EPA na mambo yake

EPA na mambo yake

wakati mnazitumia na kuchekelea mlikuwa hamjui zitatumika kwenye mdhamana!!!
nexty tym muwe makini
 
Hivi hii thread imewekwa ili tuwaonee huruma kwa kushindwa kutimiza mashariti ya dhamana au imewekwa kwa sababu zipi?

JF si sehemu ya kutetea uovu, waache waozee huko huko, maana hata mtaani hatuwataki. Au na wewe unaye ndugu yako huko?
 
Hivi hii thread imewekwa ili tuwaonee huruma kwa kushindwa kutimiza mashariti ya dhamana au imewekwa kwa sababu zipi?

JF si sehemu ya kutetea uovu, waache waozee huko huko, maana hata mtaani hatuwataki. Au na wewe unaye ndugu yako huko?

DHAMANA NI HAKI YAO. Punguzeni chuki, kama hela ya EPA inakuuma mbona hupi kelele hela walizochukuw CCM kwa mgongo wa kagoda uchaguzi wa 2000 na 2005 EPA ilitumika kuua demokrasia nchini, hao waliokamatwa ni vichuguu vilivyofuata nyayo za mlima kilimanjaro (CCM & RAs)
 
Hivi hii thread imewekwa ili tuwaonee huruma kwa kushindwa kutimiza mashariti ya dhamana au imewekwa kwa sababu zipi?

JF si sehemu ya kutetea uovu, waache waozee huko huko, maana hata mtaani hatuwataki. Au na wewe unaye ndugu yako huko?
..Safi sana kashaija, mi pia sina huruma nao hata kidogo ulafi wao umetusababishia madhira mengi tu wangeendelea tu kunyea debe kwanza watie akili....
 
Hatustahili kuwa wapungufu wa fikira eti tu kwa sababu tunapiga vita ufisadi!!! Nasema ni vema hao jamaa nao wakaangaliwa kwa jicho hilohilo la kifisadi, maana si vema kwao kuanza kuleta monopoly ktk kuhakiki nyaraka za hao watuhumiwa, ni vema jf irejee kwa kutambua kuwa ktk maeneo ambayo yamekuwa kero ni aina hii ya huduma nyoronyoro ambayo mwishowe watu wanahongwa ili watoe hizo data kwa mahakama ili haki ya dhamana itendeke.

Suala si huruma bali mabadiliko kiutendaji ktk kumhudumia mwananchi yeyote yule bila kujali hali yake.
Change waungwana
 
Kwani hela zote wamezichezea ni wapuimbavu kiasi hicho Alafu kwa nini hawakukimbia nchi hivi hawa wezi ni wa aina gani jamani mimi sijasikia wezi wajinga hivi ha ha ha ha au waliambiwa nothing will happen to them they own the country. Thats why we here the economi will go down Please what economy. Tanzanians have the right to very angry they are being played like toys.
 
Nyie si mna hela wapeni hongo kama mlivyohonga kupata hizo Hela za EPA. Au mghushi hizo documents.

Ila poleni sana
 
Jamani hii ni habari ya kuskitisha sana kama si kusosononesha watanzania kumbe ukiiba pesa nyingi unheshimika mpaka jela!!!
Wale wahalifu wa epa wanishi maisha ya peponi,inasemekana wako katika vyumba bora kabisa na vitanda murua wanachomiss haswa ni wake zao na hivyo kuwaongezea hamu !!!gazeti la nipashe linasema hata yule rijali wetu """zombe ""nae anishi room hizo hizo

babu,kubwa!!!
 
Haya Rostam tena huyooooo!!!! Na tuone kama watamgusa

Raia Mwema - Siri mpya ya EPA yaiumbua Kagoda

http://www.raiamwema.co.tz/images/P/8/1112/nyaraka.jpg

Siri mpya ya EPA yaiumbua Kagoda

Mwandishi Wetu
Novemba 12, 2008

WAKATI watuhumiwa 20 wakiwa, hadi juzi, wamekwisha kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), ushahidi mpya umeibuliwa unaoonyesha kwamba kampuni ya Kagoda Agricultural Limited, ambayo wahusika wake bado hawajashitakiwa, ilikuwa ya kwanza kuchota mapesa hayo zaidi ya miaka minane iliyopita.

Uchunguzi wa muda mrefu wa Raia Mwema umethibitisha kuwapo kwa uhusiano mkubwa kati ya kampuni ya Afritainer (T) Limited na kampuni ya Kagoda Agricultural Limited ambayo hadi sasa wahusika wake na mahali ilipo ni kitendawili.

