EPA na mambo yake

EPA na mambo yake

The Mafia establishment is fond of the saying "Dead men tell no tales".
 
AAH.. hawa watu mbuzi kweli... inamaana watanzania hatuna sauti yakupigakelele?
 
Mahakimu wahofu usalama kesi za EPA
Shadrack Sagati
Daily News; Friday,November 14, 2008 @21:15

Mahakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam ambako kesi za ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinasikilizwa, wamehofia usalama wao; hali iliyowalazimu kuomba kupatiwa ulinzi wa polisi.

Mahakimu hao wanadai wamepewa dhamana ya kuendesha kesi hizo kubwa wakati usalama wao ni mdogo kutokana na kutokuwa na usafiri, hali inayowalazimu wakimaliza kuendesha kesi hizo wapande daladala. Malalamiko mengine ya mahakimu hao ni kutolipwa posho na Idara ya Mahakama wakati mwingine wanalazimika kuendesha kesi hizo nje ya muda wa kazi kutokana na unyeti wa suala hilo.

Lakini pia wanadai mazingira ya mahakama yenyewe ya Kisutu haiko katika hali nzuri ya usafi, kwani licha ya kuwa ni padogo, lakini kutokana na msongamano wa watu ndani ya vyumba vya mahakama, kunakuwa na harufu mbaya. Mahakimu hao wanadai majengo ya mahakama hiyo yalivyo yanawalazimu wanapomaliza kusikiliza kesi hiyo, kupishana na watu mabarazani, jambo ambalo wanadai sio zuri kwa usalama wao.

Kutokana na malalamiko hayo jana, mahakimu hao walisitisha shughuli za mahakama na kwenda kukutana na uongozi wa Mahakama Kanda ya Dar es Salaam kuwasilisha malalamiko yao mbalimbali yanayohusu kesi hizo. Walirejea mahakamani hapo saa sita mchana ndipo wakaendelea na kesi mbalimbali, lakini baadaye tena walikatisha kusikiliza kesi hizo baada ya viongozi wa Mahakama Kuu na Rufaa kwenda kukutana nao tena.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Semistocles Kaijage alikiri mahakimu hao kufanya kikao jana na Msajili wa Mahakama ya Rufaa. Jaji Kaijage alisema suala la usalama tayari limeshashughulikiwa kwani wamelazimika kulipeleka Polisi. “Unajua mahakama sio chombo cha kutoa ulinzi, lakini tunashukuru Polisi imekubali kutoa ulinzi kwa mahakimu wetu,” alisema Kaijage na kuongeza:

“IGP ametuthibitishia kuwa suala hilo atalifanyia kazi ili kuhakikisha ulinzi kwa mahakimu.” Alisema masuala mengine yanayohusu fedha yanashughulikiwa na wasajili wa Mahakama Kuu Kanda na wa Mahakama ya Rufaa. “Hilo siwezi kulizungumzia kwani linashughulikiwa na wasajili wote wawili, waulize watakufafanulia vizuri, si unajua hayo ni masuala ya fedha za Serikali,” alisema Jaji Kaijage.

Baada ya kikao na mahakimu hao, gazeti hili lilimtafuta Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Ferdinand Wambari ambaye alisema suala lilikuwa ni ulinzi wa kutosha mahakamani hasa kutokana na watu kuwa wengi wakati wa kuendesha kesi hizo. “Tumewahakikishia kuwa tutajitahidi kuwasiliana na mamlaka zinazohusika kuwapo na ulinzi wa kutosha wakati kesi zinaendelea,” alisema Wambari.

Pia alisema kwa kuwa kesi zenyewe wakati mwingine zinamalizika baada ya muda wa kazi, suala la ulinzi kwa mahakimu nalo wamelizingatia pamoja na wadau wengine wanaokuwapo mahakamani muda huo. “Tumewahakikishia kuwepo kwa usalama wa kutosha sio kwa mahakimu tu, pia na kwa wadau wengine,” alisema.

