Ephraim Mrema na Ufisadi TANROADS

Ephraim Mrema na Ufisadi TANROADS

Rais Jakaya Kikwete `ameicharukia` Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Barabara nchini TANROADS kutowapa kazi wakandarasi wababaishaji, pia kutowalipa wanaojenga barabara chini ya viwango.

``Wakandarasi wababaishaji wasipewe kazi, wanatufikisha pabaya,`` alisema.

Aidha, aliwataka wizara ya ujenzi wanapotoa tenda wamchague yule aliyetoa hesabu kubwa na sio kuangalia mwenye hesabu ndogo kwani wao pia ukubwa wa kazi wanaijua.

``
Hakuna sababu wizara, TANROADS kumchagua mtu mwenye hesabu ndogo, mnapotangaza tenda lazima kuangalia kama kazi ataiweza, ingawa wale watakaokosa watasema mnajali mafisadi,... hayo msiyajali!,`` alishauri.

Aidha, amesema yapo makampuni kadhaa hapa nchini ambayo kazi yao ni kudanganya pindi wanapokuwa wamepewa tenda za kutekeleza miradi mbalimbali.

Alisema hayo jana mjini hapa wakati akizindua barabara ya Isuna hadi Manyoni yenye urefu wa kilomita 55 baada ya mkandarasi aliyepewa kazi ya kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kushindwa kazi kwa visingizio.

Rais Kikwete yuko mkoani humu kwa ziara ya siku sita kwa ajili ya kukagua shughuli za maendeleo pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua mwaka 2005.

Rais Kikwete alisema awali barabara hiyo ya Isuna-Manyoni, ilikuwa ikijengwa na mkandarasi kutoka China ambaye alishindwa kukamilisha kazi kama ilivyotakiwa.

Alisema kilichotokea hapo iwe ni fundisho na kwamba tatizo la namna hiyo lisijitokeze tena.

Aidha Rais Kikwete alibainisha kuwa kupewa tenda kwa mkandarasi mwenye hesabu ndogo ndiko kunakosababisha matatizo ikiwa ni pamoja na miradi kutokamilika kwa wakati uliotakiwa.

Alisema wakiendelea na utaratibu huo wa kuangalia hesabu ndogo watakwama wakati nchi bado ni maskini.

``Ninaomba sana, bure ni ghali sana, kwani angalia sasa tunaingia gharama nyingine tena kubwa zaidi kuliko zile za awali,`` alisema.

Aliongeza kuwa mzabuni atakayekiuka utaratibu unaotakiwa wanapaswa kumuita na kumuuliza ili wasimamie katika ukweli na haki na sio kuwachanganya.

Kuhusu makampuni yanayodanganya alisema hapa nchini yapo kadhaa na kazi yao ndio hiyo halafu badaye huhitaji majadiliano.

``Simamieni wataalamu mlio nao, makampuni yawe yanasema ukweli kuepusha hasara katika nchi,`` alisema.

``Nchi hii ni maskini, ujenzi huu unagharamiwa na fedha za wananchi, epukeni kuingia gharama mara mbili, kwani wanaofanya hivyo wanakuwa wanyonya damu,`` alisema.

Pia aliwataka kukasirika na kuwachukulia hatua makampuni yanayokiuka utaratibu ikiwa ni pamoja na kuwaambia kwa herini (byebye) wakatafute tenda nyingine nje ya nchi.

Rais aliongeza kuwa mhandisi mshauri naye hatakiwi kulipwa malipo yake endapo ujenzi hautakuwa umekamilika kwa kiwango kinachotakiwa kwani wasipofanya hivyo Tanzania itakuwa shamba la wajinga.

Lazima Watanzania waone uchungu na kutekeleza miradi ya wananchi katika kiwango kinachotakiwa, alisisitiza.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Bw. Omar Chambo alisema barabara hiyo itagharimu kiasi cha Sh. bilioni 30.43 na ujenzi wake ulisainiwa Desemba 11, mwaka 2007.

Alisema barabara hiyo ilisainiwa kati ya TANROADS na Kampuni ya China Geo Engineering kutoka nchini China na kwamba sehemu ya barabara hiyo inatarajiwa kukamilia ifikapo mwaka 2010.

Alisema mradi huo unasimamiwa na mhandisi mshauri Black &Veatch kutoka Afrika Kusini akishirikiana na Kampuni ya Mak Consult ya Tanzania kwa gharama ya Sh. milioni 857.23.
 
Sasa wanaoleta UKABILA HAPA...WASOME HAYO HAPO JUU KABLA HAWAJAENDELEZA PROPANGANDA KWA SABABU MTAJIUMBUA BURE!
HAYO NI MANENO YA KIKWETE MWENYEWE KAWAAMBIA HAO KINA MREMA WASIJALI KUITWA MAFISADI!
SASA...FISADI NI MCHAGGA?
ACHENI PROPAGANDA NA MUWAHIMIZE WABUNGE WAULIZIE RIPOTI MARA MOJA TUPATE UHURU WETU!
 