Kampuni ya Afritainer ilifanikiwa kuchota zaidi ya Shilingi bilioni 12 za EPA kwa kutumia nyaraka zilizosainiwa na watumishi wa kampuni moja maarufu ya Dar es Salaam (jina tunalo) wakidaiwa kuwa wakurugenzi wa kampuni hiyo kabla ya kufahamika kwamba hawakuwa wakurugenzi halali kisheria.

Kagoda, ambayo ilitumia nyaraka za kughushi, ilichotewa mabilioni hayo ya fedha kabla haijasajiliwa na katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Hadi sasa hakuna taarifa rasmi zinazoonyesha watu waliorejesha fedha za EPA kwa jina la Kagoda pamoja na kuwapo taarifa za uhakika kuhusiana na wafanyabiashara wazito waliorejesha fedha hizo kwa nyakati tofauti kabla ya muda uliowekwa kwisha Oktoba 31, 2008.

Nyaraka zilizotumiwa na Afritainer kuchota mabilioni ya fedha za EPA mwaka 2000 zinaonyesha kwamba kampuni hiyo imetumia namba za simu 2861371 na 2861372 ambazo pia ndizo zimetumiwa na Kagoda katika kuchota fedha za EPA mwaka 2005. Namba hizo zinaonekana katika nyaraka za kampuni nyingine yenye uhusiano na wamiliki wa Afritainer.

Nyaraka kutoka Wakala wa Usajili wa Makampuni na Leseni (BRELA) zinaonyesha kwamba Tabu Omari Masula na Barati A. Goda, walidaiwa kuingizwa kuwa wakurugenzi wa kampuni hiyo Mei 15, 2000 kinyume cha sheria.

Barua ya BRELA ya Februarin 18, 2002, miaka miwili baada ya Tabu na Barati kuchota fedha za EPA, ilieleza kwamba wakurugenzi hao hawakuwa halali kutokana na kutokuwa na hisa katika kampuni ya Afritainer.

Kwa mujibu wa barua hiyo kwenda kwa kampuni ya mawakili ya M.A.Imail, Tabu na Barati walikiuka kifungu cha 50 cha hati ya usajili ya kampuni hiyo kinachomlazimu mkurugenzi kuwa na hisa katika kampuni kwanza ili aweze kuwa na maamuzi.

Waraka wa Afritainer uliowasilishwa BRELA Mei 15, 2000, ulieleza kwamba wakurugenzi pekee na waazilishi wa Afritainer ni Bahram Abdurasul Chakaar na Gulam Abdurasul Chakaar, wamejiuzulu ukurugenzi na kuwaachia Tabu na Barat.

Hata hivyo, BRELA katika barua ya Februari 18, 2002 iliyoandikwa na Msajili Msaidizi wa wakala huo, L. Kimaro, ilieleza wazi kwamba hadi wakati huo ubadilishaji wa wakurugenzi haukuwa umeidhinishwa kutokana na kutokufuata masharti ya usajili.

Tabu anatajwa kufanya kazi katika kampuni moja ya jijini Dar es Salaam yenye ofisi zake eneo la viwanda barabara ya Nyerere na Upanga.

Kwa mujibu wa habari ambazo Raia Mwema imezipata fedha hizo kiasi cha Sh. Bilioni 13 zilichukuliwa Agosti 2000 kabla ya uchaguzi wa pili wa vyama vingi ambao Benjamin Mkapa aligombea tena urais.

Waidhinishaji wakuu wa mikataba ya uchukuaji wa fedha hizo walikuwa ni mawakili maarufu wa kampuni ya uwakili ya Law Associates chini ya mkuu wake Dk. Ringo Tenga. Dk. Tenga sasa ni mwanasheria wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Nyaraka za uchukuaji wa fedha hizo mwaka 2000 zinaonyesha kwamba benki ya Akiba Bank ilitumika kupitishia fedha hizo kutokea BoT.

Haikuweza kufahamika mara moja kama vyombo vya dola vimefanikisha kupata nyaraka husika, pamoja na kuwapo taarifa kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ilikwishachunguza nyaraka hizo ikiwa ni pamoja na kuwahoji watumishi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kuhusiana na na matumizi ya namba za simu 2861372 na fax zilizotumiwa na kampuni ya Afritainer na Kagoda Agricultural.