Kuhusu suala la usafiri, alisema Idara ya Mahakama pia imelizingatia hilo ili kuhakikisha wanapomaliza kesi hizo kuwepo na usafiri wa kuwarejesha majumbani kwao. Alisisitiza pia amewataka mahakimu hao kuhakikisha kuwa kesi za EPA haziathiri uendeshaji wa kesi n yingine kama za madai na jinai.

Naye Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Eliezer Feleshi amewataka wananchi waiachie ofisi yake kushughulikia kesi za mafisadi wa mabilioni ya fedha yaliyochotwa katika EPA. Feleshi katika taarifa yake ya jana kwa vyombo vya habari, alifafanua kuwa licha ya kuwa ofisi yake ni ya umma, lakini inafanya kazi bila kuingiliwa na mtu au mamlaka yo yote.

“Kwa misingi hiyo ninawaomba wananchi kuwa na subira na kuiacha ofisi kufanya kazi yake kwa mujibu wa sheria,” alisema Feleshi. Alisema majalada yote yanayohusiana na EPA yamewasilishwa kwake na yanaendelea kufanyiwa kazi. “Kama mnavyoshuhudia baadhi ya watuhumiwa wamepelekwa mahakamani. Kwa majalada ambayo yanahitaji uchunguzi zaidi, yanaendelea kufanyiwa kazi kama nilivyoelekeza vyombo vya uchunguzi.

Ni kwa msingi hiyo, ninawaomba wananchi kuwa na subira na kuiacha Ofisi kufanya kazi yake kwa mujibu wa sheria,” alisema Mkurugenzi wa Mashitaka. Tayari DPP ameshawafikisha mahakamani watuhumiwa 20 wakiwamo wamiliki wa kampuni 12 pamoja na maofisa wanne wa BoT wanaodaiwa kushirikiana na watuhumiwa hao kufanya ufisadi.

Wakati huo huo, watuhumiwa wengine wawili jana walipata dhamana baada ya kutimiza masharti waliyopewa. Watuhumiwa hao ni ndugu wawili ambao ni Johnson Lukaza na Mwesigwa Lukaza. Hakimu Mkuu Mkazi Euphemia Mingi alitoa dhamana hiyo baada ya kuridhika na hati zilizowasilishwa jana zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 3.1.

Ndugu hao wawili wanatuhumiwa kuiba Sh bilioni 6.3 kwa kutumia kampuni yao ya Karnel Ltd. Washitakiwa sita kati ya 20, wameshapata dhamana. Washitakiwa hao ni Godfrey Mosha na Davis Kamungu, Manase Mwakale na mkewe Eddah Mwakale waliodhaminiwa baada ya kutimiza masharti ya kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika kwa kila mshitakiwa yenye thamani ya Sh milioni 240.
 
Hivi hao vogogo ndio tuliowapa mtaji wa kujenga pale ilipokuwa salamander?
 
Wanaweza kwepa kwenda kisutu, Je wanaweza kukwepa mshale wangu wa sumu ya kimakonde?
Dawa ya mijitu kama hii ni kuimaliza kimya kimya kwa kujipenyeza kwenye udhaifu wao.
 
Wanaweza kwepa kwenda kisutu, Je wanaweza kukwepa mshale wangu wa sumu ya kimakonde?
Dawa ya mijitu kama hii ni kuimaliza kimya kimya kwa kujipenyeza kwenye udhaifu wao.

Ndugu, wezi hawa hawana direct impact kwetu kama ambavyo, mwizi aliyekuibia kuku banda la uwani. ingelikuwa hivyo walahi hawa watu wangechomwa moto kama wezi wa kuku mataani!
 
Ndugu, wezi hawa hawana direct impact kwetu kama ambavyo, mwizi aliyekuibia kuku banda la uwani. ingelikuwa hivyo walahi hawa watu wangechomwa moto kama wezi wa kuku mataani!

