiza hakuna kikao kilichowatuma

Na Mwandishi Wetu

BAADHI ya watuhumiwa wa ufisadi kwenye Akaunti ya EPA iliyokuwa Benki Kuu (BoT) sasa wameamua kuitisha Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, uchunguzi wa Majira umebaini.

Kitisho hicho kimekuja kufuatia baadhi yao kukamwatwa na kufunguliwa kesi mbalimbali za jinai huku ikionekana kuwa wao walikuwa mawakala tu katika kupitisha fedha hizo na vigogo husika wakiwa nje.

Chanzo chetu kilicho karibu na baadhi ya watuhumiwa hao kilieleza kuwa kukamatwa, kufunguliwa mashitaka kumewadhalilisha sana baadhi yao huku wakiumia zaidi kwa kusota rumande, kwenye gereza la Keko na wale wanawake wakiweka Gereza la Wanawake Segerea.

"Jamaa ameumia sana rohoni, hata kuhangaikia dhamana alisita mwanzo baada ya kuona kwa nini ahangaike kutoa mali zake, wakati alikuwa wakala tu," kilisema chanzo chetu kilicho karibu ni mmoja wa watuhumiwa waliokwisha funguliwa kesi na akasota sana kwenye gereza la Keko.

Ingawa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa kikikana mara kadhaa kuhusika kunufaika na fedha hizo katika chaguzi mbalimbali, duru za uchunguzi, zinawakariri baadhi ya watuhumiwa hao wakilalamika 'kutolewa kafara.'

Ndugu mwingine wa mtuhumiwa ambaye ameshafanikiwa kwa kiasi kikubwa kulikwepa sakata la EPA, ingawa taarifa za kiuchunguzi bado zinaamini huenda akaburutwa naye kortini, aligusia kuwa kwa sababu yeye alitumiwa tu, ameandaa faili la utetezi ambalo pamoja na nyaraka nyingine, limeheheni kile alichokitaja kuwa vocha za malipo kwenda kwa baadhi ya vigogo wa CCM.

"Hapa ndipo Serikali itakapoumbuka. Kila kitu kipo. Hajakamatwa bado, ameshahojiwa na kubanwa katika shughuli zake, anasubiri tu afikishwe kortini atoe vielelezo vyake, yeye si fisadi, aliombwa asaidie shughuli halali akafanya hivyo, kwa namna anavyojiheshimu, asingeweza kusaidia akakubali wizi," kilisema chanzo chetu kilicholiona faili hilo la utetezi.

Wakati watuhumiwa hao wa EPA wakijipa 'kujiondoa katika ukafara,' Mwandishi Wetu Eckland Mwaffisi anaripoti kuwa uongozi wa juu wa CCM, umeendelea kusisitiza kuwa hawahusiki na ufisadi wa EPA.

Akitoa tamko kwa niaba ya Chama chake Dar es Salaam jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Bw. John Chilligati, alisema CCM haikuhusika na wizi huo kama ilivyodhibitishwa na ripoti ya kamati ya wanasheria.

Alisema pamoja na madai yanayotolewa na viongozi wa vyama vya upinzani, pasipo kuthibitisha madai hayo, CCM haikuchukua fedha hizo wala haikumtuma mwanachama wake au mkereketwa yoyote kwenda kuchukua fedha hizo katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Bw. Chilligati alisema pamoja na orodha ya watuhumiwa wa EPA kuhusisha majina ya wanachama wa CCM ama Wakereketwa, Chama hakijahusika kumtuma bali ni kitendo cha mtu binafsi.

Hadi sasa miongoni mwa waliokamatwa kwa tuhuma za wizi wa fedha za EPA wanaohusishwa na ukaribu na vigogo wa CCM au kuwa makada ni Bw. Rajabu Maranda na mfanyabiashara, Bw. Jeetu Patel.

"Kwenye ukweli, uongo hujitenga, madai yote ya kuihusisha CCM na ufisadi wa EPA ni uongo wenye nia ya kukivunjia heshima chama chetu machoni mwa jamii pamoja na hila za kuchafua jina la chama zinazofanywa na wapinzani ambazo kamwe, hazitafanikiwa," alisema Bw. Chilligati.

Kutokana na hali hiyo, Bw. Chilligati aliongeza kuwa, baadhi ya wanachama wanaokiuka maadili hayo, isichukuliwe kwamba wanatumwa na vikao vya chama bali ni vitendo vyao binafsi na watachukuliwa hatua za kisheria na vyombo vya dola kama ilivyo kwa wahalifu wengine.