Kwa sasa wafuatiliaji wa sakata la EPA wanasubiri wahusika wa kampuni ya Kagoda Agricultural Limited iliyochota Sh bilioni 40 kufikishwa mahakamani baada ya kufikishwa kwa watuhumiwa wengine 20 hadi sasa.

Tayari inafahamika kwamba kati ya shilingi bilioni 90 zilizoibwa katika akaunti ya EPA, sehemu kubwa ilichukuliwa na kampuni ya Kagoda Agricultural Limited ambayo hadi sasa wahusika wake hawajaguswa pamoja na kujitokeza kwa vigogo wawili kurejesha fedha zilizoibwa na kampuni hiyo.

Vyanzo vya uhakika vinaeleza kwamba sehemu kubwa ya Shilingi bilioni 90 zilizothibitika kuchukuliwa kihalifu zilichukuliwa na makundi mawili tu, kundi la kwanza likiwa chini ya Jeetu Patel na lingine likiwa chini ya usimamizi wa vigogo wawili waliotumia kampuni ya Kagoda.

Imefahamika kwamba kwa sasa kuna hekaheka kubwa za kutaka kuzuia kushitakiwa kwa wahusika wa Kagoda, lakini vyanzo vya ndani ya serikali vimeeleza kwamba kwa sasa serikali haitabiriki na lolote linaweza kutokea wakati wowote kabla ya mwisho wa mwaka.

Kumekuwa na utata kuhusiana na ilipo na umiliki wa Kagoda Agricultural Limited ambayo imethibitika kujichotea kiasi cha Dola za Marekani 30,732,658.82 (zaidi ya Sh Bilioni 40/-) kutoka akaunti ya EPA na hakuna anayeweza kubainisha hasa zilipo ofisi na wahusika wa kampuni hiyo tata.

Kumbukumbu za BRELA zinaonyesha kwamba ofisi zake zipo Kipawa Industrial Area Plot namba 87, Temeke, Dar es Salaam lakini eneo hilo lina makampuni tofauti jirani lakini namba iliyotajwa haionekani na badala yake eneo lenye ofisi na kampuni viwanja vyenye namba 77, 86 na 88 katika eneo hilo la viwanda.

Katika ukaguzi wake wa awali wa mkaguzi wa nje Samuel Sithole kutoka kampuni ya Kimataifa ya Deloitte & Touche yenye makao yake Afrika Kusini alionya kuhusu matendo ya kihalifu ndani ya Kagoda kabla ya kuandikiwa barua na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji kwamba fedha hizo zilienda katika mambo "nyeti" ya kiusalama.

Hata hivyo siku nne baada ya kuandika barua hiyo, Meghji alifuta barua hiyo akielezea kupotoshwa na aliyekua Gavana, Dk. Daudi Ballali, uamuzi ambao ulimgharimu kwa kiasi kikubwa mwanamama huyo makini ambaye alijikuta akiachwa nje ya Baraza la Mawaziri.

Wakati Rais Jakaya Kikwete akisema serikali yake haitomuingilia Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), watuhumiwa wengi walikamatwa na kufikishwa mahakamani walikuwa wamejiaminisha kuwa wamekwishapona na sasa waliobaki "hawalali" kuhofia kushitukizwa na kupandishwa kizimbani.

Tayari watu 20 wamekwisha kufikishwa mahakamani baada ya wafanyabiashara watatu kufikishwa mahakamani Jumatatu wiki hii wakitanguliwa na watuhumiwa wengine wakiwamo watumishi wa BoT waliohusika katika mchakato wa wizi huo.

Waliopandishwa kizimbani Jumatatu ni Ajay Somani na Jai Somani wanaodaiwa kula njama ya wizi wakiwa na watu wengine ambao hawajafahamika kuiibia BoT na kwamba Septemba 2, 2005 waliiba Sh. bilioni 5.9 mali ya benki hiyo.

Mtuhumiwa mwingine aliyefikishwa Jumatatu ni mfanyabiashara Mwesiga Lukaza, aliyepandishwa kizimbani akiunganishwa na mshtakiwa mwingine Johnson Lukaza, ambaye alishapandishwa kizimbani mapema wiki hii.

Watuhumiwa wengine ambao tayari wamefikishwa mahakamani ni Farijala Hussein, Rajab Maranda, Japhet Lema, Bahati Mahenge, Davis Kamungu, Godfrey Mosha, Manase Mwakale na Eddah Mwakale, Devendra Vinodbhai Patel, Amit Nandy, Ketan Chohan, Jayantkumar Chandubahi Patel na Johnson Lukaza.