JokaKuu,
Naona hukusoma ujumbe wangu vizuri au umesoma ila ukaamuwa kuchukua tu yale uliyoyataka. Naomba upitie tena ujue nini nilisema juu ya UKABILA na hasa sehemu zenye rangi NYEKUNDU.

Juu ya Ukabila mie naunga mkono. Huu ugomvi ulikuwepo, upo na utaedelea kuwepo. Siyo siri kuwa makabila mengi yanawaonea wivu Wachaga, Wahaya, Wasukuma, Wakinga, Wanyakyusa ...... Ukifika Bukoba, Mwanza, Arusha/Kilimanjaro, Mbeya .... kwa kweli utashangaa kama uko Tanzania (baadhi ya maeneo). Kuna mikoa imesahaulika kabisa na tujikumbushe bajeti ya ujenzi wa Barabara ya Mramba. Sasa watu wakiona hata TANROAD iko chini ya Mchaga, na pesa zote zaenda huko kwa kweli unataka kulia. Ukifika huku kwetu Sikonge, loo ni kwa Wamasembere kweli kweli. Barabara nzuri Tabora mjini ni ile inaenda Airport na lami imeishia mita kadhaa na hapo unaanza TOPE zito hadi ile Landing lane yenyewe ni ya TOPE. Kama huamini jaribu kuvuta GOOGLE EARTH na uangalie picha ya Tabora mjini jinsi ilivyochoka, na watu wanalima Mpunga na Mahindi hadi City center. Hii siku zote italeta Cheche. Msiwe watu wa kulaumu kuwa watu wanawasha moto wakati serikali yetu imeweka kuni kavu tayari, nyasi kavu na kumwagia petroli. Hii utaiona mikoa mingi tu kama Kigoma, Singida, Lindi, Mtwara, Tanga nk. Serikali au yenyewe Ijitahidi kubadilisha maisha ya watu huko na ikishindwa basi IWALAZIMISHE hawa watu wabadili maisha yao. Wanaweza kila kitu wakitaka. Just WAKITAKA.
Ukiangalia vizuri utaona kuwa makosa nimeyatupa kwa SERIKALI na MAKABILA MASIKINI na WIVU WAO. Sijasema hapa Wachaga au Wahaya ndiyo wamesababisha hawa wawe masikini. Nimekaa Arusha/Kilimanjaro na nimeona jinsi jamaa wanavyochapa kazi na siyo kujishughulisha kama huku kwetu Sikonge. Ila kwa LIMBUKENI wa hapa Sikonge, unafikiri ukimwambia kosa ni lake atakuelewa? Yeye ataamini kuwa Umasikini wake unaletwa na hayo makabila. Ninafahamu sana kuwa sehemu zilizokaliwa na Wazungu zamani ziko mbele kimaendeleo (devide and Rule). Ndiyo maana ninasema kuwa SERIKALI IJITAHIDI kubadilisha maisha yao hawa kwa kuwafundisha na ikibidi hata kwa FIMBO. Joka wewe naona una zile za "ahh, makosa yenu wenyewe na UVIVU WENU". Watusi na Wahutu walichinjana kwa hayahaya. Mungu apishie mbali ila kwa mwenendo huu ..... Hakuna kitu kizuri kama kuongelea TATIZO na kuanza kufikiri namna ya kulitibu. Nyie pia mnajua TATZIO lipo ila mnasema "hiki si chanzo chake.." na mnakunja 4 kwenye kochi.
 
JokaKuu,
Naona hukusoma ujumbe wangu vizuri au umesoma ila ukaamuwa kuchukua tu yale uliyoyataka. Naomba upitie tena ujue nini nilisema juu ya UKABILA na hasa sehemu zenye rangi NYEKUNDU.

