GE2025 Eric Shigongo adai Buchosa kuna watu wamesambaza pesa ili wamuondoe kwenye jimbo lake

GE2025 Eric Shigongo adai Buchosa kuna watu wamesambaza pesa ili wamuondoe kwenye jimbo lake

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hatukutaki Shigongo, tangu tumekuchagua miaka mitano ilopita hatuja kuona tena! Hautufai kabisa ulitoa ahadi ya kututetea kupunguziwa kodi ya majengo yetu kutoka shs: 1,000/= hadi mia mbili kwa hatua lakini mbadala wake tumeminywa zaidi ya mwanzo.
Mbona aliahidi kutuletea t-shirt na ametimiza
 
Wajumbe Huu ndio muda wa kupiga pesa lakini akili kumkichwa.Kupiga kura ni siri yako🤔
 
Shigongo atashinda bila shaka, wananchi wengi wa buchosa wanamkubali sana amewafanyia mengi mazuri jimboni Tizeba anapoteza pesa zake tu
 
Lazima atang'oka tu, sio chaguo la wanabuchosa, aliingizwa na jiwe kwa dhulma
 
Wakuu mi nazidi kushangaa tu juu ya hawa wa mama mitano tena jinsi wanavolalamika huyu anasema wanataka kumtoa Katka jimbo mwingine mke wake katekwa na kuchomewa gari,mi niirdhani chadema tu ndo tunateseka kumbe hata wao wanatesana,,kweli nimeamini ukimuacha nguruwe alietoka kuzaa na vitoto vyake njaa ikimkamata anakula vitoto vyake ndiomana nguruwe Ni HARAMU.
 
Kwani Shigongo ndio mmiliki wa Jimbo la Buchosa, hadi aseme jimbo lake? Kuna watu wa ajabu sana
 
Wakuu,

Inashangaza sana kuona mtu ambaye alikuwa anahonga wananchi Matisheti analalamikia kuhusu rushwa kwenye Uchaguzi

Yaani hapa kasema kabisa yeye hana hela na kwamba huko Buchosa kuna watu wanasambaza hela ili wachukue nafasi yake.

"Mtakachokifanya kesho wazazi kisitegemee ni kiasi gani cha pesa mtu ametoa. Uongozi haunuliwi hatuwezi kutengeneza taifa la watu wanaonunua uongozi. Jimbo hili fedha zinamwagwa kila kona. Wazazi wangu hii sio sawa na Chama Cha Mapinduzi kinakemea hili jambo"

Natumaini ACT na CHAUMMA wanaangalia kwa umakini mkubwa nini kinaendelea kwenye mchakato wa CCM

Yaani kama huko CCM watu washaanza kumwaga hela na kuchezeana rafu, itakuwaje sasa ikiwa mgombea wa CCM na mpinzani?


Kwani alishapatiwa hati miliki ya jimbo?
 
Ndio maana wenya akili hawapigi kura, mtu anatoa pesa apate ubunge ili akakutumikie wewe!!?
 
Wakuu,

Inashangaza sana kuona mtu ambaye alikuwa anahonga wananchi Matisheti analalamikia kuhusu rushwa kwenye Uchaguzi

Yaani hapa kasema kabisa yeye hana hela na kwamba huko Buchosa kuna watu wanasambaza hela ili wachukue nafasi yake.

"Mtakachokifanya kesho wazazi kisitegemee ni kiasi gani cha pesa mtu ametoa. Uongozi haunuliwi hatuwezi kutengeneza taifa la watu wanaonunua uongozi. Jimbo hili fedha zinamwagwa kila kona. Wazazi wangu hii sio sawa na Chama Cha Mapinduzi kinakemea hili jambo"

Natumaini ACT na CHAUMMA wanaangalia kwa umakini mkubwa nini kinaendelea kwenye mchakato wa CCM

Yaani kama huko CCM watu washaanza kumwaga hela na kuchezeana rafu, itakuwaje sasa ikiwa mgombea wa CCM na mpinzani?


Na hapo hizo ni fedha za watia nia. Bado wagombea
 
Shigongo amemshinda mpinzani wake mkubwa Tizeba Kwa kishindo wajumbe wamekula pesa zake kura kwa shigongo
 
Back
Top Bottom