Ephraim Kibonde Jahazi Show

Ephraim Kibonde Jahazi Show

Moja ya nguzo zilizoijenga JF ni kuheshimu uhuru wa wengine kutoa mawazo,hata kama wengi hatuafikiani nayo.Kibonde ametumia ipasavyo haki yake ya kikatiba na kidemokrasia kutoa utetezi kwa Membe,regardless ya kilichomo kwenye utetezi huo.

Pili,just like Uhuru na Mzalendo zinavyoitetea CCM ambayo ni mmiliki wao,au IPP Media zinavyomfagilia Chairman Mengi,na au Habari Corporation wanavyomsujudia Rostam,same as kila chombo cha habari cha News Corp kinavyomheshimu Rupert Mordoch,Clouds nao wana uhuru wa kuwafagilia "wafadhili" wao.

Principles za uandishi wa habari ni vigumu sana kutekelezeka in real life pale wafadhili wa vyombo hivyo wanapokuwa sehemu ya habari.Ndio maana kwa hapa UK kuna wanaoliona gazeti la The Guardian kuwa lina fursa nzuri ya kufanya uandishi wa habari usiosukumwa na "kuwapepea wafadhili" kwa vile "it's owned by no one"

It's even worse katika mazingira ya Kibongo ambapo to succeed you need to win hearts and minds za mafisadi.And cheapest and easiest way ni kufanya wanafanyavyo akina Peter Serukamba.Not that I agree with them lakini hate them or love them wauza utu wao kwa ajili ya kupata maslahi yao ni miongoni mwa watu waliofanikiwa katika malengo yao huko Bongo,iwe kisiasa,kiuchumi au hata kijamii.

Going beyond alichokiongea Ephraim Kibonde,pengine ni muhimu kutambua aina ya wanahabari tulionao kwenye vyombo vya habari binafsi kama Clouds FM.Vipaji pekee walivyonavyo wengi wao ni sauti za kuiga,kubabaikiwa na wanajamii na vitu vingine visivyo na msingi kama hivyo.Ukitegemea mijadala iliyokwenda shule sehemu kama Clouds FM you could as well expect Osama kuwa the next US President.Tusishangae moshi kutoka kwenye exhaust ya gari mkweche.

Nafasi ya professionalism kwenye pandemic ya ubabaishaji ni pipedream.

Hakuna mtu aliyemzuia Kibonde kutoa maoni yake, tutamzuiaje na yeye ana redio sie hata hapa tunatoa maoni kwa hisani za watu?

Kama yeye alivyo na uhuru wa kutoa maoni, na sie tuna uhuru huo huo. Sasa hapo ndipo mashindano ya ideas yanapokuja.

Yeye kamtetea Membe na upupu wake, sisi tunamueleza jinsi alivyochemka yeye Kibonde na Membe wake.

Ndiyo maana ya forum. Mawazo kuruhusiwa kugongana.
 
Kibonde hana Lolote, he is just lining up kwa Nape Nnauye
 
huu ushabiki usio na faida kwa Taifa linalo didimia hautakiwi kuachwa hivi kama wana JF tunatakiwa tuukemee na kuugopa kama ukoma!

Naomba kujua CV ya Gadner na Kibonde ili tujue tuanzie wapi katika kupangua matumizi yao mabaya katika Radio kupotosha!

Leteni CV zao humu! Halaaa this can not be tolerated haswa ukiangalia ni uhusiano gani Clouds FM inao na Vijana !
 
Mwongo mtupu jamaa ni memba hapa mnadanganywa sio guest

Mi sidanganyiki

BTW amekiharibu kipindi cha kutoka magazetini kwenye jahazi zamini nilikuwa nakipenda alikuwa anasoma vizuri vichwa vya habari vizuri then siku hizi kichwa cha habari kimoja baada ya hapo ni kujisifia tuuuu haendi kwa time tena kama zamani
That's where we differ, Kibonde amefanya tutamani kusikiliza kile kipindi

He is good
 
Hakuna mtu aliyemzuia Kibonde kutoa maoni yake, tutamzuiaje na yeye ana redio sie hata hapa tunatoa maoni kwa hisani za watu?

Kama yeye alivyo na uhuru wa kutoa maoni, na sie tuna uhuru huo huo. Sasa hapo ndipo mashindano ya ideas yanapokuja.

Yeye kamtetea Membe na upupu wake, sisi tunamueleza jinsi alivyochemka yeye Kibonde na Membe wake.

Ndiyo maana ya forum. Mawazo kuruhusiwa kugongana.

