Bluray
JF-Expert Member
- Mar 25, 2008
- 3,449
- 137
Moja ya nguzo zilizoijenga JF ni kuheshimu uhuru wa wengine kutoa mawazo,hata kama wengi hatuafikiani nayo.Kibonde ametumia ipasavyo haki yake ya kikatiba na kidemokrasia kutoa utetezi kwa Membe,regardless ya kilichomo kwenye utetezi huo.
Pili,just like Uhuru na Mzalendo zinavyoitetea CCM ambayo ni mmiliki wao,au IPP Media zinavyomfagilia Chairman Mengi,na au Habari Corporation wanavyomsujudia Rostam,same as kila chombo cha habari cha News Corp kinavyomheshimu Rupert Mordoch,Clouds nao wana uhuru wa kuwafagilia "wafadhili" wao.
Principles za uandishi wa habari ni vigumu sana kutekelezeka in real life pale wafadhili wa vyombo hivyo wanapokuwa sehemu ya habari.Ndio maana kwa hapa UK kuna wanaoliona gazeti la The Guardian kuwa lina fursa nzuri ya kufanya uandishi wa habari usiosukumwa na "kuwapepea wafadhili" kwa vile "it's owned by no one"
It's even worse katika mazingira ya Kibongo ambapo to succeed you need to win hearts and minds za mafisadi.And cheapest and easiest way ni kufanya wanafanyavyo akina Peter Serukamba.Not that I agree with them lakini hate them or love them wauza utu wao kwa ajili ya kupata maslahi yao ni miongoni mwa watu waliofanikiwa katika malengo yao huko Bongo,iwe kisiasa,kiuchumi au hata kijamii.
Going beyond alichokiongea Ephraim Kibonde,pengine ni muhimu kutambua aina ya wanahabari tulionao kwenye vyombo vya habari binafsi kama Clouds FM.Vipaji pekee walivyonavyo wengi wao ni sauti za kuiga,kubabaikiwa na wanajamii na vitu vingine visivyo na msingi kama hivyo.Ukitegemea mijadala iliyokwenda shule sehemu kama Clouds FM you could as well expect Osama kuwa the next US President.Tusishangae moshi kutoka kwenye exhaust ya gari mkweche.
Nafasi ya professionalism kwenye pandemic ya ubabaishaji ni pipedream.
Hakuna mtu aliyemzuia Kibonde kutoa maoni yake, tutamzuiaje na yeye ana redio sie hata hapa tunatoa maoni kwa hisani za watu?
Kama yeye alivyo na uhuru wa kutoa maoni, na sie tuna uhuru huo huo. Sasa hapo ndipo mashindano ya ideas yanapokuja.
Yeye kamtetea Membe na upupu wake, sisi tunamueleza jinsi alivyochemka yeye Kibonde na Membe wake.
Ndiyo maana ya forum. Mawazo kuruhusiwa kugongana.