Waacheni wahandisi wale nchi, hivi wale waliokwiba mabilioni mboni mpo nao hadi bungeni na hamuwafanyi chochote? Yaani watu kula honoraria ya ka-tumiloni 40 tu imekuwa nongwa?
Hivi mnajua TANROADS inafanyaje kazi kimuundo na kimaslahi inatakiwa wajiendesheje au mnabwata ? TANROADS ni agency period. Kama hamjui jambo ni vyema mkauliza kwanza.
Hebu eleza maana hasa ya agency?, maana naona umelipuka na taarifa nusu nusu. Mimi ninavyojua kuna "Government agencies", sasa hizi zinaweza kuwa "quangos" - quasi-non government organizations ambazo zina semi-autonomy lakini zinategemea most of their resources from public (hapa naamanisha pesa za walipa kodi, au kwa bongo tunasema wanapewa pesa toka hazina), Kwa kuwa TANROADS ni agency iliyo chini ya serikali, ni dhahiri kabisa kuwa pesa walizogawana zimetoka hazina na ndiyo maana wamempa hata katibu mkuu wa wizara Shs 10m kama ahsante ya kuidhinisha malipo hayo.
Huu ni ufisadi tosha, hasa ukizingatia barabara nyingi hazipitiki na nyingine hata maintenance hazifanyiwi kama hazina mwenyewe vile. Wizi ni wizi tu uwe wa kuku au ng'ombe. Wewe unayesema watu wameiba mabilioni tunawaacha wakati wengine wanaiba tu-milioni 40 tunawakomalia unatakiwa kujua kuwa baya kubwa halihalalishi baya dogo kuwa zuri. Watu kama hawa wasiojali resources walizopewa kuzilinda hawastahili kuendelea na nafasi hizi, kwani wakipewa nyingi wataiba zaidi.
hebu fikiria hizo Shs 40m zingetumika kutengeneza madimbwi yalipo barabarani hata kama ni mita 20 watu wangapi wangepata ajira?. Hatukatai kupongezana kupo makazini ila si kwa style hii ya bonus za kurudisha nyuma maendeleo. Unakumbuka Maghufuli alipokuwa wizara ya miundombinu alivyokuwa anawapasha hawa TANROADS, wanalipana mishahara mikubwa bila kuwa na tija. Huu ni wizi wa pesa za walipa kodi na ingekuwa kwa wenzetu wangezirudisha zote kwa wenyewe wananchi.