Ephraim Mrema na Ufisadi TANROADS

Ephraim Mrema na Ufisadi TANROADS

hapo TANROADS ni pa wachaga kama hamjui na itakuwa ngumu sana Mrema kuondoka maana naye anakata fungu kwa vigogo.
Barabara hamna watu wanalipwa kama ma TX huku wenye magari wakizidiwa na mzigo wa kurepea magari yao,
Nchi hii watu wanakula tu ila nakwambia siku inakuja watalia na kusaga meno!!
Kwanza kwanini alipwe kwa dola?Au wanajaribu kupunguza makali ya kutaja hayo mabiliono kwa mwaka ambayo anachota??
 
Mrema amekuwa akitumiwa na World Bank kama Procurement specialist kwenye miradi yao. eg Barabara za Kijitonyama. Alishawahi kufanya kazi hapo zamani NEDCO. Alikuwa one of the best students nationally o level na a level.
 
Shukuru jana alikuwa mdogo wakati hoja nzito zikipangwa mbele ya meza yake na wabunge
 

Aliweka hadharani viwango hivyo kuwa Mrema alipoanza kazi alipewa posho ya kuanza (Commencement allowance) dola za Marekani 9,000 kwa siku 60 (sawa na Sh milioni 10.8), mshahara wake kwa mwezi ni dola za Marekani 8,500 (Sh milioni 10.2), posho ya nyumba kwa mwezi ni dola 2,200 (Sh milioni 2.6), posho ya matibabu dola 400 kwa mwezi (Sh 480,000), posho ya usafiri dola 500 (Sh 600,000).

Pia analipwa pensheni kwa mwaka kiasi cha dola za Marekani 10,200 (Sh milioni 12.4), akienda likizo analipwa dola 3,000 (Sh milioni 3.6), bonasi yake kwa mwaka analipwa dola 102,000 (Sh milioni 122.4) na mwisho wa mkataba wake analipwa dola 10,000 (Sh milioni 12) kama malipo ya kumaliza kazi.



Hivi Tanroads si ni Idara ya Serikali...kwa nini huyu halipwi mshahara wa Serikali?
 
Ukitaka kumfahamu vizuri Mrema alivyo ktk utendaji wake....fuatilia pale alipokuwa ktk mradi uliokuwa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu..........in short niliposikia huyu jamaa kawa CEO wa TANROADS...........nikasema basi tena tumekwisha...........
 
kuwa best students hakumpi sifa ya kulipwa hivyo jamani

Wakuu,
Hebu tuacha kumlaumu Mrema kwa kulipwa alikuta kimewekwa na Serikali, yeye hakujipangia hiyo package....aliikuta....inawezekana pia hiyo package ndiyo iliyomvumtia hadi akaomba hiyo kazi. Pia hakuna haja ya kuongelea uchagga wala upare (au labda watu waje na facts za ukabila). Pia, wahandisi kulipwa kidogo sio kosa la Mrema. Hivi ni wapi kuna terms kwamba afisa mtendaji mkuu wa TANROADS lazima awe mhandisi ujenzi?

Tuangalie jinsi alivyoingia (kama aliingia kifisadi) na pia kama kuna watu anawatendea sivyo (kama hili la mizani Kibaha)!

Binafsi napenda jinsi Mrema anavyoshughulikia wakandarasi wazembe, kama mtu amevuta kitu kidogo ni vigumu kuchukua hatua nachokua Mrema. Inatugharimu lakini inaleta nidhamu kwenye ujenzi wa miundo mbinu yetu.
 
Mrema amekuwa akitumiwa na World Bank kama Procurement specialist kwenye miradi yao. eg Barabara za Kijitonyama. Alishawahi kufanya kazi hapo zamani NEDCO. Alikuwa one of the best students nationally o level na a level.

That is rubbish!
 

Wakuu,
Hebu tuacha kumlaumu Mrema kwa kulipwa alikuta kimewekwa na Serikali, yeye hakujipangia hiyo package....aliikuta....inawezekana pia hiyo package ndiyo iliyomvumtia hadi akaomba hiyo kazi. Pia hakuna haja ya kuongelea uchagga wala upare (au labda watu waje na facts za ukabila). Pia, wahandisi kulipwa kidogo sio kosa la Mrema. Hivi ni wapi kuna terms kwamba afisa mtendaji mkuu wa TANROADS lazima awe mhandisi ujenzi?

