Eric Shigongo, njoo hapa nikufundishe maana ya vita ya kiuchumi

Eric Shigongo, njoo hapa nikufundishe maana ya vita ya kiuchumi

sina uhakika kama unayoyasema yana ukweli 100%. kwa sababu hawa jamaa wakitaka kukupiga hata huko kwenye umeme wetu watatupiga tu tena huko ndio hata usiseme. Kumbuka mitambo na vipuli vyote tunategemea toka kwao,
Sio kweli China kabadili game.Vingi vya umeme havitoki kwao tena.Nenda maduka yote ya vifaa vya umeme ukiona kifaa cha mzungu ni bip
 
Babati nzuri nina kipaji cha ualimu ingawa mimi ni Askari kwa fani...
Mkuu ina maana viongozi wale wote wa gov wanaposema tunapigana vita vya kiuchumi kumbe hawajui wanacho kiongea? 😂😂😂 Usitake niwacheke.

Lkn huenda ikawa wana wivu hawa mabeberu maana tmeshusha sgr kaliii, bwawa lile la umeme kila wanapo sikia ule mradi mabeberu wanaona hawaaaa watu hawa.
 
Unasikia wewe jwao walikuwa na mbuga kibao wakaziua zote wakajenga viwanda sisi hatukukuwapinga sasa huku kwetu d
yanawahusu nini? mikataba yote ya kudhibiti hewa ya ukaa wamegoma kusaini viwanda vyao vinafuka moshi kwenda mbele na kuchafuwa hewa ya dunia...
Sasa hilo bwawa la kutengeneza vifaa vya umeme au la kuzalishia umeme?

Kama ni kwa ajili ya kuzalishia umeme huoni kua mitambo ya kuzalishia umeme kwenye hilo bwawa bado tutaendelea kutegemea kutoka kwao?

We unaleta hisia badala ya evaluation ya ki mazingira? Sijui atakua ni beberu wa aina gani masikini kama Tanzania hadi aanze kushindana mradi wa umeme na Tanzania.

Tuje kwenye hoja ya Shigongo kua Kenya kuzuia mahindi ya Tanzania ni vita vya kiuchumi ya mabeberu. Je, mmefanya uchunguzi wa kutosha kujua source ya hili tatizo. Maana naona kama huyo mbunge karopoka tu ili naye aonekane na Mh Raisi
 
Makampuni ya kimataifa. Vita ya kiuchumi huwa hasa kati ya makampuni ya kimataifa. Mfano ujenzi wa bwawa kubwa la umeme la Mwalimu nyerere tuiingia vita ya kiuchumi sababu mataidfa makubwa hayautaki huo mradi .Hawataki tujitosheleze kwa umeme kwa nini? Tuendelee kununua umeme kwenye mitambi ya makampuni yao ya kimataifa iliyoko nchini!!!

Sababu tukijitosheleza kwa umeme wetu mitambo yao kazi haina na dola haziendi kwao tena!!
Niliwahi hisi una akili timamu
 
Wewe unaweza kumfundisha Shigongo au unataka akuajiri kwenye makampuni yake, akutoe kwenye ajira ya keyboard company
 
Yaonekana hata zile hadithi zake alikuwa anacopy sehemu na kuzi interprete. Kwa maneno yake siamini kama ana kipaji hata cha utunzi.
Umenifanya hata mimi nimfikirie mara mbili mbili huyo mtu, sidhani kama kweli alikuwa anazitunga yeye
 
Mataga mna matatizo sana. Anyway ni maoni yako tu. Jiwe yuko wapi mkuu?
 
Umeandika usichokijua. Wale wanatetea ecolojia ambayo ni faida kwetu pia. Mbona kulikuwa na umeme wa gas toka mtwara iliishia wapi. Sema nchi haina mipango inajiendeaendea tu Kama gari bovu na raisi wenu mwehu
 
Kuna faida gani kwa mtanzania zaidi ya kiwafukarisha tu. Bora turudi kulekule angalau ajira zilikuwa zipo nyingi ukilinganisha na sasa ambapo tunadanganya uchumi umekua wakati watu wanazidi kuwa makapuku biashara hamna, wakulima wanalia, wafanyakazi wanalia kila kada inalia
 
Kumuweka kibaraka ni Imperialism sio Economic War!! Marekani anayekupa ARVs na pesa ya bajeti kila mwaka ndio uwe rival wake kivita? Are we serious! Si angeshatumia vikwazo kuzuia mafuta kuletwa huku!!
Tusikuze mambo vita ni labda na Kenya au Rwanda maana ndio tupo level moja
 
Inawezekana kitendo kilichofanywa na Jiwe mwaka jana kilimchukiza M/Mungu zaidi ya yote aliyofanya na anamlipa kadri ya matendo yake...ukweli ni muda sahihi wa kupambania katiba mpya.
Waliopita bila kupingwa uchaguzi ukirudiwa hakuna atakaerudi, hawakutegemea mambo kugeuka hakika ni msiba mzito kwao.
 