Wengine ni wafanyakazi wa BoT ambao ni Mkuu wa Idara ya Madeni ya Biashara, Iman David Mwakyosa, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Madeni, Ester Mary Komu na makaimu Katibu wa benki wawili ambao ni Bosco Ndimbo Kimela na Sofia Joseph Lakila.

Kati ya watuhumiwa hao, ni wawili tu ambao wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana hiyo ambao ni Godfrey Mosha na Davis Kamungu. Washitakiwa wengine licha ya dhamana zao kuwa wazi, wanaendelea kusota rumande kutokana na kushindwa kutimiza masharti.
 
Watuhumiwa wa EPA waponda raha Keko

2008-11-13 10:21:29
Na Joseph Mwendapole

Washitakiwa 18 wanaokabiliwa na mashitaka tofauti ikiwemo kughushi na kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wanaishi katika vyumba maalum (VIP) katika gereza la Keko tofauti na mahabusu wengine.

Uchunguzi wa Nipashe umebaini kuwa, baadhi ya washitakiwa hao wamewekwa katika vyumba maalum (VIP) katika gereza la Keko ambapo wametengwa kabisa na maabusu wa kawaida maarufu kama walalahoi.

Chanzo cha gazeti hili kilielezwa kuwa, Jayantkumar Patel maarufu kama Jeetu Patel na Jonson Lukaza, wanaishi katika vyumba vya VIP, ambapo Jeetu Patel inadaiwa kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu huku Lukaza akidaiwa kuwa na maradhi kama hayo pia.

Hata hivyo, Ofisa Uhusiano wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Omari Mtega aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu jna kuwa, katika magereza yote hapa nchini, hakuna vyumba vya VIP.

Kamishna Mtega alisema ni jukumu la Magereza kuhakikisha ulinzi na usalama wa wahalifu hivyo ni muhimu walindwe kwa utaratibu waliojiwekea.

Aliongeza kuwa, jamii nzima inawachukia watuhumiwa wa EPA hivyo jeshi hilo haliwezi kufanya uzembe kwa kuwachanganya na watuhumiwa wa makosa mengine.

``Unasikia mwandishi, `EPA is EPA`kwa hiyo sio jukumu la vyombo vya habari kujua usalama wa watuhumiwa na wanalindwaje na hatuwezi kuwachanganya na watuhumiwa wengine kwa kuwa wanaweza wakauawa na lawama zikaenda kwa jeshi,`` alisema.

Aliongeza kuwa, mahabusu ambao ni watuhumiwa sugu kwa makosa tofauti, hawachanganywi na wale wanaofikishwa gerezani kwa mara ya kwanza.

``Kwa mfano, ili kuimarisha ulinzi na usalama wa watuhumiwa gerezani, jeshi haliwezi kufanya makosa kwa kuwachanganya na Abdallah Zombe kwa sababu wanaweza kumdhuru au hata kumuua hasa wale waliokamatwa kwa tuhuma mbalimbali kabla Zombe hajakamatwa kwa tuhuma za mauaji,`` alifafanua Kamishna Mtega.

Baadhi ya masharti ya dhamana ambayo wamekuwa wakipewa ni pamoja na kulipa nusu ya fedha wanazodaiwa kuiba BoT au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Sharti lingine ni kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali, kuwasilisha hati za kusafiria na kuripoti polisi kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi na kutosafiri nje ya Dar es Salaam bila kibali cha Mahakama.

Hivi karibuni, gazeti moja liliripoti kuwa, serikali ilikuwa ikifanyia ukarabati vyumba vya VIP kwa ajili ya vigogo waliotarajiwa kufunguliwa mashitaka kutokana na wizi uliotokea BoT.

Hata hivyo, baada ya taarifa hizo, serikali ilikuja juu na kukanusha kuwa ukarabati huo haufanywi kwa ajili ya vigogo bali ni taratibu za kawaida wamewekwa katika vyumba maalum (VIP) katika gereza la Keko ambapo wametengwa kabisa na mahabusu wa kawaida maarufu kama walalahoi.

Chanzo cha gazeti hili kilielezwa kuwa, Jayantkumar Patel maarufu kama Jeetu Patel na Jonson Lukaza, wanaishi katika vyumba vya VIP, ambapo Jeetu Patel inadaiwa kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu huku Lukaza akidaiwa kuwa na maradhi kama hayo pia.

Hata hivyo, Ofisa Uhusiano wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Omari Mtega aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu jna kuwa, katika magereza yote hapa nchini, hakuna vyumba vya VIP.