Tuangalie jinsi alivyoingia (kama aliingia kifisadi) na pia kama kuna watu anawatendea sivyo (kama hili la mizani Kibaha)!

Binafsi napenda jinsi Mrema anavyoshughulikia wakandarasi wazembe, kama mtu amevuta kitu kidogo ni vigumu kuchukua hatua nachokua Mrema. Inatugharimu lakini inaleta nidhamu kwenye ujenzi wa miundo mbinu yetu.

Nashukuru, lakini inaonesha unamjua vyema huyu mrema wa tnroads. Hebu basi thibitisha utendaji wake unaousifia. Vinginevo utakuwa hueleweki.
 
Yaani mimi mtu akishatamka WORLD BANK na ndugu zake ndo namuona anatulostisha kabisa..Hata akina Balali and co..walikuwa na utumishi uliotukuka huko World Bank, lakini mpaka leo ndo wametufukarisha.

Please whoever wants to make a point, atupe ila siyo hizi siasa za best student Olevel na resume ya World Bank nk..Na kama nimemuelewa Mporogomyi..anauliza hivi: IWEJE APPLICANT AMBAYE HAKUWEMO KWENYE TOP FOUR WALIOKUWA RECOMMENDED KUAJIRIWA APATE AJIRA? Interview haikuwa na maana tena! Ndilo swali linahitaji jibu..mengine ni longo longo tuu hapa..

Tatizo la watanzania...kwa sababu ya unafiki wetu..watu hapa wataanza kuligeuza hili swala kwenye ukabila kwamba jamaa anaonewa kwa vile ni mchagaa! Wakati watu wanauliza maswali na wanahitaji majibu! Period.
 
PATA NAFASI, ONGEA NA WAFANYAKAZI WA TANROADS, HAPO UTAJUA MREMA NI NANI NA AMEWAHI KUTAMKA MANENO GANI KUHUSU NAFASI YAKE.....! (hakuna wa kumtoa kwa sababu amewekwa)(?)
 
Nashukuru, lakini inaonesha unamjua vyema huyu mrema wa tnroads. Hebu basi thibitisha utendaji wake unaousifia. Vinginevo utakuwa hueleweki.

Mkuu Kungurumweupe,
Kumfahamu vizuri bwana Ephraim Mrema, hapana! Namfahamu kiasi kidogo tu na ni kwa sababu mimi ni mdau wa ujenzi.
Niliandika kwamba napenda anavyoshughulikia wakandarasi wazembe....kama yule wa barabara ya Marangu Mkuu na yule wa Kagoma Lusahunga.
Naomba nieleweke kwamba simtetei CEO wa TANROADS, nimesema nilichoona ni sahihi tu.
Pia niliomba kama kuna mtu anafahamu vema njia yake kuingia TANROADS (kutoka sekta binafsi) amwage ili tuona kama kuna mizengwe (ama ufisadi) katika kuingia kwake TANROADS....pia imesemwa kwamba anawakwaza wanaotenda haki au kutetea masilahi ya umma, hili pia linahitaji data.
Ni hayo tu Mkuu.
 
Last edited:
Roya Roy,Masanja,Kungurumweupe,

..kuna yeyote yule mwenye majibu ya Waziri wa Miundo mbinu?

..nitashangaa sana kama habari hii itaishia na madai ya Mporogomyi tu, bila kuweka majibu ya waziri mhusika.

NB:

..shahada ya Construction Economics, ina maana Mrema ni quantity surveyor au?
 
Pia niliomba kama kuna mtu anafahamu vema njia yake kuingia TANROADS (kutoka sekta binafsi) amwage ili tuone kama kuna mizengwe (ama ufisadi) katika kuingia kwake TANROADS.

Ina maana huziamini data za Mh. Mbunge ambaye aliyasema hayo Bungeni na yeye (Mrema) akiwa ndani ya mjengo? Habari imetaja majina 4 ya watu ambao baada ya usaili (interview) walikuwa recommended kuchukua hiyo nafasi, lakini mtu ambaye hakuwamo kwenye orodha ndiyo akaja kupewa hiyo nafasi. Je, hapo ametumia njia gani kupata hiyo ajira? Au kuna inteview mbili zilifanyika kwa nyakati tofauti? Na kibaya zaidi records lazima zipo unless kama watu walicheza na ma-file na hata wale walio conduct interview wapo wanaweza kuulizwa na kutoa majibu kama Waziri atakuwa na nia ya kushughulikia hilo swala.

