Erasto Mfugale: Kilichotokea kazini sisi hatujui

Erasto Mfugale: Kilichotokea kazini sisi hatujui

Kama imeibua madudu katika utendaji wako!! na hukutegemea! na hujuwi hatua zipi zitakufata!! lazima uzime!!Nawaza tuu
Pengine kuna mtu alimtonya kuwa mzee umenasa ripoti ya BOT. Sasa hizo safari za dodoma ghafla ghafla veepe.
 
Erasto Mfugale: Kusema kweli hatukuwa tumepata taarifa dhahiri hata imetokea nini kwasababu mimi Jumapili iliyopita nilikuwa kwake Temboni, nimekuwa na mazungumzo naye mpaka saa saba usiku lakini akaniambia kesho nina kikao kidogo kule Dodoma, kwahiyo nitatoka na ndege ya mchana. Nikamuaga nikasema naenda.

Alivyokuwa kule, mtoto wake Aron Mfugale alikuwa anaumwa pia akamtakia hali. Asubuhi amepata chai pale nyumbani kwake Dodoma, akatoka kwenda kazini.

Sasa kilichotokea kazini sisi hatujui, mwisho wa siku nashkuru wizara ya ujenzi kupitia Edgar Msigala nikapigiwa simu lakini akaona hatuelewani, baadae Hija akapiga simu na akaniambia moja kwa moja Engineer amefariki dunia, nilikuwa barabarani Bagamoyo, nilitaka nigongwe na gari maana sikuwa nimetegemea kwasababu jana yake mimi nimekuwa na dada yangu, Frida Mfugale alikuwa na andiko, akasema mimi silielewi peleka kwa kaka yako, Frida ilikuwa aje Bagamoyo kwaajili ya usaidizi wa hilo andiko ili liwe andiko makini.

Basi ni maajabu, sijui kimetokea nini. Tumefika jana Dodoma, tunawashkuru serikali, tumeenda hospitali, tumefatilia ile nyaraka, wanasema hatujui ugonjwa, sasa kulikoni?

Mgonjwa alikuja ameshafariki, alikuwa wapi? Baadae habari zinasemekana alikuwa kazini, sisi hatukuelewa kabisa, tukaendelea kuchanyikiwa, kusema kweli ilituuma kweli lakini hata hivyo Binadamu njia yake ni moja.

PIA, SOMA=> Waziri Chamurilo: Familia(Mfugale) wameonyesha ombwe kwamba ilikuwa haifahamu, Mhandisi Mfugale alisema anajisikia vibaya kikaoni

Tutasema na Kuhisi kila Jambo kwa Upuuzi wetu baadhi ya Waswahili, ila ninachojua kila Mwanadamu hata awe nani automatically tu ni Marehemu mtarajiwa na muda wake wa Kufa ukifika atakufa tu.

Watanzania baadhi yetu sasa tunaanza Kupanda Mbegu mbaya sana ya Kuhisi kila Mtu Mkubwa au Maarufu anapokufa tu basi kuna Mkono wa Mtu hasa Maadui zake iwe Serikalini au katika Jamii.
 
Ukiwa na akili ya aina hii kuchukulia kila jambo ni mapenzi ya Mungu utapotea. Hata Yesu aliuwawa na wanadamu.
 
Ukiwa na akili ya aina hii kuchukulia kila jambo ni mapenzi ya Mungu utapotea. Hata Yesu aliuwawa na wanadamu.
Ni mapenzi ya mungu pia
Maana yeye ndo alipanga kumtoa mwanae wa pekee sadaka ili kuokoa mataifa
 
Erasto Mfugale: Kusema kweli hatukuwa tumepata taarifa dhahiri hata imetokea nini kwasababu mimi Jumapili iliyopita nilikuwa kwake Temboni, nimekuwa na mazungumzo naye mpaka saa saba usiku lakini akaniambia kesho nina kikao kidogo kule Dodoma, kwahiyo nitatoka na ndege ya mchana. Nikamuaga nikasema naenda.
Kaka yake ndiye alikuwa msimamizi wa upigaji wa mwendazake, mpaka wakapeana MFUGALE TOWER,bila shaka hata mpunga mwingi was mwendazake alikuwa nao
 
Back
Top Bottom