Juu ya Ukabila mie naunga mkono. Huu ugomvi ulikuwepo, upo na utaedelea kuwepo. Siyo siri kuwa makabila mengi yanawaonea wivu Wachaga, Wahaya, Wasukuma, Wakinga, Wanyakyusa ...... Ukifika Bukoba, Mwanza, Arusha/Kilimanjaro, Mbeya .... kwa kweli utashangaa kama uko Tanzania (baadhi ya maeneo). Kuna mikoa imesahaulika kabisa na tujikumbushe bajeti ya ujenzi wa Barabara ya Mramba. Sasa watu wakiona hata TANROAD iko chini ya Mchaga, na pesa zote zaenda huko kwa kweli unataka kulia. Ukifika huku kwetu Sikonge, loo ni kwa Wamasembere kweli kweli. Barabara nzuri Tabora mjini ni ile inaenda Airport na lami imeishia mita kadhaa na hapo unaanza TOPE zito hadi ile Landing lane yenyewe ni ya TOPE. Kama huamini jaribu kuvuta GOOGLE EARTH na uangalie picha ya Tabora mjini jinsi ilivyochoka, na watu wanalima Mpunga na Mahindi hadi City center. Hii siku zote italeta Cheche. Msiwe watu wa kulaumu kuwa watu wanawasha moto wakati serikali yetu imeweka kuni kavu tayari, nyasi kavu na kumwagia petroli. Hii utaiona mikoa mingi tu kama Kigoma, Singida, Lindi, Mtwara, Tanga nk. Serikali au yenyewe Ijitahidi kubadilisha maisha ya watu huko na ikishindwa basi IWALAZIMISHE hawa watu wabadili maisha yao. Wanaweza kila kitu wakitaka. Just WAKITAKA.
Ukiangalia vizuri utaona kuwa makosa nimeyatupa kwa SERIKALI na MAKABILA MASIKINI na WIVU WAO. Sijasema hapa Wachaga au Wahaya ndiyo wamesababisha hawa wawe masikini. Nimekaa Arusha/Kilimanjaro na nimeona jinsi jamaa wanavyochapa kazi na siyo kujishughulisha kama huku kwetu Sikonge. Ila kwa LIMBUKENI wa hapa Sikonge, unafikiri ukimwambia kosa ni lake atakuelewa? Yeye ataamini kuwa Umasikini wake unaletwa na hayo makabila. Ninafahamu sana kuwa sehemu zilizokaliwa na Wazungu zamani ziko mbele kimaendeleo (devide and Rule). Ndiyo maana ninasema kuwa SERIKALI IJITAHIDI kubadilisha maisha yao hawa kwa kuwafundisha na ikibidi hata kwa FIMBO. Joka wewe naona una zile za "ahh, makosa yenu wenyewe na UVIVU WENU". Watusi na Wahutu walichinjana kwa hayahaya. Mungu apishie mbali ila kwa mwenendo huu ..... Hakuna kitu kizuri kama kuongelea TATIZO na kuanza kufikiri namna ya kulitibu. Nyie pia mnajua TATZIO lipo ila mnasema "hiki si chanzo chake.." na mnakunja 4 kwenye kochi.

Nashukuru SIKONGE kwa ujumbe wako wenye kuonyesha UELEWA!
Ni kweli mpango mzima ulikuwa wa ccm kuintroduce RASMI POLICIES ZA UKABILA NA UDINI!
NI UMAFIA AMBAO WATU KAMA SISI INABIDI TUWAELEWESHE WANANCHI KABLA DIVIDE AND RULE HAIJATAKE PLACE MOJA KWA MOJA!
 
2. Mbunge kahoji; Mshahara na marupurupu ya Mrema ni ya Kifisadi. Hili halina nguvu na tena lawezakuwa Mbunge alitumia hoja hii ili kulazimisha hoja yake ya Kwanza na ya tatu (kutishia wafanyakazi) zipate nguvu.
Kama Mghana aliyekuwepo alikuwa analipwa mshahara na marupurupu hayo hayo, kwa nini Mtanzania asilipwe hivyo hivyo? Kwa nini Mtanzania aendelee kuwa Daraja la Tatu lakini wengine wabebwe na kulipwa First Class? Je Mbunge na hata Wachangiaji wengine humu tumesahau kuwa tumelia kwa muda mrefu kuhusu Mishahara midogo na kupuuzwa? Je tunasahau katika mfumo wetu mpya wa Uchumi ambao umeachana na Ujamaa, ni kuwa mishahara si maamuzi ya Kamati kuu bali ni uwezo wa ushawishi wa anayetaka kazi kutaka alipwe mshahara unaolingana na Elimu, Uzoefu, Ufanisi na Utendaji (track record)? Kuna mwana JF katoa maoni kuwa akiwa Mtanzania alipwe Shilingi kwa kufuata viwango vya mishahara ya Serikali, lakini akiwa ni Mgeni asiye Mtanzania, basi tumlipe ki-ulaya ulaya, this does not make any sense. Kwa nini ajira ya kazi hiyo hiyo iwe na mishahara ya kiubaguzi?

Kishoka,
Heshima yako. Naona na wewe umechukua maneno yangu na kama Nyerer ukayakuza ili YAPENDEZE wakati unajibu na wakati huo unakuwa umebadilisha kabisa nilichosema. Mimi si mwana siasa. Mie ni fundi Mchundo na haya majibu na maneno ya WANASIASA huwa yananitia kichefuchefu. Nyerere aliambiwa kuwa ANACHAGUA WAKRISTO kwenye baraza la mawaziri, yeye akasema "Wananishutumu kuwa nachagua WAKATOLIKI.." wakati huo wakatoliki walikuwa yeye, nani sijui na George Kahama ambaye tayari alikuwa na wake watatu. Kwa maana nyingine Mkatoliki alikuwa yeye tu.