Kuna mahala nimesema kuna mtu amemzuia Kibonde?Mbona ume-cherry pick hiyo opening statement pekee yangu badala ya mjumuisho wa chote nilichoongelea.
 
mumesahau kitu kimoja ana mpango wa kugombea ubunge jimbo moja la mkoani Mbeya mwaka 2010

Please Shy you can do better than this!!! lini alikwambia anataka kugombea? You sio lazima uibe ndio uitwe mwizi!! You know what i mean...
 
,
Ni mmoja wa watangazaji wa TV/Radio ambao ni maceleb wetu hapa bongo, he is good kwa kuigiza sauti mbalimbali ikiwepo ya Baba wa Taifa.

Kwenye Jahazi is doing good ingawa sometimes ana-over do jokes kwenye serious news zihusuzo loss of life.

Angalizo, ni celeb kwa viwango vyetu vya bongo, naombeni tusilinganishe na maceleb wa huko..
Well, we definately don't have any A-lister in Bongo, so he (she?!) must be either a C-list, F-list or Z-list celebrity........or probably just a poor shiterati (D-lister).
 
- Mkulu Kibonde, bravo kwa kuitangaza JF mbele ya jamii, as a JF member I humbled, juzi ilikuwa Kulikoni/This Day, leo Clouds, guess what kesho itakuwa Rais wa jamhuri, JF mbele tunazidi kunga'ara na kukubalika mbele ya jamii kwamba inapokuja kwenye masilahi ya taifa we know better than all,

- Mkuu Kibonde, ubarikiwe sana na ninakupa promise, mimi kesho asubuhi sana nitaongea na mabossi wako ambao ninawafahamu kwa karibu sana yaani Joe na Ruge, nitaweka a word of respect kwao for you na pia ningekuomba sana ujaribu kuelimisha na wanahabari wengine ulio karibu nao kuhusu your JF experience,

- Ubarikiwe na Mungu wa Mbinguni, na JF idumu zaidi!

Respect.

Field Marshall Es!
 
Naomba kujua CV ya Gadner na Kibonde ili tujue tuanzie wapi katika kupangua matumizi yao mabaya katika Radio kupotosha!

Leteni CV zao humu! Halaaa this can not be tolerated haswa ukiangalia ni uhusiano gani Clouds FM inao na Vijana !
Gezaulole, utangazaji ni kipaji kama wanamuziki, hii habari ya kutafuta CV, has nothing to do na kipaji hicho ingawa ni added advantage, naomba tusianze kuwahukumu watangazaji wetu kwa cv, its delivarence that matters, sio paperwork, wako watangazaji wasomi wenye masters degree za Lenigard University waliajiriwa TVT they delivered nothing huku ma form four leavers pale RTD wakifanya kazi nzuri tuu.
 
Habari nilizozipata punde..

Mtangazaji wa clouds Fm Ephraim Kibonde ameitumia salamu Jamii Forums, home of great thinkers na ameshukuru na kuheshimu michango yake..

Wewe ndio kibonde nini?
 
hakuna lolote la maana kutoka kwake ..mwambie tunashukuru kwa salaam afanye kazi yake kwa ufasaha na aache chokochoko
Na umuulize yeye Siasa anaiweza??????????

NB: kwa nini akutume wewe na asije yeye hapa anaogopa ? au wewe ndio yeye na yeye ndio wewe

aahaaaaa,
kun wakti anakera sana huyu
 
Kila mtu anasoma jamii.....iko juu sana.....inatanua vichwa na kisima cha wazalendo...na wanamapinduzi
 
Habari nilizozipata punde..

Mtangazaji wa clouds Fm Ephraim Kibonde ameitumia salamu Jamii Forums, home of great thinkers na ameshukuru na kuheshimu michango yake..
Kibonde GO AHEAD, ENDELEA KUSHAINI........... Maana mti wenye matunda ndiyo unaopigwa mawe................... Humu JF kuna msemo unaosema MKONO MTUPU HAULAMBWI.................. Mkono wako si mtupu, ndiyo maana unatajwa sana........................... WHO THE HELL IS KIBONDE........... ANAGOMBEA UBUNGE................ HAJUI KUTANGAZA................. ANAROPOKA............... CV............. BIBLIOGRAPHY ..................etc
Remember, one day someone in this JF said ............. THE ONE WHO HATES YOU MOST........... LOVES YOU MOST
 
Kwa hiyo hata majambazi, wauza unga, vibaka waendelee tu kwa sababu jamiii inawatajataja? kazi kwelikweli!!
 
Jamani acheni uongo. Kibonde sio member humu na wala sio guest wa kila siku. Jana alinihaidi kuja humu na kusoma mliyoandika juu yake. Sijui kama alikuja au la maana hakunipa feedback

Ni jambo zuri kama ameamua kuipa JF sifa inayostahili.
 
Back
Top Bottom