Eric Ten Hag kumuacha De gea hawezi kufanikiwa Manchester United

uwe hodari

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2022
Posts
4,045
Reaction score
8,608
Hii timu tumevumilia kwenye nyakati zote ngumu de gea akitubeba timu ikiwa mbovu kupindukia na makocha wabovu kupindukia ila degea amekuwa kwenye ubora wake kwa muda wote huo ametubeba

Nilimuunga hatua ETH kwa kila hatua kwenye maamuzi yake ya kujenga timu ikiwemo kuwaondosha wachezaji waliochoka kina Ronaldo pamoja na wachezaji wabovu kina martial na kina sancho na wengine

Lakini hili la kumuondoa degea litakuja na mikosi kwake
Imeniumiza sana hii degea reserved more respect than this angemuongezea mkataba wa miaka miwili hata asipdaka mechi zote

Hili la kusingia kuwa de gea ni traditional goal keeper sioni kama linauzito kwa sababu degea ni bora kwenye kila kipengele na sidhani km footwork kwake inakuwa shida kudeliver

Ten hag nilikupa odds nyingi kuinyanyua manchester united ila kwa hili utafeli kwa kweli

Watu wengi sana duniani wameumizwa na hiki alichofanyiwa degea

Poor Eric prepare to be fired
 
Ngoja aje ajitetee hapa
 
Reactions: BRB
Kumbe ETH huwa anapitia jf basi ongeza juhudi za kupaza sauti anaweza akajirudi
 
Degea AMEISHA CHEZA sana.

Inahitajika timu mpya, Ujenzi WA timu mpya ama maendeleo yanaendana na maumivu nk.

Hakuna JINSI Lazima Mti upukutishe majani.
 
Kitabu kimejifunga na tulimpenda sana kwakeli
 
Yaani mtu unaumia kabisakabisa yanayotokea timu ya Uingereza wewe upo Mivumoni hata hauumizwi na timu yako ya KMC. Acheni tu tuwe watumwa
 
Yaani mtu unaumia kabisakabisa yanayotokea timu ya Uingereza wewe upo Mivumoni hata hauumizwi na timu yako ya KMC. Acheni tu tuwe watumwa
Kwanini wewe hujaja kuandika hapa uzi hata mmoja wa Team yako ya NYAMTENDE kama kweli unaipenda?
 
Kama ni shabiki kweli wa UNITED kama Mimi huwez kupinga De gea kuondoka, Ila tuseme the way anavyoachwa haikua sahihi ila kama kuondoka ni sawa coz De Gea ni Man of Saves hilo halina ubishi haza zile za kutumia miguu jamaa anajua sana ila kocha ukimuangalia yeye anaamini kabisa akipata kiungo mzuri na beki nzuri hahitaji golikipa mzuri ku save tu wakat hawez kuchezesha Team kuanzia Nyuma.

Nenda kaangalie na utajua why Pep alipata wakati mgumu Kupress zidi ya Inter kwenye final ya UEFA coz ONANA laikua ana kaa mstari ule wa Beki namba 5 halaf beki nammba 5 na 4 wanakua kama Left na Right back then wale Ma Left na Right back wanasogea Mbele wanaongeza namba ya washumbuliaji

Even ETH anamtaka Golikipa wa Namna hio na De Gea atatakiwa ampishe.
 
Uchezaji wa Onana ni wa kimuhemko akikutana na watu wanaojua kuchungulia mtamkataa asubhi na mapema, simlaumu Rigobert Song kumuacha national team kipa Gani anakupa pressure Kila muda.
 
De gea mwenyewe ndo alikosea kukataa ofa za Madrid mwenzie Mbappe alitaka kujipoteza ila kashtuka mapema
 
Usihukumu kabla ya kujua mrithi wake, na pia menejiment yake huenda ilitaka dau kubwa, na kama meneja eric anaona ataweza kupata kipa mwingne bora wa kiwango chake au zaidi.
 
Uchezaji wa Onana ni wa kimuhemko akikutana na watu wanaojua kuchungulia mtamkataa asubhi na mapema, simlaumu Rigobert Song kumuacha national team kipa Gani anakupa pressure Kila muda.
Rigobert Song alimuacha Onana kwa siasa zao Cameroon wanaendeshwa kipuuzi.

Hajawahi kuchomesha kwa huo uchezaji wake why aachwe kama sio watu hawajui modern football.

Onana alizinguana na kocha kibaraka wa Eto'o ambaye anataka kikosi aweke yeye,Cameroon wapuuzi tu na Mbappe kama Mungu alimuona kutopewa nafasi kwa hiyo timu
 
Nikikumbuka aliyopitia huyu Sergio Romero sioni haja ya kuleta huruma kwa De Gea,kocha aachwe afanye kazi yake

Kila mtu ana wakati wake apishe wengine
 
Uchezaji wa Onana ni wa kimuhemko akikutana na watu wanaojua kuchungulia mtamkataa asubhi na mapema, simlaumu Rigobert Song kumuacha national team kipa Gani anakupa pressure Kila muda.
Inter imefika fainal na huyo huyo kipa.

Ubora wake tangu Yuko ajax au umeanza kuangalia mechi Jana.

Hiyo fainal ya Uefa kaangalie mshambuliaji hatari kabisa Halland alivyokuwa anasumbuliwa na ile Pressing
 
Haland si mviziaji bila kulishwa mipira hakuna kitu mule, huyo Onana alishukuru Mungu KDB alivyoumia
 
Umenielewa tofauti

Mimi toka miaka mingi nafuatilia Barclays PL
Na soka la ulaya
. sikumbuki ni lini nilipoteza muda kufuatilia ligi ya Tanzania labda itokee bahati mbaya tupo out weekend na mpira inachezewa but sijui kitu kuhusu mpira wa tanzania
Yaani mtu unaumia kabisakabisa yanayotokea timu ya Uingereza wewe upo Mivumoni hata hauumizwi na timu yako ya KMC. Acheni tu tuwe watumwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…