Alisema CCM, inapongeza Rais Jakaya Kikwete kwa hatua alizozichukua katika kushughulikia sakata hilo.

Hadi wiki inayoanza leo, ambapo zipo tetesi za watuhumiwa zaidi kuanza kufikishwa kortini huku Mkurugenzi wa Mashitaka ya Umma (DPP), Bw. Eliezer Feleshi akikiri kuwa bado kuna mafaili yanapitiwa, idadi ya watuhumiwa waliokwishafikishwa kortini ni 20.

Baadhi ya makampuni ambayo yameshafikishwa mahakamani ni pamoja na Money Planners, Kiloloma & Brothers, Njake Hotel, Rashhas, Mibare Farm, Changanyikeni, Bencon International, Kernel, Malta Mining, Navy Cut Tobacco na BC Grassel & Company.

Makampuni yanayosubiriwa kwa hamu na wananchi katika Mahakama ya Kisutu ni pamoja na kampuni ya Kagoda ambayo inadaiwa kuchota fedha nyingi kulikoni kampuni nyingine.

Chanzo: Majira
Imetolewa mara ya mwisho: 17.11.2008 0022 EAT

HAPA CCM WATAJIKAANGA TU. MOVIE LINAENDELEA!
 
Date::11/16/2008
Mkurugenzi wa TAKUKURU, Dk Edward Hosea, anadai kutishiwa maisha kwa njia ya simu.
Na Exuper Kachenje
Mwananchi

MKURUGENZI wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hosea ameeleza kuwa amekuwa akipokea vitisho kutoka kwa watu mbalimbali wanaotuhumiwa kwa rushwa na ufisadi.

Hoseah amekuwa akitoa kauli za kijasiri katika siku za karibuni, ikiwemo kauli yake ya mapema wiki iliyopita kuwa iwapo serikali itawakamata kwa wakati mmoja watuhumiwa wote wa kashfa ya EPA, nchi inaweza kuyumba na juzi alitamka bayana kuwa wale wanaodhani vigogo hawapandishwi kizimbani kwa tuhuma za rushwa, wasubiri mwezi ujao.

Katika mahojiano na Mwananchi baada ya kufunga Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Mapambano Dhidi ya Rushwa kwenye Ukumbi wa Karimjee, Dk Hoseah alisema kuwa katika siku za karibuni amekuwa akipokea simu za vitisho na matusi kutoka kwa mafisadi, ingawa hakutaja ni kundi gani la mafisadi wanaofanya vitendo hivyo.

Hoseah alisema kuwa vitisho hivyo vimekuwa vikitolewa kwa nyakati tofauti na watuhumiwa hao ambao hutumia njia ya simu na ujumbe mfupi wa maandishi wa simu (sms)

"Vitisho vipo... napokea vitisho vingi kutoka kwa watu mbalimbali, kwa kutumia simu na sms ili nisifanye kazi ya kuwatumikia Watanzania ya kuwashughulikia watuhumiwa," alisema Dk Hoseah.

Dk Hoseah alisema kuwa pamoja na vitisho anavyopokea bado yupo imara katika kulitumikia taifa katika wajibu alionao na kwamba vitisho hivyo havimnyimi usingizi.

"Bwana mdogo, kama mimi nikiogopa na wewe (mwandishi) ufanyeje?," alisema Dk Hoseah akimhoji mwandishi wa Mwananchi na kuongeza kuwa iwapo ataogopa atakuwa hawatendei haki Watanzania.

Mkurugenzi huyo wa Takukuru alisema kuwa wakati mwingine amekuwa akipokea ujumbe wa sms wenye matusi ya nguoni juu yake na kwamba ameamua kutoyatilia maanani.

Kauli hiyo ya Dk Hoseah imekuja muda mfupi baada ya kueleza kuwa mwezi huu wa Novemba ndiyo mwisho wa mafisadi kutamba, kauli aliyoitoa katika kongamano hilo.

Dk Hoseah alikuwa akijibu kauli ya mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba aliyeonyesha mashaka kama kweli serikali ina dhamira ya kushughulikia wara rushwa wakubwa kwa kuwa hadi sasa hakuna kigogo aliyepandishwa kizimbani.

Katika kuonyesha msisitizo, Dk Hoseah, aliyekuwa mwenyekiti wa kongamano hilo, alirudia kutoa kauli hiyo katika hotuba yake fupi ya kufunga kongamano hilo ambalo lilifunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi, Sophia Simba.

Katika hotuba yake ya ufunguzi Waziri Simba alisema kuwa serikali ina nia ya dhati kumaliza maumivu ya rushwa yanayowakabili wananchi na itahakikisha inawezesha wadau kuendesha vita dhidi ya janga hilo.

