Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,804
- 10,715
Nimeona nianzishe thread maalum kwa ajili ya kufafanua program ambazo kila uchao zinatangazwa humu jukwaani kama njia rahisi ya kujipatia fedha mtandaoni ilhali ni Ponzi. Mfano wa program hii ni BTCClock.io kama alivyopost Shafi_Abeid kwenye hii thread Wekeza kwenye biashara ya Bitcoin upate faida kila dakika. Ni vema watu wakaelewa ni nini hasa dhumuni la program hizi kabla hawajaliwa pesa zao.
HYIP (High Yield Investment Program ) ni aina ya Ponzi scheme (kama ile ya DECI) isipokuwa tu hizi hufanya kazi mtandaoni. Program za aina hii hutoa ahadi ya malipo makubwa ndani ya muda mfupi. Kwa mfano BTC Axis LTD inajigamba kutoa faida kama ifuatavyo:
10.5% - 20% Hourly For 10 Hours
103% - 200% After 1 Day
120% - 800% After 5 Days
900% - 1200% After 15 Days
Vip Plans : 1500% After 5 Days , 2000% After 7 Days , 7000% After 10 Days
Hivyo, ni rahisi kwa asiyeelewa kuingia kichwa kichwa kwa tama ya faida ya chap chap. Lakini kimsingi ni bahati nasibu tu.
Ziko program nyingi sana zinazoendesha Ponzi za aina hii. Hukusanya fedha kutoka kwa watu mbalimbali kisha wakipata mpunga wa kutosha hupotea hewani na kuacha kilio. Leo nimechoka sana hivyo siwezi kuanika kwa kina. Nitaendelea kesho wadau.
Part II
Wakuu, niliahidi hii leo kuleta kwa kina maelezo kuhusu aina hii ya utapeli ingawa inaonekana ni mpya kwa wengi.
Cryptocurrency (Bitcoin) mining
Hii ni biashara halali kabisa mtandaoni. Unawekeza pesa zako kwa kampuni zinazofanya bitcoin mining halafu wewe unasubiri gawio. Gawio hili hupatikana baada ya kukokotoa ggharama za uendeshaji ambazo kimsingi ni kubwa mno. Kwa kiasi kikubwa ni ngumu kupata faida kwenye haya makampuni. Kwa mfano kampuni zinazoheshimika kwa kulipa wateja wake kwa muda sasa ni Hashflare na Genesis Mining ambazo hata hivyo itakuchukua zaidi ya mwaka kurudisha tu mtaji wako kabla ya kuanza kupata faida ambayo ni ndogo kweli kweli. Mara nyingi ROI huwa ni negative. Hizi hapa baadhi ya cloudmining co pamoja na siku utakazochukua kurejesha mtaji wako.Sehemu ya comment utakuta mawazo ya waliowekeza wengi wakilalamika kupata hasara
Hyip
High Yield Investment Programs ni kama nilivyoeleza hapo juu. Hizi website zinazoendeshwa na wajanja ili kujipatia kipato. Wamiliki hujitahidi kuzipamba na kuzifanya zionekane legit (halali) kwa kutoa habari za uongo. Mara nyingi watasema wanatumia wataalamu wa hali ya juu kufanya biashara zenye faida kubwa. Mfano uchimbaji madini, betting, uchimbaji mafuta n.k.
Kufuatia kuibuka kwa cryptocurrencies mfano bitcoin, matapeli hawa wamegeukia biashara hiyo na sasa wanajificha nyuma yake. Kampuni nyingi zinadanganya kufanya cryptocurrency mining lakini kiukweli hazifanyi hivyo. Wanategemea watu wavutike wawekeze pesa nyingi halafu wanapotea na pesa hizo.
Yako makampuni mengi mno yanayofanya hivi, lakini yote yana sifa moja kubwa, yanaibuka na kupotea ndani ya mwaka mmoja tu (kwa yale yanayodumu sana). Katika kipindi hiki yataonesha kuwa ni halali kwa kulipa gawio kama kawaida. Hii inafanyika ili kuwashawishi watu kwani wengi huanza kuwekeza mitaji midogo kwanza kupima uaminifu. Chanzo pekee cha mapato ni kuingiza watu (members) wapya wawekeze.
Makampuni haya hayako regulated (hayasimamiwi na taasisi yoyote ya kifedha inayojulikana). Hivyo hupotea kimya kimya. Hutumia usajili fake (nitatolea mfano hiyo kampuni pendwa ya btcclock.io). Kuna websites ziitwazo HYIP MONITORS ndio hutoa mwongozo kama ni kampuni ipi inalipa ama hailipi. ONYO: sites hizi (hyip monitors) zina ushirikiano mkubwa sana na matapeli hawa. Hupewa gawio ili zitoe rating nzuri kuwaaminisha watu wawekeze. Sasa angalia hapa chini hii hyip monitor mojawapo ikipigia debe hizo sites:
Kisha tazama hizi ambazo zimeacha kulipa na kupotea na pesa za “wawekezaji”
Btcclock.io
Mimi sio kwamba nina chuki na hawa wanaotangaza hii program, lengo lamgu ni kionesha kuwa hii biashara ni high risk. Kwanza ifahamike kuwa katika hatua za awali kampuni hizi hulipa fedha mpaka pale watakapoona wamepata kiasi watakacho hupotea.
Nasikitika kusema kuwa btcclock.io ni hyip. Iko kwenye hyp monitors list kama inavyoonesha hapa
Kwa sasa bado inalipa, lakini ni kwa muda gani, hakuna ajuaye.
USAJILI:
imesajiliwa chini ya kampuni iitwayo 'LUCKY TIMES LIMITED'
Mmiliki wake anajiita David STRIVAY
Anuani yake ni “virtual address.” Maana yake hii hapa:
A virtual office is a business location that exists only in cyberspace. A virtual office setup allows business owners and employees to work from any location by using technology such as laptop computers, cell phones and internet access.
Certificate yao ni fake na wameiweka kiasi ambacho huwezi kuisoma kiurahisi
Director ni yeye mwenyewe, kampuni haina mtaji wala uwekezaji wowote.

Itaendelea……………