Sikonge,
..i will grant you the benefit of doubt ktk haya masuala ya ukabila.
..i will also speculate kwamba ulihemewa tu ulipotoa mfano kwamba Mramba[mchaga] na bajeti ya barabara ni moja ya dhuluma za serikali dhidi ya mikoa ya pembezoni.
..naomba pia nikuelimishe kwamba mradi wa barabara jimboni kwa Mramba ulianza wakati wa John Magufuli. pia mradi ule ulipewa pesa zaidi wakati wa Mramba kwasababu ulikuwa ktk advanced stage ya ujenzi. Mbunge aliyelalamika mradi wake ulikuwa ama ktk design stage au feasibility study, ndiyo maana ukapewa fedha kidogo.
..nilitegemea baada ya posting yangu ungejielimisha zaidi kuhusu miradi hiyo miwili, na pia ungeomba radhi kwa kauli yako.
..nasubiri kwa hamu kuona kama Mbunge Selelii, na wenzake, atamkaba koo Waziri wa sasa miuondo mbinu Dr.Kawambwa, kama alivyofanya kwa Mramba mwaka jana.
..Basil Mramba ana kashfa[kuchapisha noti chafu na kampuni ya kijerumani, misamaha ya kodi...] nyingi tu kama mwanasiasa, lakini hili la kusema amedhulumu barabara za jimboni kwa Lucas Selelii na wenzake, siyo kweli.
..tofauti uliyoitaja kuhusu Kilimanjaro,Mbeya,Arusha, kulinganisha na mikoa ya pembezoni ni suala kihistoria. ule msingi[elimu,miundo mbinu...] uliowekwa na wamisionari na wakoloni ndiyo unaowapa ahueni mikoa hiyo. vinginevyo nchi nzima imeathirika kutokana na uongozi mbaya wa Tanu na baadaye CCM.
..zaidi siamini kama Mchaga,Mhaya,Mnyakyusa ana akili zaidi, au ni mjanja zaidi, au ni mchapakazi zaidi, kuliko Muha, Mnyaturu, Makonde etc etc. tofauti za makabila hayo ni exposure tu.
..naamini kabisa kabisa kwamba Waha,Wanyaturu,...wangepewa historical opportunities walizopewa Wachaga,Wahaya,..basi leo hii Kigoma,Singida,Mtwara, ingekuwa inasifika kwa "maendeleo" na Kilimanjaro,Kagera,..ingekuwa ndiyo mikoa ya pembezoni.
..hakuna hata siku moja nchi nzima[makabila yote,mikoa yote]itakuwa ktk hatua moja ya maendeleo. siku zote kutakuwepo na maeneo yaliyopiga hatua zaidi kulinganisha na mengine. kitu cha kuzingatia ni kujaribu kuzielewa tofauti hizo, na zaidi eneo moja kujifunza toka eneo lingine. mara nyingine maendeleo hupatikana kwa kuiga.
..nashauri kabla ya kuwashutumu Msuya na Mramba, tuwabane kina Samwel Sitta,Rashidi Kawawa,Maokola Majogo,Ben Mkapa,Nalaila Kiula, Anna Abdalah, Jakaya Kikwete,Paul Kimiti,Chrisant Mzindakaya...wajieleze kwanini wameshindwa kuhimiza maendeleo ktk mikoa ya kusini na mingine ya pembezoni.