Erasto Mfugale: Kusema kweli hatukuwa tumepata taarifa dhahiri hata imetokea nini kwasababu mimi Jumapili iliyopita nilikuwa kwake Temboni, nimekuwa na mazungumzo naye mpaka saa saba usiku lakini akaniambia kesho nina kikao kidogo kule Dodoma, kwahiyo nitatoka na ndege ya mchana. Nikamuaga nikasema naenda.
Alivyokuwa kule, mtoto wake Aron Mfugale alikuwa anaumwa pia akamtakia hali. Asubuhi amepata chai pale nyumbani kwake Dodoma, akatoka kwenda kazini.
Sasa kilichotokea kazini sisi hatujui, mwisho wa siku nashkuru wizara ya ujenzi kupitia Edgar Msigala nikapigiwa simu lakini akaona hatuelewani, baadae Hija akapiga simu na akaniambia moja kwa moja Engineer amefariki dunia, nilikuwa barabarani Bagamoyo, nilitaka nigongwe na gari maana sikuwa nimetegemea kwasababu jana yake mimi nimekuwa na dada yangu, Frida Mfugale alikuwa na andiko, akasema mimi silielewi peleka kwa kaka yako, Frida ilikuwa aje Bagamoyo kwaajili ya usaidizi wa hilo andiko ili liwe andiko makini.
Basi ni maajabu, sijui kimetokea nini. Tumefika jana Dodoma, tunawashkuru serikali, tumeenda hospitali, tumefatilia ile nyaraka, wanasema hatujui ugonjwa, sasa kulikoni?
Mgonjwa alikuja ameshafariki, alikuwa wapi? Baadae habari zinasemekana alikuwa kazini, sisi hatukuelewa kabisa, tukaendelea kuchanyikiwa, kusema kweli ilituuma kweli lakini hata hivyo Binadamu njia yake ni moja.