Kupambana watenda haki kuna mtu katajwa jina na kiwango cha fine ambacho alitoza magari yaliyozidisha mzigo na kituo chake cha kazi kiko wazi na records lazima zitakuwapo kwenye vitabu. Bado tunataka data? Kuna data nyingine kuzileta hapa inaweza kuwa ngumu, nina amini Mbunge alichokisema ni kweli na sidhani kama anaweza kujipunguzia heshima yake kutamka hayo maneno mbele ya Bunge na mhusika mwenyewe akiwa ndani ya mjengo.
 
''Anger is a condition in which the tongue works faster than the mind''

Huyu Mbunge alikuwa na hasira kweli. Hata hivyo hajajiuliza anayepanga na kupitisha policy za hiyo Tanroads ni nani. Mishahara na maslahi ya shirika kama Tanroads sio specific kwa mtu bali kwa nafasi.Mrema alikuta haya tokea kwa mtangulizi wake.

Niliwahi kusikia siku za nyuma kuwa wafanyakazi wa Tanroads ndio the highly paid workers in Tanzania. mbunge angetuambia pia mishahara ya Tanroads iko vipi na sio kumchachamalia CEO kama vile yeye ndiyo Tanroads. Think about the role of the Board Of Directors Mr Mp and stop political bla blas.

Kwa mtazamo wowote ule tanroads ni vyema ikachunguzwa kwani kama kweli aliyoyasema mp ni ya kweli basi liko tatizo kubwa kuliko unavofikiria.
 
Wana JF,
Nafikiri hii position ingelikuwa vema ishikwe na Mhandisi aliyesomea Uongozi. Kama hakuna Mtanzania basi apewe Mwafrica mwingine. Ila kama ni Mwafrica ina maana apewe mshahara wa Dola au Euro au Paund. Mtanzania kwa sababu hii ni idara ya serikali basi apewe Tsh. Hivi kwa nini hatuiheshimu hii hela yetu? Inawezekana alikuta huo mshahara ila ilibidi ajue kuwa huo ulikuwa wa Mghana. Kwa Mtanzania anayefanyika kazi kwao inabidi uwe tofauti, hasa hayo ma-allowance. Maana yapo hadi ya likizo wakati likizo utakuta hata akienda kwao basi pesa si sawa na kwenda Ghana.

Juu ya Ukabila mie naunga mkono. Huu ugomvi ulikuwepo, upo na utaedelea kuwepo. Siyo siri kuwa makabila mengi yanawaonea wivu Wachaga, Wahaya, Wasukuma, Wakinga, Wanyakyusa ...... Ukifika Bukoba, Mwanza, Arusha/Kilimanjaro, Mbeya .... kwa kweli utashangaa kama uko Tanzania (baadhi ya maeneo). Kuna mikoa imesahaulika kabisa na tujikumbushe bajeti ya ujenzi wa Barabara ya Mramba. Sasa watu wakiona hata TANROAD iko chini ya Mchaga, na pesa zote zaenda huko kwa kweli unataka kulia. Ukifika huku kwetu Sikonge, loo ni kwa Wamasembere kweli kweli. Barabara nzuri Tabora mjini ni ile inaenda Airport na lami imeishia mita kadhaa na hapo unaanza TOPE zito hadi ile Landing lane yenyewe ni ya TOPE.

Kama huamini jaribu kuvuta GOOGLE EARTH na uangalie picha ya Tabora mjini jinsi ilivyochoka, na watu wanalima Mpunga na Mahindi hadi City center. Hii siku zote italeta Cheche. Msiwe watu wa kulaumu kuwa watu wanawasha moto wakati serikali yetu imeweka kuni kavu tayari, nyasi kavu na kumwagia petroli. Hii utaiona mikoa mingi tu kama Kigoma, Singida, Lindi, Mtwara, Tanga nk. Serikali au yenyewe Ijitahidi kubadilisha maisha ya watu huko na ikishindwa basi IWALAZIMISHE hawa watu wabadili maisha yao.

Wanaweza kila kitu wakitaka. Just WAKITAKA.
 
Back
Top Bottom