Eric Shigongo, njoo hapa nikufundishe maana ya vita ya kiuchumi

Eric Shigongo, njoo hapa nikufundishe maana ya vita ya kiuchumi

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Bahati nzuri nina kipaji cha ualimu ingawa mimi ni Askari kwa fani.

Vita ya kiuchumi maana yake ni mgongano wa kiuchumi unaotokea baina ya mataifa mawili. Wakati mwingine msuguano huu unaweza kutokea baina ya mataifa mengi lakini yenye pande mbili zilizoungana direct or inderect zenye nguvu sawia kiuchumi au zenye nguvu zinazokaribiana.

Pande hizi huungana ili kuunganisha nguvu kwa lengo la kuangusha upande mmoja.
Lengo la vita hii ni kundi moja au kila kundi kutaka kukaa peak(kileleni).

China and US ukisema zina vita ya kiuchumi sawa. Tanzania na Zimbabwe ukisema zina vita ya kiuchumi huenda ukawa sawa maana tunakaribiana kiuchumi.

Sasa je, ni nchi gani ya kibeberu inafight na Tanzania kukaa peak? Na inapigana vita ya kiuchumi na Tanzania kwa manufaa yapi?
Tukisema labda Kenya ndio wanaopigana nasi na si mabeberu. Je, Tunagombea soko lipi, na hii vita imeanza lini, je, kwanini iibuke kipindi cha Magufuli?.

Mabeberu na Tanzania wanapigania
Soko la dhahabu, mahindi, korosho au?
Kama ulipata Ubunge kwa njia za haramu ni heri utulie ule pesa taratibu na si kuendelea kujipendekeza.

FB_IMG_16157563055370678.jpg
 
Mleta mada hata hicho kipaji cha ualimu huna na hujui chochote kuhusu vita za kiuchumi pamoja na uaskari wako.

Congo na Marekani hazifanani lakini kuna vita za kiuchumi za kufa mtu.

Libya au Iraq hazifanani kiuchumi na Marekani hata robo lakini kuna vita za kiuchumi za kufa mtu zilizosababisha Gadaffi na Saddam Hussen kupinduliwa.

Vita ya kiuchumi yaweza lenga kushika soko la nchi husika au kukamata raslimali za nchi husika mfano waweza taka kuweka kibaraka wao Lisu mbelgiji ili wapore raslimali zetu.
 
Sasa we tuambie tunapigana vita ya kiuchumi na kina nani hasa? Marekani au England au kina nani hasa?
Makampuni ya kimataifa. Vita ya kiuchumi huwa hasa kati ya makampuni ya kimataifa. Mfano ujenzi wa bwawa kubwa la umeme la Mwalimu nyerere tuiingia vita ya kiuchumi sababu mataidfa makubwa hayautaki huo mradi .Hawataki tujitosheleze kwa umeme kwa nini? Tuendelee kununua umeme kwenye mitambi ya makampuni yao ya kimataifa iliyoko nchini!!!

Sababu tukijitosheleza kwa umeme wetu mitambo yao kazi haina na dola haziendi kwao tena!!
 
Porojo tu hizi, hakuna taifa la Ulaya au Marekani linaloweza kuiona Tanzania kama tishio kwa uchumi wake, hiyo stigler tu mitambo yote inatoka kwao, hata nut tu hatuwezi kutengeneza wenyewe, mtoa mada yuko sahihi, tunajiaminisha na vitu ambavyo havina msingi wowote, ivi mkuu unajua bajeti ya afya na Elimu tunafadhiliwa kwa % ngapi? Sisi tukomae tu mdogo mdogo one day tutatoboa lakini siyo chini ya miaka 50
 
Kwako mtoa mada, naona kuna kitu kidogo umeshindwa kutambua japo umeeleza vizuri kabisa kwamba hii vita ya kiuchumi inaweza ikawa direct au indirect.

Kuna wazungu na wachina, ila Tz imeamua kumpa miradi yake mingi Mchina. Na hapo Mmarekani na mchina wana ushindani wao.
Je unafikiri Mmarekani atatusupport sisi tuliochagua kufanya kazi na mchina.

Binafsi naona kuna vita ya kiuchumi dhidi ya Tz na hawo mabeberu, japo ni indirect.
 
Sasa we tuambie tunapigana vita ya kiuchumi na kina nani hasa? Marekani au England au kina nani hasa????
Ahahahahhaha.

Hawa vijana kazi yao ni kukiri na kutetea upumbavu tu.

Ni kama ndugu aliyerogwa kwa limbwata la Kiswahili. Ukimwambia kuwa umerogwa na mkeo anakusikiliza kisha anakwenda kumwambia yote mke wake.
 
Mkuu umeongea kitaalamu, ila wengi watakupinga based on story za vijiwe vya kahawa. Kiuhalisia Mataifa makubwa huichukulia Africa as a soft landing continent kwa kuja kupora rasilimali za kuendesha Mataifa yao Rejea (Berlin Conference 1884/1885).

Kwahiyo inapotokea mtu anakwamisha jitihada zao huonekana kuwa adui dhidi ya Maslahi yao. Kwa Mfano; Marejeo ya Sheria ya Madini dhidi ya Mgawanyo wa faida itokanayo na rasilimali hiyo haikufurahiwa na Makampuni ya Madini ya Kimataifa yanayofanya shughuli zao nchini on behalf of their States. I stand to be corrected
 
Hasara ya mwanamke kutofikishwa kileleni.

Achana na bwana wako goigoi kijana tafuta jibaba likunyooshe maana unaonekana mwenye stress.
 
Back
Top Bottom