dalalitz
JF-Expert Member
- Sep 6, 2013
- 3,423
- 1,987
Hili lijamaa ni libobevu kwenye Mapigano Majini ( US-NAVY SEAL) 'listahafu' na pia lenye Mapesa yake mengi tu.
Sijajua iwapo limetumwa au ni vipi lakini, limenukuliwa likitamka Uozo huo unaoweza kumchefua Muafrika yeyote.
Kauli hii inasikitisha.
Kuona kuwa inafaa mwingine kutawaliwa, tena Zama hizi?
Anasema Waafrika wanashindwa na hawawezi kujisimamia wenyewe na kuwa Viongozi wa Kiafrika ni Waporaji Mali wanaojinufaisha wenyewe na wafanya matanuzi wakubwa Ughaibuni kwa Mali za Waafrika Masikini wa kawaida.
Phew!
Ndio, ni kweli na wazi kuwa yapo makandokando yanayochefua lakini haiwezi kuwa kwa Viongozi wote na kwa Afrika yote na kwamba basi suluhisho liko kwa wao 'Weupe'.
Kufikia hatua ya kuona kuwa ni sahihi na suluhisho pekee kwa mwingine atawaliwe hii amelitiliza.
Ni kejeli, ni dharau ni kutweza Waafrika wote.
Kwa maneno yake, anadhani ni wakati Wanagharibi wafikirie kuitawala AFRIKA tena YOTE.
Kinachosikitisha zaidi,
Anadhani wao ndio suluhisho.
Hata hivyo, Waafrika tujitafakari sana.
Yanatokea haya kwakuwa tunawapa sababu na mianya ya wao kuona wanaweza kufika huku.
Siku si nyingi hatahivyo unaweza ukasikia lijamaa lipo Afrika limekuja kupumzika na Familia yake.
Nadhani hawa ndio watu wa kuwafungia wasiingie Afrika kabisa.
Nawasilisha.