Mhafidhina,
Kwa hilo la kupewa maswali ya Interview, nitakupinga kwa kitu kimoja. Maswali ya Interview siyo mtihani wa Mock au Form Four.
Kama mtu umeshafanya kazi kwa muda mrefu na kufanya interview nyingi, maswali huwa ni yale yale, from one corner of the wordl to the other.
Mmesema Mrema kafanya kazi kimataifa, je huko alikokuwa si alifanya interview, je ni ugumu gani kujua kuwa anaweza kujibu swali?
Nitakupa mfano, miaka mitatu iliyopita, nilikuwa natafuta kazi nyingine katika shirika ninalofanya kazi. Kwa kipindi cha miezi mitatu, nilifanya zaidi ya interview 20 na masuali pamoja yalikuwa ni kutoka kwa watu tofuati wa idara tofauti na wasiojuana, yalikuwa na common theme.
Ni ujinga na upumbavu mkubwa ambao unapaswa kuepukwa na sisi hasa tunaojiita wasomi kuanza kuropoka kuwa mtu alipewa maswali ya Interview.
Nitakuambia maswali ya msingi ambayo aliulizwa kwenye interview,
1. Tell us about your self
2. Why should we hire you?
3. What can you bring to our company?
4. What is your vision foer this company and its future projects?
5. What are the obstacles of buuilding good roads in Tanzania?
6. How will you handle contracts disputes?
7. How and what ways you will motivate your employees to be efficient, creative and be productive?
Hata kama aliulizwa swali la Kiufundi kama asphalt in chemical composition ngapi, ni upuuzi kutamka na ni aibu kudai eti alipewa pepa!
Na hao ambao walimshangaa Mrema kwa umahiri na kujiamini kwake kunaniambia kuwa hawajui kufanya interview, ni watu biased na zaidi wana poor exposure na wamezoea ku-interview one dimensional candidates. Kama hawajamaa walishangaa na kuzubaa kwa umahiri wa Mrema kujieleza na kujibu maswali, basi tuna tatizo Tanzania na hawa wanaofanya interviews ni wabovu!
Kuongea kwa ufasaha na kujiamini si suala la pepa, ni uwezo wa mtu. Ndio maana nimesema kigezo si Elimu na Vyeti bali ni ufanisi.
Rev. Kishoka,
Interviews za tanzania ziko tofauti na hasa hizo zinazoendeshwa na wizara.
Pia kwenye mambo ya technical, ukiachia maswali ya jumla kama uliyoyaandika, kuna kampuni wanaingia deep kwenye nyanja husika.
Huku West sasa wameacha kwenda ndani kwenye nyanja husika na badala yake wanauliza maswali genaral kwasababu wanaamini kwenye uwezo wa mtu ku cope kwenye mazingira mbalimbali, Tanzania na Afrika, tunaamini kwenye ukipanga, uwezo wa kukokotoa majibu kama yalivyo kwenye vitabu vya wasomi.
Sisemi Mrema alipewa maswali, ila nataka kutofautisha tu juu ya interviews ambazo zinaendeshwa na makampuni ya uajiri na zile za wizarani.
Aidha ukiaangalia matatizo mengi ya Tanzania utakuta kinachokosekana ni management skills na wala sio hizo technical skills. Nafasi kama ya CEO inatakiwa skills zaidi ya zile za ujenzi barabara. Ukiwa fundi ujenzi ni added value lakini muhimu zaidi ni management skills.
Huyo Mrema ni mwakilishi tu wa kundi kubwa amblo mimi huwa naliita middle class ya Tanzania ambao ni mzigo kwa maendeleo ya nchi yetu. Wanapata pesa nyingi lakini utendaji wao mbovu, wanapiga vita watanzania wenzao, wanakula rushwa, wana ukabila nk.