Mimi ninaona wana direct impact, kwa sababu hapo ulipo chochote unacho taka kufanya , kinakuwa affected na mafisadi, iwe usafiri, huduma nyingine kama matibabu/kiwanja, elimu , kisaikolojia etc
 
Mahakimu wahofu usalama kesi za EPA
Shadrack Sagati
Daily News; Friday,November 14, 2008 @21:15

Mahakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam ambako kesi za ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinasikilizwa, wamehofia usalama wao; hali iliyowalazimu kuomba kupatiwa ulinzi wa polisi.

size]


Mahakimu nao waache woga wa kitoto wabunge walipiga kele za EPA bila woga na hawana ulinzi,Haikimu gani au jaji gani mwoga jamani.Hiyo kazi mlitafutia nini nyie waoga.

Anyway naapa kwa nafsi yangu sababu sina dini kuwa mtu yeyote hakimu yeyote yule anayesimamia kesi ya EPA akifa kipindi kesi inaendelea hata kama atakufa kwa sababu yeyote ile basi mafisadi wa EPA itabidi wajipeleke wenyewe kulala polisi vinginevyo nikimkuta fisadi yeyote EPA POPOTE lazima nimlambe nondo kichwani ya kumpeleka kweye kaburi.Mafisadi wasiwatishie kabisa mahakimu wananchi tuna hasira nao.

Mahakimu msiogope lolote wananchi tuko nyuma yenu.Hata mkiona hakuna polisi wenye unifomu wanaowalinda mnapopanda daladala mjue kuna akina netanyahu na Invissible tutakuwa tunawazunguka kuwalinda popote mlipo kuhakikisha usalama wenu.Lakini mjue pia mkipokea Rushwa kwa mafisadi wa EPA tutajua na tukijua huo moto utakaowawakia.Mtajiju.
 
DPP returns EPA case files to law organs for further probe

THIS DAY

THE Director of Public Prosecutions (DPP), Eliezer Feleshi, has returned some of the case files on the Bank of Tanzania’s external payment arrears (EPA) account scandal to law enforcement agencies for more detailed investigations.

’’Files that require further investigations continue being worked on as per my instructions to investigating agencies,’’ the DPP said in a brief press statement yesterday.

This means that the DPP considers the evidence gathered in some of the investigation files submitted to his office as insufficient for drafting charge sheets and ultimately sending the cases to court for prosecution.

The EPA probe team led by Attorney-General Johnson Mwanyika handed over its investigation files to the DPP’s office on November 2, this year.

On the basis of those investigation files, public prosecutors have thus far filed criminal charges against 20 suspects linked to the EPA scandal.

Feleshi did not elaborate how many EPA files had been returned to investigators, but called for patience from members of the public to enable public prosecutors to do their work.

He also insisted that the DPP’s office was an autonomous government agency working ’’without the interference of anybody or any authority.’’

The DPP’s statement comes as latest THISDAY findings suggest that two prominent business tycoons linked to Kagoda Agriculture Limited, who are considered the main architects of the EPA scandal, will not face criminal charges despite stealing more than 40bn/- from the key BoT account.

Officials in close contact with the EPA investigation describe the prominent businessmen as ’’The Untouchables’’ behind the massive scandal.

’’These two businessmen are well connected and will be protected from prosecution at all costs,’’ a well-placed source told THISDAY.

It has been alleged that several influential people had been compromised to ensure the Kagoda case never goes to trial.

Although Feleshi did not offer any details, observers say his statement suggests that the Kagoda case files could be among those sent back to law enforcement agencies for further investigation.

Since Mwanyika’s team was appointed by President Jakaya Kikwete to probe the EPA scandal, government officials say the DPP has probably returned the ’incomplete’ case files to the AG for further investigation.

Sources say an elaborate strategy had already been put into action to ensure the two prominent businessmen linked to Kagoda are not included in the high-profile EPA criminal cases before the Kisutu Resident Magistrate’s Court.

Among the suspects arraigned so far include well-known businessmen Jeetu Patel, Johnson Lukaza and several other private individuals and BoT officials.