Msumbiji kuna sheria kali? DRC kuna sheria kali za madini? Ila mbona mnadai hayana amani sababu ya mabeberu?

Na ndio maana nliuliza unless vita ni ya beberu vs beberu kma kule Libya au Syria lakini sio eti Beberu Vs DRC huo ni uongo afterall makampuni yakibeberu yana mikataba ya kuchimba ya zaidi ya miaka 20 sasa mnapodai mpaka watumie vita kupata madini tueleweje???

Nachojua kwenye hii migogoro ni ile China/Russia Vs Us/EU ndio wanagawanyika hivo. So kma madini ya TZ yapo zaidi mrengo wa Western Bloc basi magaidi wakiletwa ni mrengo wa Eastern Bloc!! Ila sijaona haja ya beberu kutumia silaha kuvuna madini wakati bila ya vita bado tu wanavuna tena kwa mikataba hovyo
 
Sasa mbona bado tunaendelea kupokea misaada yao?
Tunatumia magari yao?
Simu,compyuta,internet,mitambo nk tunatumia vilivyotengenezwa na wao?
Elimu pia ni ya kwao?
Mfumo wa siasa nk vyote wao ndo wameunda?
Viwanda ,barabara,madawa vyote wanatengeneza wao?

Yaani kila kitu ni chao..sasa unasemaje wanatuonea wivu Leo wakisena sasa hatufanyi biashara yoyote na Tanzania tuna nini hasa cha maana cha kujivunia?
 
Mleta mada hata hicho kipaji cha ualimu huna na hujui chochote kuhusu vita za kiuchumi pamoja na uaskari wako.

Congo na Marekani hazifanani lakini kuna vita za kiuchumi za kuga mtu.

Libya au Iraq hazifanani kiuchumi na marekani hata robo lakini kuna vita za kiuchumi za kufa mtu zilizosababisha Gadaffi na Saddam Hussen kupinduliwa.

Vita ya kiuchumi yaweza lenga kushika soko la nchi hudika au kukamata raslimali za nchi husika mfano waweza taka kuweka kibaraka wao Lisu mbelgiji ili wapore raslimali zetu.

Umemaliza yote maana yeye kaandika tuu bila kufikiri!
 
Kwako mtoa mada, naona kuna kitu kidogo umeshindwa kutambua japo umeeleza vizuri kabisa kwamba hii vita ya kiuchumi inaweza ikawa direct au indirect.

Kuna wazungu na wachina, ila Tz imeamua kumpa miradi yake mingi Mchina. Na hapo Mmarekani na mchina wana ushindani wao.
Je unafikiri Mmarekani atatusupport sisi tuliochagua kufanya kazi na mchina.

Binafsi naona kuna vita ya kiuchumi dhidi ya Tz na hawo mabeberu, japo ni indirect.
Ww ndio umeelezea vzuri ila umekosea hapo mwishoni.

Vita ni US na China so Tanzania ina kua kwenye proxy war lakini US haiwezi pigana vita na TZ hyo kitu haipo sababu ingemalizwa cku moja tu. Hvi zile hujuma za US kwa N.Korea na Russia na vikwazo likuki Tz tungehimili?
 
Tanzania hakuna Vita ya kiuchumi mnadanganyana tuu vita itoke wapi wakati kuna mbuga tumegawa miaka ya kutosha huko ni ya waarabu hiyo Loliondo gate sijui inaendeleaje nikiikumbuka nambuka mwandishi nguli Katebaro...mpaka kesho madini wanunuzi ni wao wapangaji bei ni wao wanachukua kwa bei wanayotaka baada ya kupanga huko kwenye soko lao hapo kutakua na vita ya nani na nani Sasa....hapo kuna vita ya Watanzania kupewa kesi za uhujumu uchumi lakini sio Vita ya kiuchumi na mataifa makubwa mkenya tuu katufungia tusipeleke mahindi masikini mwenzetu ndio mzungunzie mabeberu ambayo hata condom zinatoka kwao za msaada na dawa za Arv.
 
Kuna tofauti kati ya EXPLOITATION AND ECONOMIC WAR.
Huyo mjeshi ameandika point sana.

Ku avoid exploitation siyo kupigana vita ya kiuchumi.
Ni kujitambua na pengine kujitawala.

Eventually there must be a fair play.
 
Back
Top Bottom