Mimi nimesema kuwa "TANROAD ni kitengo cha serikali ya Tanzania kwa hiyo Mtu ALIPWE KATIKA TSHs na siyo Dola au Euro. Sijasema kiasi gani. Hata akipewa milion 50 kwa mwezi poa tu ila iwe Tshs. Kama yupo Tanzania na yeye ni Mtanzania kwa nini alipwe kama Mghana? Mghana ukimpa hela ya madafu ataenda kuifanyia nini Ghana? Yaani hili nalo mnalijibu KISIASA? Mie ninachosema na kutaka kutetea ni HELA YANGU YA TANZANIA na si MSHAHARA. Kila mtu anajua kuwa UKIAJILIWA kama Expert nchi fulani basi kuna vitu vingi vinaanza kuingia ndani. Sasa tusema "mnamgharamia usafiri kwenda likizo". Mghana atapewa hela zaidi kwani nauli ni kubwa. Anakuja Mkala anadai "Mbona Mghana alipewa hivi, na mimi nataka hivyo hivyo" wakati huo kwenda kwao anapanda MAMBA. Ukimpa hela ya AIR TANZANIA hapo anakuja Kishoka na kusema "kwa nini Mghana mlikuwa mnamlipa ki-ULAYA ULAYA na mie mnalipa Ki-Africa Africa..."

Ninachosema mie ni kuwa hawa ma CEO walipwe vizuri tu na lazima kwanza watafutwe Watanzania. Tukikwama Waafrica na kama hamna twende sasa popote pale. Nafikiri unaelewa nikisema KWANZA WATANZANIA, kwani tutawapa hela ya MADAFU. Akija TX basi ni hasara kwa taifa kwani huyu pamoja na mshahara mkubwa atakaopata (iwe sawa kwa wote) basi marupurupu yake yako kibao kwani HAYUKO KWAKE/KWAO.

Juu ya nani anafaa kuwa CEO wa TANROAD nilisema kuwa "itakuwa vema kama atapatikana Mhandisi aliyeongeza masomo ya management.." Kama nilivyosoma huyu jamaa ni Quantity Surveyer. Sasa huyu bwana ni MKADIRIAJI wamapesa mangapi yalipwe kwa ujenzi au ukarabati.

Kama mfanyakazi au mshauri wa kampuni ni poa sana. Nafurahi kuwa TANROAD ina mtu kama yeye. Akiweza aandae vijana wengine wengi tu kwa kuwafundisha kazi ila nina wasiwasi kama kwenye mambo ya MANAGEMENT ni mkali kama hayo ya QS. Huo ni wasiwsi wangu tu.
 
George Kahama wake wawili. Samahani nisije eleweka vibaya...
 
Kishoka,
Heshima yako. Naona na wewe umechukua maneno yangu na kama Nyerer ukayakuza ili YAPENDEZE wakati unajibu na wakati huo unakuwa umebadilisha kabisa nilichosema.

Sikonge,

Sikuwa nakujibu wewe per se na kutaka alipwe dollar. Niliposema kulipwa ki-ulaya ulaya ni ile kasumba ya kulipa wageni mishahara mikubwa lakini Wazawa tunawapunja iwe wamelipwa kwa madafu au dola!

Ulipozungumzia mishahara ya Serikali, nilikataa kwa kuwa najua Mishahara ya Serikali ni midogo mno katika ngazi zote, na ndio maana nikasema mpeni anachostahili.

Ninachokikataa mimi ni ile hamaki ambayo alianzia Mbunge na hata wachangaji wengine humu ambao wanadai eti mshahara huo ni mkubwa sana, wa kifisadi. Lakini kama tulimlipa Mghana mshahara huo huo kwa kazi hiyo hiyo, kwa nini tumnyime Mtanzania mwenzetu anapofanya kazi hiyo hiyo?

Nimekuelewa vema na nashukuru kwa ufafanuzi wako.
 
Mhafidhina,

Nitakuambia maswali ya msingi ambayo aliulizwa kwenye interview,

1. Tell us about your self
2. Why should we hire you?
3. What can you bring to our company?
4. What is your vision foer this company and its future projects?
5. What are the obstacles of buuilding good roads in Tanzania?
6. How will you handle contracts disputes?
7. How and what ways you will motivate your employees to be efficient, creative and be productive?

Hata kama aliulizwa swali la Kiufundi kama asphalt in chemical composition ngapi, ni upuuzi kutamka na ni aibu kudai eti alipewa pepa!

