Tukumbuke Mambo makubwa ya John Pombe Magufuli Enzi Hizo
(i) Aliadabisha na kufukuza wahandisi wazembe 224 Wizarani
(ii) Alizifuta kampuni hewa za makandarasi zaidi ya 1000
(iii) Alirudisha magari, mitambo na pikipiki zikiwa mali za serikali zaidi ya 21,000 na kuyasajili upya mfano PT,DFT,STK, US n.k zoezi hili liliigwa na Kenya na Uganda
(iv)Alimwadabisha mkandarasi aliyekuwa akijenga barabara ya Dsm-Bagamoyo kwa kutotii mkataba kitu kilichompelekea kufilisika
(v) Aliahidi kusafiri kutoka Mtwara kwa taksi mpaka Bukoba-ndoto imetimia
(Vi) Na mengine mengi mtayaongezea
Huu ndio uzalendo tunaoutaka " matumizi mazuri ya hela ya walipa kodi" hakuna ubishi watanzania wameiona kazi yake!