It remains to be seen if any so-called ’big fish’ will be arraigned in court next week or in the near future in connection with the EPA scandal.

Authorities have roundly been criticized by members of the public for failing to prosecute the well-known architects of grand corruption in the country.
 
Date::11/15/2008
DPP: EPA bado mbichi, aagiza uchunguzi baadhi ya majadala
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

SIKU chache baada ya kutanda ukimya wa kufikishwa mahakamani watuhumiwa wa ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), Mkurugenzi wa Mashitaka ya Umma (DPP), Eliazer Feleshi, amesema sakata hilo bado bichi.

Kauli ya DPP Feleshi imekuja siku chache baada ya watu wa kada mbalimbali, kuanza kuhoji kama idadi ya wanaotuhumiwa kwa wizi huo imekamilika baada ya jumla ya watu 20 kupandishwa kizimbani katika muda wa wiki mbili.

Swali kubwa la msingi ni kwamba, kati ya watu maarufu wanaotajwa kwenye sakata hilo la EPA, hadi sasa ni mfanyabiashara Jeetu Patel pekee, ambaye anaonekana kuwa kigogo kati ya wafanyabiashara hao 20.


Hata hivyo, DPP, katika kauli mpya ambayo aliitoa jijini Dares Salaam jana, ameongeza shinikizo la damu kwa baadhi ya watuhumiwa wa EPA akiashiria kuwepo uwezekano wa vigogo wengine, akiwemo waziri mmoja wa serikali ya awamu ya tatu, kutinga mahakamani.

Akivunja ukimya baada ya siku nne za hisia na mawazo tofauti, DPP Feleshi alisema hadi sasa kuna majalada ambayo bado yanafanyiwa uchunguzi.

Alifafanua kwamba hatua ya kuendelea kufanyiwa uchunguzi kwa baadhi ya majadala ni katika kuhakikisha ushahidi wa kutosha unapatikana.

Mkurugenzi huyo, ambaye ofisi yake kwa sasa inaangaliwa na umma kwa umakini, alisema hadi sasa majalada yote ambayo yako kwake yanafanyiwa kazi.

"Kwa majalada ambayo yanahitaji uchunguzi zaidi, yanaendelea kufanyiwa kazi kama nilivyoelekeza vyombo vya uchunguzi vifanye," alisema Feleshi kuthibitisha ubichi wa sakata la EPA.
Alisema Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ni ya umma inayofanya kazi zake bila kuingiliwa na mtu au mamlaka yeyote.

"Majalada yote yanayohusiana na EPA yanaendelea kufanyiwa kazi. Kama mnavyoshuhudia, baadhi ya watuhumiwa wamepelekwa mahakamani," alisisitiza.
"Ni kwa misingi hiyo, ninawaomba wananchi kuwa na subira na kuiacha ofisi kufanya kazi yake kwa kwa mujibu wa sheria."

Hadi sasa watuhumiwa 20 tayari wamekwishafikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa EPA, wakiwemo vigogo wanne wa BoT.

Hata hivyo, matarajio zaidi ni kuona vigogo zaidi ambao baadhi yao ni wafanyabiashara wakubwa.

Ufisadi huo wa EPA ulibainika katika hesabu za BoT za mwaka 2005/06, baada ya ukaguzi wa Kampuni ya Deloitte&Touche ya Afrika Kusini, ambayo ghafla ilisitishwa kazi na BoT bila sababu za msingi baada ya kubaini ufisadi wa sh 40 bilioni zilizochotwa na Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited.

Hata hivyo, baadaye serikali mwaka jana ilimwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutafuta kampuni ya kimataifa, kufanya ukaguzi huo kubaini ukweli.

Ofisi ya CAG iliteua Kampuni ya kimataifa ya Ernst&Young, ambayo ilibaini ufisadi wa fedha hizo zaidi ya sh 133 bilioni, ambazo zilichotwa na makampuni 22.