Mkuu,
Ninavutiwa sana na umahiri wako katika kuangalia jambo na kulitafakari kwa mapana na marefu yake....

Tukijali sana jazba na maono ya moyoni bila kuwa objective basi tutajikuta tunaendekeza majungu yasiyo na ushahidi....

Mchakato wa kupata kazi na hasa kazi zenye mvuto kama hii inayojadiliwa hapa si lelemama.... anybody who has gone through such processes atashindwa kukubaliana na hoja zinazoletwa hapa kuwa msailiwa alipewa maswali kabla...

Kama CEO huyo ameshindwa kutenda..au anakiuka ethics za kazi basi ahukumiwe kwa hayo..na siyo kwa kabila lake au urafiki na watu fulani katika jamii ya Watanzania....
 
as if to add some spice to this soup, whoever is in doubt about the FISADI connection should read that Ephraim Mrema is well connected to them trhough his mume mwenza, a goon called Macha currently in the employment of COWI. This goon is bonafide member of the Magai-Masha genge of philanderers. Whatever patronage Macha has required, he just whistles and FISADI provides. By the way they were all gathered in Monduli last XMass. Rings a bell anywhere_
 
as if to add some spice to this soup, whoever is in doubt about the FISADI connection should read that Ephraim Mrema is well connected to them trhough his mume mwenza, a goon called Macha currently in the employment of COWI. This goon is bonafide member of the Magai-Masha genge of philanderers. Whatever patronage Macha has required, he just whistles and FISADI provides. By the way they were all gathered in Monduli last XMass. Rings a bell anywhere_

WHOEVER THEY ARE...Whether they are MUSLIMS OR CHRISTIANS...Whether they are HINDUS OR NON BELIEVERS...They are all accountable for selling out our NATION AND THE PEOPLE'S FREEDOM!

Nani hajuwi kuwa mafisadi na makaburu ndio wanaishi maisha mazuri?!
Unataka kusema ni wachagga tu?

AMA WAISLAM WANAMTANDAO?

Hata kama ni wao...WOTE PAMOJA NAWAISLAM WALIOANZISHA HAYA YOTE KWA KUTUMIA MTANDAO WA ccm AMBAO NI WAISLAM TUPU NI MAFISADI!

WAKIANZIWA NA SERA YA EPA YA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA ccm WAZAZI KWA KUSHIRIKIANA NA FAMILIA YA LUKAZA NA WAKILI MALEGESI KUANZISHA MAKAMPUNI FEKI AMBAYO WACHAGGA HATA WASIOJUWA SIASA WALIPEWA PESA HIZO NA SASA KELELE ZA chadema ni ccm WADINI...

Na za ccm ni CHADEMA NI YA WACHAGGA NA WACHAGGA NI MAFISADI NA SI ccm WAISLAM!

UPO?
 
WHOEVER THEY ARE...Whether they are MUSLIMS OR CHRISTIANS...Whether they are HINDUS OR NON BELIEVERS...They are all accountable for selling out our NATION AND THE PEOPLE'S FREEDOM!

Nani hajuwi kuwa mafisadi na makaburu ndio wanaishi maisha mazuri?!
Unataka kusema ni wachagga tu?

AMA WAISLAM WANAMTANDAO?

Hata kama ni wao...WOTE PAMOJA NAWAISLAM WALIOANZISHA HAYA YOTE KWA KUTUMIA MTANDAO WA ccm AMBAO NI WAISLAM TUPU NI MAFISADI!

WAKIANZIWA NA SERA YA EPA YA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA ccm WAZAZI KWA KUSHIRIKIANA NA FAMILIA YA LUKAZA NA WAKILI MALEGESI KUANZISHA MAKAMPUNI FEKI AMBAYO WACHAGGA HATA WASIOJUWA SIASA WALIPEWA PESA HIZO NA SASA KELELE ZA chadema ni ccm WADINI...

Na za ccm ni CHADEMA NI YA WACHAGGA NA WACHAGGA NI MAFISADI NA SI ccm WAISLAM!

UPO?

Do you even understand what you have just stated?
 
Do you even understand what you have just stated?

Starting what? The truth kuwa mnaleta UKABILA NA UDINI NA KU UHUSISHA NA UFISADI?
NO...MAFISADI NI MCHANGANYIKO WA MAKABILA NA DINI ZA TOFAUTI!
AMA TUWATAJE WAHUSIKA WOTE NA HALAFU TUONE KAMA WOTE NI WACHAGGA?
CHENGE NI MCHAGGA?
KIKWETE JE?
WHAT ABOUT YOU? AMA KWASABABU WEWE NI MSUKUMA NA HUONI CHENGE ANA KOSA?
 
