Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shule ya upili ndio ipi hiyooo
Second-ary = u-pili
Nimeskia hii:
1. J. Zuma ni form 4 ya kwao!
2. Bakhresa wanasema hajamaliza primary sch!
3. Sumaye wanasema alikuwa na diploma wkt anapata u-pm!
4. Wanasema MZEE RUKSA alisoma madrassa tu!
Wanawataja wengi zaidi!
shigongo aache uongo sikamakuza nsumba boys kidato cha sita asiuhadae ulimwengu watu wa igoma mwanza tunamjua shigongo vizuri tu asiwadanganye
Hata Davis Mosha alikuwa anauza wese sheli kibaha.
Kibaha hakun Shell.
Zuma hajawahi kufika sekondari mkuu, jiridhishe wikipedia.
Hahahaaaa,kwa hiyo kibaha yote hakuna sheli mkuu?nilikua sijui hii
Mkuu ni kweli, kibaha hakuna shell!
Elimu ni muhimu ili upate pesa. Sema elimu sito lazima uipate darasani katika mfumo rasmi. Unaweza kujifunza kupitia mfumo usio rasmi na ukapata elimu kuliko aliyepita mfumo rasmi
Kwa kweli ES pamoja na mapungufu yake anahitaji sifa aisee...nadhani alisoma kozi moja ya afya ya zamani sana inaitwa 'Rural Medical Aid' (RMA) wakitakiwa kufanya kazi vijijini kutoa huduma za afya. Ila kaishia mjini. Nakumbuka wakati bado nasoma udaktari Muhimbili, alikuwa anakuja na kujichanganya na wanafunzi kuingia wodini. Alikuwa anachagua wale wagonjwa wako hoooi na matatizo ya kutisha tisha..anawahoji kwa kificho na kupiga picha, anapublish kwnye gazeti lake la Uwazi. Hata gazeti lenyewe alikuwa anaandikia pale internet café MTC Muhimbili. Umaarufu ukaanzia hapo and now he is on 'Straight Talk Africa, VOA' interviewed by Prof Shaka Ssali! Hongera zake..penye nia pana njia.
Kajitahidi ukifananisha na kundi kubwa likiokosa elimu. Lakini apunguze habari za umbeya na uongo kwenye media zake. Credibility ya business inajengwa na clean reputation.
Na mimi ndivyo nilikua najua hivyo sasa nashangaa kuona anaupotosha umma. Dah kweli wabongo hawaishwi vituko.