Epuka mihemko ya kijinga ili kulinda amani ya nchi yako

Right Marker

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
194
Reaction score
625
UZI MAALUM
Ikiwa taifa lolote litaingia kwenye machafuko (vita au mapigano ya wenyewe kwa wenyewe) kwasababu ya siasa, dini, makabila, n.k - yafuatayo ni baadhi ya matokeo ambayo yanaliandama taifa lililoingia kwenye machafuko.

Kabla sijaorodhesha matokeo hayo kwanza rejea mataifa ya Afrika yaliyowahi kupitia kwenye hiyo shida kama vile Libya, Somalia, DRC, Burundi, n.k. Sasa naorodhesha matokeo kadhaa ya machafuko kama ifuatavyo;

1. Vyuoni, shuleni, madrasa, na ibadani kote hakutaendeka wala hakutakalika.

2. Maeneo yote ambayo ni vitovu vikuu vya biashara, kama vile Kariakoo hakutaendeka wala hakutakalika.

3. Kwenye makampuni, maofisini, na maeneo yote ya kazi hakutaendeka wala hakutakalika.

4. Sheli za mafuta zitafungwa, wafanyakazi wataogopa kufika kazini, wakulima hawatazungusha mazao yao sokoni, wajasiriamali wa maduka, masoko, n.k - hawatafungua biashara zao.

5. Njaa, ukame, magonjwa, vifo, na uhalifu wa kiwango cha juu - vyote vitatesa wananchi hasa wanawake, watoto, na wazee.

NB: Kitakachofuata ni wananchi wenyewe kujuta, na wakati huo watu waliojipata kimaisha watakuwa wameshasafiri na familia zao kwenda nje ya nchi. Epuka mihemko ya kijinga ili kulinda amani ya nchi yako.

RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM
 
Kupigana kunaleta kuheshimiana kwa namna fulani hivi.

Watoto wa vigogo wa CCM wametuzoea vibaya sana mpaka wanasema hadharani kuwa wanaiba kura.

Haya ni mazoea ya kiseng€ sana.
 
Heshima ya Rai inaletwa kwa Mapigano Nchi nyingi za Africa Hawaeshimu maamuzi ya Raia pia Mamlaka haieshimu Uchanguzi na Box la kupigia kura.
Bora Mapigano Ili Baadae kue na Heshima kwa Raia.
 
Bila vita haki haiwezi kupatikana, bila kuipambania haki huwezi kupewa haki. Amani bila haki ni utumwa.
 
Hivi unadhani vijana ni wajinga kiasi hicho kwamba hawataki amani ya nchi? Nyie ndio mnaovuruga amani ya nchi kwa kutokutenda haki kwenye uchaguzi na mambo mengine. Kwanza shukuruni vijana wa nchi hii hawana mihemko hiyo ya kisiasa, wao ni ushabiki wa mpira, simba na yanga, ligi za ulaya na kubeti. Hiyo mihemko umeina wapi?
 
UZI MAALUM
Ikiwa taifa lolote litaingia kwenye machafuko (vita au mapigano ya wenyewe kwa wenyewe) kwasababu ya siasa, dini, makabila, n.k - yafuatayo ni baadhi ya matokeo ambayo yanaliandama taifa lililoingia kwenye machafuko.

Kabla sijaorodhesha matokeo hayo kwanza rejea mataifa ya Afrika yaliyowahi kupitia kwenye hiyo shida kama vile Libya, Somalia, DRC, Burundi, n.k. Sasa naorodhesha matokeo kadhaa ya machafuko kama ifuatavyo;

1. Vyuoni, shuleni, madrasa, na ibadani kote hakutaendeka wala hakutakalika.

2. Maeneo yote ambayo ni vitovu vikuu vya biashara, kama vile Kariakoo hakutaendeka wala hakutakalika.

3. Kwenye makampuni, maofisini, na maeneo yote ya kazi hakutaendeka wala hakutakalika.

4. Sheli za mafuta zitafungwa, wafanyakazi wataogopa kufika kazini, wakulima hawatazungusha mazao yao sokoni, wajasiriamali wa maduka, masoko, n.k - hawatafungua biashara zao.

5. Njaa, ukame, magonjwa, vifo, na uhalifu wa kiwango cha juu - vyote vitatesa wananchi hasa wanawake, watoto, na wazee.

NB: Kitakachofuata ni wananchi wenyewe kujuta, na wakati huo watu waliojipata kimaisha watakuwa wameshasafiri na familia zao kwenda nje ya nchi. Epuka mihemko ya kijinga ili kulinda amani ya nchi yako.

RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM

..chanzo cha machafuko ni watawala kutokutenda HAKI.

..watawala wakisimamia HAKI hakuna atakayetamani kuvunja amani.

..sasa hivi Tanzania watawala wanawatendea wapinzani kana kwamba ni raia wa daraja la chini katika nchi yao.
 
Tunawaomba msitufikishe huko. Fanyeni mabadiliko uchaguzi uwe huru na wa haki. Mtu akishinda aashinde kwa haki na atangazwe alieshinda. Hiyo ndiyo demokrasia.
 
Back
Top Bottom