Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mbunge wa Jimbo la Buchosa (CCM) anayemaliza muda wake na mtia nia wa kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa mara nyingine, Eric Shigongo, amesema kipindi chake cha miaka mitano bungeni kimekuwa kigumu na hakujawahi kufurahia nafasi hiyo kutokana na changamoto nyingi alizokutana nazo.
"Nimekuwa Mbunge wenu kwa miaka mitano tangu mwaka 2020 lakini nimekuwa na ubunge mgumu sana, nyinyi wenyewe mnajua nimekuwa na ubunge mgumu, sijawahi hata siku moja kufaidi ubunge, tangu nimekuwa Mbunge ni kila siku nipo jimboni, nimeacha shughuli zangu zote kwamba mimi nikae na wananchi wangu," amesema.
Shigongo ameongeza kuwa, “baadhi ya madiwani wetu hawakuniunga mkono, baraza la madiwani liligawanyika mara mbili, walikuwepo madiwani wanaomheshimu yeye sio mimi, sitawataja kwa majina wala kata lakini hiyo imeathiri sana maendeleo yetu kwa sababu ili maendeleo yaje lazima kuwepo muunganiko wa Rais, Mbunge na madiwani, kaka yangu aliigawa Halmashauri mara mbili nimefanya kazi kwa tabu sana,".