Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna kaukweliKwa hiyo hivi sasa GUGU ina-trend siyo mkuu.
Anyway pia watu wanalalamika kupewa mi-vitamin na midawa mingine ili miela ya kulipa iwe mingi sina uhakika lkn madai haya yapo
Upo sahihiKwanza tujiulize kwanini watu wana-Google?
Tatizo linaanzia kwny mfumo wa Afya, mfumo ukiwa dhaifu lazima watu watafute njia mbadala
Mf.Mimi binafsi nilikuwa natatizo fulani la kiafya nimeenda hospitali kubwa mara kadhaa naona na Daktari ananiandikia vipimo fulani fulan nafanya vyote sioni tatizo. Nikirudi kusomewa majibu anakwambia shida hii na hii sina so Mzee uko vizuri kabisa
Nakuaje vizuri wakati naumwa; pengine vipimo alivyonipa haviendani na tatizo langu. Nilirudi kwenye Google nikatumia muda mwingi na umakini na nikagundua tatizo langu nikasoma vyema side effect ya kila njia ya matibabu nikaanza. Alhamdulillah niko vyema kabisa na imenisaidia hata kujua chanzo cha tatizo lile ni nini na nimebadili kabisa life style iliyokuwa inanisanabishia tatizo
Drs wengi siku hizi wana fail kwenye ku-identify tatizo na ndio hapo kwny tatizo kuu