Sikonge,

..i will grant you the benefit of doubt ktk haya masuala ya ukabila.

..i will also speculate kwamba ulihemewa tu ulipotoa mfano kwamba Mramba[mchaga] na bajeti ya barabara ni moja ya dhuluma za serikali dhidi ya mikoa ya pembezoni.

..naomba pia nikuelimishe kwamba mradi wa barabara jimboni kwa Mramba ulianza wakati wa John Magufuli. pia mradi ule ulipewa pesa zaidi wakati wa Mramba kwasababu ulikuwa ktk advanced stage ya ujenzi. Mbunge aliyelalamika mradi wake ulikuwa ama ktk design stage au feasibility study, ndiyo maana ukapewa fedha kidogo.

..nilitegemea baada ya posting yangu ungejielimisha zaidi kuhusu miradi hiyo miwili, na pia ungeomba radhi kwa kauli yako.

..nasubiri kwa hamu kuona kama Mbunge Selelii, na wenzake, atamkaba koo Waziri wa sasa miuondo mbinu Dr.Kawambwa, kama alivyofanya kwa Mramba mwaka jana.

..Basil Mramba ana kashfa[kuchapisha noti chafu na kampuni ya kijerumani, misamaha ya kodi...] nyingi tu kama mwanasiasa, lakini hili la kusema amedhulumu barabara za jimboni kwa Lucas Selelii na wenzake, siyo kweli.

..tofauti uliyoitaja kuhusu Kilimanjaro,Mbeya,Arusha, kulinganisha na mikoa ya pembezoni ni suala kihistoria. ule msingi[elimu,miundo mbinu...] uliowekwa na wamisionari na wakoloni ndiyo unaowapa ahueni mikoa hiyo. vinginevyo nchi nzima imeathirika kutokana na uongozi mbaya wa Tanu na baadaye CCM.

..zaidi siamini kama Mchaga,Mhaya,Mnyakyusa ana akili zaidi, au ni mjanja zaidi, au ni mchapakazi zaidi, kuliko Muha, Mnyaturu, Makonde etc etc. tofauti za makabila hayo ni exposure tu.

..naamini kabisa kabisa kwamba Waha,Wanyaturu,...wangepewa historical opportunities walizopewa Wachaga,Wahaya,..basi leo hii Kigoma,Singida,Mtwara, ingekuwa inasifika kwa "maendeleo" na Kilimanjaro,Kagera,..ingekuwa ndiyo mikoa ya pembezoni.

..hakuna hata siku moja nchi nzima[makabila yote,mikoa yote]itakuwa ktk hatua moja ya maendeleo. siku zote kutakuwepo na maeneo yaliyopiga hatua zaidi kulinganisha na mengine. kitu cha kuzingatia ni kujaribu kuzielewa tofauti hizo, na zaidi eneo moja kujifunza toka eneo lingine. mara nyingine maendeleo hupatikana kwa kuiga.

..nashauri kabla ya kuwashutumu Msuya na Mramba, tuwabane kina Samwel Sitta,Rashidi Kawawa,Maokola Majogo,Ben Mkapa,Nalaila Kiula, Anna Abdalah, Jakaya Kikwete,Paul Kimiti,Chrisant Mzindakaya...wajieleze kwanini wameshindwa kuhimiza maendeleo ktk mikoa ya kusini na mingine ya pembezoni.
 
Nimefuatilia mjadala huu kwa makini sana ingawa naweza kuwa nimeruka baadhi ya posts kwa vile TANROADS ni taasisi moja ya serikali inayonikera sana kutokana na nchi yetu kuwa na barabara mbovu. Baada ya kuchambua habari mbalimbali zilizopatikana hapa nimegundua kuwa:

  1. Mbunge Mporogomyi alikosea sana kumsakama hadharani CEO wa TANROADS kwa kutumia kikao cha bunge. Ingawa lengo lake lilikuwa ni kuhoji mazingira ya ajira za huyo CEO, lakini alivyotoa mada yake ilikuwa ni wazi kuwa alikuwa anamshambulia CEO yule kuwa hafai kazi na alipendelewa kuwekwa madarakani pale bila sifa za kutosha ili kusudi aweze kupewa malipo makubwa namna ile. Ni vizuri mbunge angemuuliza waziri kwa pembeni na endapo asingeridhishwa na majibu ndipo angetumia kikao kile. Kwa pale Mporogomy alitumia nyumba ya wananchi vibaya. Hata marekani ni jambo la kawaida sana kwa wanachi kwenda kutoa malalamiko yao kwa seneta wao kama hawaridhishwi na utendaji wa afisa au idara fulani ya serikali. Seneta hachukui malalamiko yale moja kwa moja hadi bungeni, badala yake huifuata idara inayohusika na kujaribu kuelewa kulikoni kabla hajachukua hatua yoyote.
  2. Napenda kuwakumbusha kuwa huyu Mporogomy alikuwa ni naibu waziri wa fedha katika serikali ya kwanza ya Mkapa na alifanya ufisadi mkubwa sana hadi akalazimishwa kujiuzulu. Simshangai sana anaposhupalia mshahara wa CEO wa TANROADS
  3. Kulingana na qualifications za bwana Mrema kama zilivyoandikwa kwenye gazeti la Majira, kama zote ni kweli basi sina shaka kabisa kuwa anazo sifa za kutosha kuweko katika madaraka yale. Kuhusu utendaji wake kazini, hilo ni jambo linalotakiwa kuwekwa katika kumbukumbuku ili kusudi lije lijadiliwe wakati wa ku-renew contract yake. Nina imani kabisa kuwa madaraka makubwa kama yale yanahitaji kuwa ya mkataba wa muda maalum kati ya miaka mitatu au minne, na siyo indefinite kama mwalimu.
  4. Jambo linaloshangaza ni ukubwa wa malipo wanayopewa viongozi wa nchi hii. Baada ya kupitia mchakato wa malipo ya Bwana Mrema, ni kama anapokea zaidi dola 17,000 kwa mwezi ukiunganisha marupurupu yote. Hiyo ni zaidi ya dola 200,000 kwa mwaka, ambazo ni zaidi ya mshahara wa Makamu wa Rais wa Marekani. TANROADS siyo kampuni la biashara, ni kama kitengo cha serikali tu, wala hakiingizi mapato yoyote serikalini, badala yake ni kitengo kinachuhukua fedha kutoka serikalini. Malipo makubwa ya BONASI yana maana gani. BONASI huwa ni malipo yatokanayo na kuzalisha zaidi ya malengo, na ni malipo ambayo siyo fixed bali yanategemea na jinsi malengo yalivyovukwa, yakiwa yanatathminiwa kila mwaka. Vile vile bonasi hutolewa kwa wafanya kazi wote wa kampuni ingawa kwa viwango tofauti. Je kweli TANROADS huzalisha nini na huzidi malengo yao kwa kiasi gani kufikia uamuzi wa kumpa BONASI kubwa vile huyu CEO? Je wafanyakazi wengine wa TANROADS pia wanapata bonasi hiyo pia? Nadhani hili la malipo kweli linahitajiwa kutazamwa kwa makini. Najua kuna vitengo vingi vya serikali ambako Ma-CEO wanalipwa kiasi kikubwa vile: tuliwahi ikuambiwa kuwa Gavana wa BOT alikuwa analipwa zaidi ya hapo ukichukulia mshahara wake wa dola 12,000 na marupurupu ya zaidi ya dola 7,000 kwa mwezi. Nimewahi kuambiwa kuwa Bosi wa TRA analipwa karibu dola 15,000 (sina uhakika na namba hiyo) kwa mwezi pamoja na mrupurpu za zaidi ya dola 8,000 kwa mwezi.
 
Kwa mtazamo wowote ule tanroads ni vyema ikachunguzwa kwani kama kweli aliyoyasema mp ni ya kweli basi liko tatizo kubwa kuliko unavofikiria.

kwa kweli Tanzania tuna kazi kubwa sana hasa kwenye swala la utawala bora. kila kitu kinachofanyika tz ni politics tuu. mimi sijali analipwa shilingi ngapi, amefanya kazi world bank hata kama ingekuwa IMF au UN, swala ni kwamba kwa nini hakuwepo kwenye wale 4? Eti kuna mtu anatoa argument kuwa alikuwa best student form 4 na 6, kwa taarifa yako watu kama hao ni wachache sana ambao ni watendaji wazuri, watu kama hao wanajua tuu kumeza na kutapika kwenye mtihani lakini real life practise hawana lolote.

The major argument hapa ni alipataje hiyo kazi? Swala zima la usaili lilifuatwa? Kama alitolewa tuu alikokuwa na kuingizwa hapo ilikuwa kwa maamuzi ya nani na kwa maslahi ya nani?
 
Nimefuatilia mjadala huu kwa makini sana ingawa naweza kuwa nimeruka baadhi ya posts kwa vile TANROADS ni taasisi moja ya serikali inayonikera sana kutokana na nchi yetu kuwa na barabara mbovu. Baada ya kuchambua habari mbalimbali zilizopatikana hapa nimegundua kuwa....

Mwalimu Kichuguu,

You are always objective, nashukuru kuchangia kwakio hapa na hasa kipengele cha mwisho ambacho nimekuwa nakifikira tangu nisome mshahara wa huyu ndugu na kujiuliza mantiki mazima ya mishahara na Marupurupu Tanzania.