Makampuni 13 yalijichotea sh 90.3 bilioni, ni pamoja na Bencon International LTD of Tanzania, Vb & Associates LTD of Tanzania, Bina Resorts LTD of Tanzania, Venus Hotel LTD of Tanzania, Njake Hotel &Tours LTD, Maltan Mining LTD of Tanzania.

Mengine ni Money Planners & Consultants, Bora Hotels & Apartment LTD, B.V Holdings LTD, Ndovu Soaps LTD, Navy Cut Tobacco (T) LTD, Changanyikeni Residential Complex LTD na Kagoda Agriculture LTD.

Kwa upande wa makampuni tisa yaliyochota sh 42.6 ni pamoja na G&T International LTD, Excellent Services LTD, Mibale Farm, Liquidity Service LTD, Clayton Marketing LTD, M/S Rashtas (T) LTD, Malegesi Law Chambers (Advocates), Kiloma and Brothers na KARNEL LtD.

Makampuni mengine mawili ambayo ni Rashtas (T) na G&T International LTD, kumbukumbu zake ikiwemo nyaraka za usajili katika daftari la Msajili wa Majina ya Makampuni na Biashara (BRELA), hazikuweza kupatikana.

Kufikia mwaka 1999 deni katika EPA lilifikia dola 623 milioni, ambazo kati ya hizo dola 325 milioni zilikuwa ni deni la msingi na dola 298 ni riba na kisha baadaye, deni likaongezeka hadi kufikia dola 677 milioni.

Hata hivyo, chini ya Mpango wa Kununua Madeni (Debt Buy Back Scheme) wa mwaka 1994 kati ya serikali na Benki ya Dunia (WB), waliokuwa wanaidai BoT waliombwa wakubali kulipwa sehemu tu ya fedha wanazodai, wapo waliokubali na wengine kukataa na kuongeza hadi mwaka 2004 taarifa zinaonyesha jumla ya dola 228 zililipwa chini ya mpango huo.

EPA ni akaunti ya madeni ambayo ilitumika wakati wa Mfumo wa Ujamaa, ambayo akaunti yake ilikuwa katika iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) chini ya usimamizi wa BoT.

Mwaka 1985, EPA ilihamishiwa moja kwa moja BoT, na ndipo mwaka juzi kulipoibuka utata wa tuhuma za ufisadi katika akaunti hiyo kwa mahesabu ya mwaka 2005/06, ambayo utata huo ulisababisha Ernst&Young kufanya ukaguzi kuanzia Septemba sita na kukabidhi ripoti yake kwa CAG mapema Desemba mwaka jana.
 


THISDAY findings suggest that two prominent business tycoons linked to Kagoda Agriculture Limited, who are considered the main architects of the EPA scandal, will not face criminal charges despite stealing more than 40bn/- from the key BoT account.

Officials in close contact with the EPA investigation describe the prominent businessmen as ''The Untouchables'' behind the massive scandal.

''These two businessmen are well connected and will be protected from prosecution at all costs,'' a well-placed source told THISDAY.


Sasa hii journalism ya wapi jamani ? How can you do such a wussy and crappy reporting like that?

Hata kama ni mwoga vipi kwani unaweza kushitakiwa kwa kusema tu "Kagoda Agriculture ina mahusiano na Fulani bin Fulani" ?

Vigazeti vyetu jamani sijui hawalipwi vizuri masikini, au sijui watu tu wanaanzisha gazeti halafu wanaajiri watoto wa shangazi wawe waandishi ?
 
au sijui watu tu wanaanzisha gazeti halafu wanaajiri watoto wa shangazi wawe waandishi ?

Mtoto wa Bloomberg, anaendesha kampuni ya utangazaji ya baba yake bila tatizo, Mtoto wa Murdoch anaendesha kampuni ya baba ya utangazaji bila tatizo, Mjukuu wa Stamford anaendesha kampuni ya babu yake ya utangazaji bila tatizo, Unapoanzisha kampuni yako iwe ya anything, ndugu zako lazima wawe first priority kuajiriwa, hawa niliowataja wana one thing in common, wanazo qualifications.