Hadi sasa serikali imeshafikisha mahakamani watu 20 kwa tuhuma za kuiba fedha kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), lakini kati yao ni mfanyabiashara mmoja tu, Jeetu Patel, ambaye anaonekana kigogo kati ya watu maarufu wanaotajwa kuhusika kwenye kashfa hiyo.
 

ukipenda kula nawe ukubali kuliwa atiii, mafisadi hawana rafiki naona amesahau mafunzo aliyopitia watamuwahi tu maana nae hana msaada alishatuambia hakukua na rushwa kwenye issue za BOT sasa wanampigia simu za nini kujikosha tu wasituchanganye kwa kesi zipi za rushwa alizozifikisha mahakamani au kwa sababu wana JF tumesitisha issue zake kwa muda anataka kujikosha..................... wala simsikitikii
 
chapa kazi acha porojo... kwani hujui hiyo ni kazi nyeti?
 
kuna kitu sisiemu waliwahi kukubali wamekosea kwa maslahi ya taifa???
 
CCM sasa yahaha kujinasua wizi EPA

2008-11-17 10:28:00
Na Muhibu Said


Jinamizi la tuhuma za wizi wa mabilioni ya Shilingi katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BoT), limezidi kukinyima usingizi Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya chama hicho kuzidi kukanusha kuhusika, huku kikiwakana hadharani baadhi ya wanachama wake walioshtakiwa mahakamani kwa tuhuma za wizi huo.

Kwa mujibu wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni John Chiligati, wanaokihusisha chama hicho na tuhuma za wizi wa fedha hizo, ni viongozi wa vyama vya upinzani.

Hata hivyo, Chiligati, ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alikiri mmoja wa wanachama wa CCM, ambaye ni Mweka Hazina wa chama hicho, Rajabu Maranda kushtakiwa mahakamani kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa fedha hizo, lakini akasema zinamhusu yeye binafsi na kwamba, chama hakihusiki kwa vyovyote na tuhuma hizo.

Mara kwa mara CCM imekuwa ikikanusha kuzitumia fedha zilizoibwa Sh133 bilioni zilizoibwa BoT.

Pia, ametetea kitendo cha CCM kupokea Sh. milioni 400 kutoka kwa mfanyabiashara, Tanil Somaiya kwa ajili ya kufanikisha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), kitendo ambacho kililaaniwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba, ni ishara ya ya kukumbatia ufisadi kwa madai kwamba, fedha hizo zilipatikana kwa njia haramu.

Chiligati alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari, katika Ofisi Ndogo za CCM, Barabara ya Lumumba, jijini Dar es Salaam.

Alisema CCM inampongeza Rais Jakaya Kikwete kwa hatua zote alizochukua katika kushughulikia sakata la watu waliochota fedha kwenye EPA kinyume cha sheria, lakini imesikitishwa kwa namna viongozi wa vyama vya upinzani walivyokipaka matope chama hicho kupitia sakata hilo.

``Katika sakata hili la EPA, napenda kumalizia kwa kutoa masikitiko kwa jinsi viongozi wa vyama vya upinzani walivyokipaka matope Chama Cha Mapinduzi-CCM kupitia sakata la EPA. Lakini kwenye ukweli, uongo hujitenga,`` alisema Chiligati.

Alisema ukweli ni kwamba CCM haikuchukua fedha BoT na kwamba, hata ripoti ya Kamati ya Wanasheria, inaonyesha chama hicho hakihusiki.

``Tunasisitiza tena kwamba CCM haikuchukua fedha za BoT, na wala haikumtuma mtu yeyote awe mwanachama wetu au mkereketwa wa CCM akachukue fedha BoT. Na kama katika orodha ya watuhumiwa wa EPA, wapo wana CCM au wakereketwa wa chama hicho, ni kitendo cha mtu binafsi na asilani hawakutumwa na CCM,`` alisema Chiligati.

Alisema kutokana na hali hiyo, hoja zote za kuihusisha CCM na ufisadi uliofanywa kwenye EPA, ni uongo wenye nia ya kukivunjia heshima chama hicho machoni mwa jamii.

``Ni hila za kuchafua jina la CCM zinazofanywa na wapinzani wa CCM, ambazo kamwe hazitafanikiwa.

Historia ya CCM ni safi na itaendelea kuwa safi, isipokuwa baadhi ya wanachama wa CCM wanaokiuka maadili isichukuliwe kwamba wanatumwa na vikao vya CCM, ni vitendo vyao binafsi na wanachukuliwa hatua za kisheria na vyombo vya dola kama wahalifu wengine wowote,`` alisema Chiligati.