Kamishna Mtega alisema ni jukumu la Magereza kuhakikisha ulinzi na usalama wa wahalifu hivyo ni muhimu walindwe kwa utaratibu waliojiwekea.

Aliongeza kuwa, jamii nzima inawachukia watuhumiwa wa EPA hivyo jeshi hilo haliwezi kufanya uzembe kwa kuwachanganya na watuhumiwa wa makosa mengine.

SOURCE: Nipashe
 
usishangae hilo peke yake. watuhumiwa wengine wakikosa wadhamini, hupelekwa gerezani na kungojea siku zisizopungua 14 kesi itakapotajwa tena ndio suala la dhamana lizungumzwe. hawa, kila siku wanarudishwa mahakamani kuangalia kama masharti ya dhamana yametimia. leo nasikia wawili wengine wametimiza masharti ya dhamana na sasa wako nje. ndio haki hiyo!!!

macikus
 
Kwani hela zote wamezichezea ni wapuimbavu kiasi hicho Alafu kwa nini hawakukimbia nchi hivi hawa wezi ni wa aina gani jamani mimi sijasikia wezi wajinga hivi ha ha ha ha au waliambiwa nothing will happen to them they own the country. Thats why we here the economi will go down Please what economy. Tanzanians have the right to very angry they are being played like toys.


Kwa nini wachechetuke kukimbia wakati wadanganyika wakiongozwa na KJ ndio wajinga wao?
 
Haya Rostam tena huyooooo!!!! Na tuone kama watamgusa

Halisi
Rostam Aziz ingekuwa dawa...ingetibu magonjwa mengi zaidi ya mwarobaini ila kwa sababu RA ni sumu, ubaya wake unazidi wa arsenic!
 
Mheshimiwa Dr. Slaa,

Labda ututengenezee timeline ya suala la EPA vinginevyo naona kumhusisha prof. Ndullu
ni makosa kwasababu timeline inakataa.

Nijuavyo mimi prof. Ndullu alichaguliwa kuwa naibu Gavana baada au siku chache kabla ya Dr. Ballali kukimbilia USA. Kama ninavyojua mimi ni sahihi, basi, yeye hakuwepo BOT wakati hizo pesa zinachotwa.

Anayejua tarehe kamili ambayo prof. Ndulu aliteuliwa kuwa naibu gavana naomba atufahamishe.


Dr. na Mheshimiwa Dr. Slaa. Pamoja na kwamba sikumbuki tarehe rasmi ya uteuzi wa Prof.Ndulu kuwa governor ni kwamba Prof. Nduli hausiki kabisa na sakata la EPA.

Kwa taarifa za uhakika ni kwamba, Prof. Ndulu lilikuwa ni pendekezo la World Bank kwa kuwa Beno alikuwa yuko hapa WB Office Dar na baadaye HQ W. DC ndipo alipotakiwa aje hapa TZ. Alichofanya Rais ni kumfanya Naibu huku akisubiri namna ya kumaliza term ya Balali. Ndulu alitoka D,C akiwa na taarifa zote kuwa anakuja kuwa Governor wa Benki. Kilichokuwa kinasubiriwa ni muda tu.

Wakati anakuwa governor soo la EPA tayari siku nyingi. Hata Annual Report ya BOT 2006 ilichelewa sana kuchapwa kwa sababu hiyo na sielewi kama mpaka sasa imeshachapwa. Nakumbuka kuna habari zilitakiwa kutoka ndani ya ripoti hiyo ili kuandika dicument fulani lakini kila ofisa au mkurugenzi aliyeulizwa kuhusu report alijibu "iko mezani kwa gavana!!!!? Tuwe just katika kuhukumu wengine. Habari ndo hiyo.
 
Haya Rostam tena huyooooo!!!! Na tuone kama watamgusa

Halisi
Rostam Aziz ingekuwa dawa...ingetibu magonjwa mengi zaidi ya mwarobaini ila kwa sababu RA ni sumu, ubaya wake unazidi wa arsenic!

Tehe tehe kazi kweli kweli hili ndo tatizo la kujificha kwenye kichaka biala kujua kwamba mwenyeshamba atakuja kufyeka siku moja. Inavyoonekana Rostam na Manji biashara zao zimejengwa katika msingi wa "ma-deal" ya wizi, rushwa, hongo na ufisadi wa kila aina yaani EPA, CIS, Richmond, etc.