Kuajiri mtoto wa shangazi sio tatizo, tatizo ni kama anazo qualifications za hiyo kazi ya utangazaji, otherwise kauli yako sio ya kistaarabu kwa wale waliojiri watoto wa shangazi zao wenye qualifications na wanatimiza kazi zao inavyotakiwa yaani professionally, bongo wako wengi sana, jaribu kuwa muangalifu na lugha mkuu maana ni wananchi wengi sana wanaoingia hapa JF kuchota elimu, si vyema kuwashusha hadhi bila ya kuwa na uhakika.

Thanxs and Later!
 
Nataka kusikia kauri moja tu.

Kagoda Agri Co yafikishwa mahakamani.

Bila Kampuni zote kufikishwa Mahakamani ikiwemo Kagoda Kesi ya EPA bado haijaanza.

CCM Msilete Maskhara kwenye hii issue ya EPA, sivyo mtakwenda ishi huko huko mliko weka hivyo vijisenti vyenu.
 
Nataka kusikia kauri moja tu.

Kagoda Agri Co yafikishwa mahakamani.

Bila Kampuni zote kufikishwa Mahakamani ikiwemo Kagoda Kesi ya EPA bado haijaanza.

CCM Msilete Maskhara kwenye hii issue ya EPA, sivyo mtakwenda ishi huko huko mliko weka hivyo vijisenti vyenu.


Kagoda nasikia haina mwenyewe, itafikishwaje mahakamani?
 
Kagoda nasikia haina mwenyewe, itafikishwaje mahakamani?

Mama Kagoda ina wenyewe lakini walipewa muda wa kutosha kuharibu ushahidi na JK alidhani huu wizi wa EPA utasahaulika baada ya kutaka kuleta usanii wake kwa kusema kwamba kiasi cha shilingi 69 billioni zimerudishwa ingawaje wameshindwa kuthibitisha ni akina nani waliorudisha na kiasi walichorudisha na zimewekwa wapi.

Angalia pesa za walimu hizo bilioni 10 tayari bank moja nchini imeshathibitisha kupokea pesa hizo, lakini za EPA bado wanafanya usanii.
 
?????????????????????????? Silewi unaelekea wapi? Uko ndani ya mada ama?

kabla hujanisomea hukumu nakuomba uiangalie thread hii toka muasisi mpaka hapo ninakupatia data za ndullu, ushindwe na kulegea mtumishi wa shetani wewe.
 
this para has been rectified, after getting the proper phrase from one of our Senior Member Mtanzania
"justice should not be done, but should manifestly and undoubtedly be seen to be done" na Mwingine ni "Justice delayed is justice denied". Sasa kuhusiana na Suala la EPA, ndugu yetu DPP amefuata misemo hiyo. Kama La tumpe Changamoto wa kulifanya hilo. ili alinde heshima yake, ya profession yake pamoja na ya Nchi yetu.
 
Nakumbuka kuna msemo "not only justice should done, but should also deemed to be done" or something like that, na mwingine ni "justice delay is justice denial" sasa kwa suala la EPA vitu hivyo vipo? au mwenendo wa case unaonyesha kuwepo kwa vitu hivyo?

Justice should not only be done, but should manifestly and undoubtedly be seen to be done.

Justice delayed is justice denied.
 
Justice should not only be done, but should manifestly and undoubtedly be seen to be done.

Justice delayed is justice denied.
Asante kwa marekebisho hayo, sasa je hilo jambo au hayo mambo unalionaje/unayaonaje kwenye kesi ya EPA.
 
Asante kwa marekebisho hayo, sasa je hilo jambo au hayo mambo unalionaje/unayaonaje kwenye kesi ya EPA.

Mimi nilianza kufurahia mafisadi kushughulikiwa lakini baada ya ile namba kubaki pale pale 20, naona hapa tunafungwa goli lingine.

Hivi kuna haja gani ya usiri kwenye jambo ambalo liko wazi kama hili?
 
Back
Top Bottom