Wakati tulipokuwa na Scopo, marupurupu yalikuwa ni kibwagizo ili kuongeza kipato kutokana na mishahara midogo.

Tuko kwenye uchumi na uendeshaji tofauti na kama tumediriki kupunguza mzigo kwa mwajiri kulipia huduma kama afya kwa mwajiriwa, sielewi ni kwa nini Mfanyakazi wa Shirika au Serikali alipwe mshahara kisha apewe marupurupu.

Mfano, CEO wa Tanroads, analipwa marupurupu ya gari, nyumba, likizo na kadhalika. Kwa nini hakupewa Mshahara mmoja ambao atamudu kila kitu kwa kutumia huo mshahara mmoja?Je haya marupurupu yanatozwa kodi ya mapato kiasi gani?

Ni mambo kama haya ya kipuuzi yanayofanywa na Serikali ya kutumia njia fupi na chafu kama kisingizio cha Marupurupu yanapaswa kuachwa. Haya marupurupu na masurufu hayana ulazima na ni mzigo mkubwa kwa Mashirika, Taasisi na hata Serikali yenyewe.

Kwa kuwa Serikali inakataa kubadilisha mfumo wa Mishahara nchini, basi inatumia mwanya kuwalipa fidia wale wachache ambao ni Wateule, walipwe Mishahara, Marupurupu na Masurufu ili waendelee na ajira na kulitumika Taifa badala ya kukimbia nje.

Je ni kosa la Mrema kulipwa Mshahara na marupurupu haya? hapana si kosa lake, amekuta mfumo na hivyo kaajiriwa na ataendelea kulipwa kwa kutumia mfumo uliopo mpaka siku Serikali itakapositisha mfumo wa kufidia mishahara midogo kwa vitu kama Marupurupu na Masurufu.
 
..nadhani Watanzania tunaelekea ktk kuamini kwamba maendeleo yanapatikana kwa upendeleo tu. hatuamini tena ktk kufanya kazi kwa bidii, kujitolea, ushirika, etc etc.
Maendeleo tanzania ni kweli yanapatikana kwa upendeleo maana wakati wa kampeni za ubunge si ndivyo tunasadikishwa? kwamba ukichaguliwa kuwa mbunge utafanya hiki na kile katika jimbo lako. Kana kwamba tayari una pesa vile. Ndiyo sababu MP hata akivurunda lakini akapata ngekewa ya kupata u minister basi hata kama ni mbovu kiasi gani jimboni wataendelea kumpatia tu kula(sorry kura).
Na utaona kila waziri anajaribu sana kuvutia kwao vijimiradi vinapotokea. Na hii sio siri. Hata ungepewa wewe u minister kesho tu ungepeleka kamradi kwenu huko.
 
Mrema Ndugu Yangu Huwezi Kudumu Tena Hapo Kwa Kuwa Umegusa Sehemu Ambazo Hata Mwenzio Ado Alikuwa Akiziheshimu...contractor Mpiluka Alikuwa Akidai Kwa Haki Kabisa Pesa Zake Za Contract Bilioni Kumi...wewe Kwa Kujifanya Unajua Hesabu Ukajidai Kereevaluate Kazi Yake Na Kumpelekea Notice Arudishe Bilion Mbili,ukamgeuzia Kibao.ukajidai Kuwaondoa Vigogo Waliokuwa Hapo Miaka Na Miaka Eti Wanakula Rushwa.wenye Hekima Walikuonya Hukusikia Na Sasa Yanakutokea Puani.na Huu Ni Mwanzo Tu Kaa Tayari Kwa Mambo Matamu Zaidi
 
Fisadi Mtoto Kazi Anayo Huo ......na Atoki Huko!!!!!
Tatizo Amekuwa Akiwabania Sana Wenye Haki Zao Huku Akila Mabillion
Haoni Mwenzio Wa Tra Anakula 18,000 Watu Wametulia Kwasababu Anawapa Watu Haki Zao Na Kula Na Vipofu!!!!!!!!!!!!!
Noshaa Mleu!!!
 
Jamani kuwa rafiki na Lowasa ni kosa?. Lowasa ni binadamu kama walivyo binadamu wengine. Amesoma na watu, ameenda jeshini na watu, amefanya kazi na watu. Na hakuna binadamu aliye kamili 100%, hivyo Lowasa kama binadamu amefanya makosa kwa hili la Richmond na amewajibika ili uchunguzi uendelee kufanywa vizuri. Kwa hili pia sioni sababu ya kumsakama Mrema kuwa rafiki wa Lowasa. Binadamu yeyote anayo haki na uhuru kujichagulia marafiki hivyo kwa hilo sioni ubaya kabisa.

.

Lowassa is the modern times KAMBONA....

Tanzanianjema
 
Back
Top Bottom