Ingekuwa heri polisi wetu wangekuwa na uwezo, wangeanzisha uchunguzi mahususi kwa ajili ya hawa jamaa na biashara zao. Bila shaka wangegundua mambo mengi sana. Lakini ni Tanzania yetu aise polisi wanasubiri amri ya Rais au Waziri Mkuu.
 
Ingekuwa heri polisi wetu wangekuwa na uwezo, wangeanzisha uchunguzi mahususi kwa ajili ya hawa jamaa na biashara zao. Bila shaka wangegundua mambo mengi sana. Lakini ni Tanzania yetu aise polisi wanasubiri amri ya Rais au Waziri Mkuu.

Asikudanganye mtu Nziku
Mifumo ya usalama ya Tanzania inajua sana tena sana kila kinachotokea...tatizo ni njaa+tamaa=rushwa, kulindana na uswahiba...historia inaonesha KJ anaongoza kwa uswahiba wa hatari kwa Taifa ... tunaweza kutoka na theory mpaya ya uswahiba...
 
Jamani hii ni habari ya kuskitisha sana kama si kusosononesha watanzania kumbe ukiiba pesa nyingi unheshimika mpaka jela!!!
Wale wahalifu wa epa wanishi maisha ya peponi,inasemekana wako katika vyumba bora kabisa na vitanda murua wanachomiss haswa ni wake zao na hivyo kuwaongezea hamu !!!gazeti la nipashe linasema hata yule rijali wetu """zombe ""nae anishi room hizo hizo

babu,kubwa!!!

Lazima tufike mahali tupiginie hata hili kwani wao ni nani mpaka wakae V.I.P? mbona wengine wanachanganywa. Na hapa ndipo inapoonyesha dhamira ya wazi kwa serikali hii ya KIFISADI kuwatetea wahalifu wanaoigusa. Tuanzishe mapambano mengine nao wakaonje selo la kawaida ili watoto wa Keko na wapi sijui nao wawafaidi ili wajue utamu wa selo na wakitoka wakawaonyeshe wake zao na watoto maana wanaweza kuishia kushitakiwa na baada ya uchaguzi wakaachiwa hawa.
 
Hivi kuna ukweli kwenye hii habari kwamba wanalala vyumba vya VIP? Ama watu tu wanadhani hivyo. Kuna wengine wanadai kwamba hawa jamaa wanapelekwa makwao usiku na kurejeshwa asubuhi. Ukweli ni upi? Na kuna evidence gani?
 
hILO LA LURUDISHWA USIKU HALIPO KABISA.....TENA FUTA USEMI WAKO....SUALA NI KULETWA KILA SIKU AJILI YA DHAMANA INGAWA NAJUA NI HAKI YAO MAANA DHAMANA IKO WAZI...KAMA INGEFUNGWA WASINGELETWA....HATA WEWE KABWELA KAMA MIMI TUTAFANYIWA HIVYO,KULETWA KILA SIKU...KAMA WADHAMINI WETU WATAKUWA WANAKAMILISHA MASHARTI BASI REMOVAL ORDER INATUMWA GEREZANI....NA UNALETWA
 
hILO LA LURUDISHWA USIKU HALIPO KABISA.....TENA FUTA USEMI WAKO....SUALA NI KULETWA KILA SIKU AJILI YA DHAMANA INGAWA NAJUA NI HAKI YAO MAANA DHAMANA IKO WAZI...KAMA INGEFUNGWA WASINGELETWA....HATA WEWE KABWELA KAMA MIMI TUTAFANYIWA HIVYO,KULETWA KILA SIKU...KAMA WADHAMINI WETU WATAKUWA WANAKAMILISHA MASHARTI BASI REMOVAL ORDER INATUMWA GEREZANI....NA UNALETWA

Kinachozungumziwa hapa ni usawa mbele ya sheria. .Hapa kuna double standards na ndicho kinacholalamikiwa na siyo ati kwanini wanapewa dhamana.
Kiutaratibu, kesi hutajwa kila baada ya siku kumi na nne.Na hapo ndipo uamuzi wa masuala yote yanayomhusu mshtakiwa ikiwa ni pamoja na kuangalia kama masharti ya dhamana yametekelezwa hufanyika.Kinachoshangaza kama ni kweli ni hili la washtakiwa wa EPA kurudishwarudishwa mahakamani kabla ya huo muda ati kwa kile kinachosemekana kuwa masharti ya dhamana yametekelezwa. Hii inaleta dhana kuwa hawa jamaa wanatendewa tofauti na washtakiwa wengine.
 
Back
Top Bottom