Alipotakiwa na waandishi wa habari katika mkutano huo jana aeleze miongoni mwa watuhumiwa wa wizi wa fedha za EPA waliofikishwa mahakamani hivi karibuni kama kuna mwanachama wa CCM anayemtambua, Chiligati alikiri kwamba, yupo na kumtaja kuwa ni Mweka Hazina wa chama hicho mkoani Kigoma, Rajabu Maranda, lakini akasisitiza kuwa suala hilo linamhusu yeye mwenyewe (Maranda).

Kuhusu taarifa zilizotolewa hivi karibuni kwenye vyombo vya habari kulaani mchango wa sh. milioni 400 zilizotolewa na mwanachama mkereketwa wa CCM, Tani Somaiya kwa ajili ya kufanikisha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), unaotarajiwa kufanyika Desemba 6, mwaka huu, Chiligati alisema chama kimeupokea msaada huo kwa mikono miwili na ndio maana ikalifanya suala hilo pasipo kificho.

Chiligati alisema wamelazimika kulizungumzia suala hilo, baada ya taarifa hizo kulaani kitendo cha CCM kupokea fedha kutoka kwa Somaiya, kwa madai kwamba, inapokea fedha hizo zilipatikana kwa njia haramu, ikiwamo rushwa na kukwepa kodi katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kwa hiyo, kitendo hicho kinaashiria chama hicho kukumbatia ufisadi.

``Tunapenda kuwahakikishia wana CCM na wananchi wote kwamba, CCM kupitia Umoja wa Vijana wa CCM imeupokea kwa mikono miwili msaada huo uliotolewa kwa Jumuiya ya Vijana na ndiyo maana ikalifanya suala hili hadharani pasipo kificho ili wananchi na wana CCM wote waweze kufahamu,`` alisema Chiligati.

Alisema kitendo cha misaada inayotolewa kwa vyama vya siasa kuwekwa hadharani, ni utamaduni mzuri na kuvitaka vyama vyote vya siasa nchini, vieleze hadharani michango wanayoipokea kutoka kwa wafadhili wa ndani na nje ya nchi.

Kuhusu madai kwamba, Somaiya anahusika na tuhuma za rushwa na kukwepa kodi za TRA, Chiligati alisema walio na ushahidi huo waupeleke katika vyombo vya dola.

``Tunavyofahamu sisi ni kwamba Bwana Tanil Somaiya kama mfanyabiashara anahitaji sana uwapo wa amani na utulivu ili aweze kufanikiwa katika biashara zake na ndiyo maana amejitolea kwa hiari yake mwenyewe kuchangia katika chama kinachosimamia na kufanikisha mazingira ya amani na utulivu,`` alisema Chilig
 
Hii ni litimus test kwa Watanzania. Jee kweli CCM watauza hii idea yao kwamba EPA haina mausiano na CCM?

Hii story inaonyesha ni jinsi gani maamuzi ya kuwaswaga ndani kina Lukaza ni more political kuliko law and order. CCM wanaoneka kuwa na strategy behind the door jinsi ya kufuta hii agenda ya EPA kwenye runoff ya 2010.

I think wapo baadhi ya Watanzania watakao rudi kundini sababu ya hii kesi feki ya EPA na hao ndio CCM inawo wa target.
 
tUSIJIHAMII sanaaa maana TUtaumiza vichwa TUSHIndwe kushughulikia matatizo ya wananchi bure sisi tunajua CCM hawahusiki wanaCCM ndo wanaohusika ati sasa TUwanyang'anye uanaCCM kwa kuharibu jina la chama kwani katiba yetu inaongeleaje/ kuhusu wezi na wachafuaji jina la chama chetu tukufu tulichosema kidumu toka miaka hiyo na kitaendelea kudumu???????????? Makamba nakutuma kila ambaye alihusika either kwenye issue ya EPA, Richmond, au kiwira, meremeta,buzwagi, BOT, na nimwanaCCM anyang'anywe uanachama mara moja hata kama ni rais makamu wa rais au waziri mkuu mbunge na hata wakuu wa dini ili tuweze kulinda chama chetu, KUMBUKENI INATUBIDI TUFANYE HIVI TU KWA KULINDA JINA LA CHAMA CHETU MTUSAMEHE

TEHETEHE TUNAWEZA BAKI NA WANACHAMA50 LAKINI TUTAINGIZA WENGINE MILIONI 34 KWA SIKU MOJA TU HATA MBOWE MTIKILA NA SLAA WATAHAMIA KWETU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…