Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Picha: Erick Kabendera
Mtanzania aliyekimbia Nchi yake kutokana na kuzorota kwa usalama wake ,kulikochangiwa na watawala, Ndugu Erick Kabendera, ametoa maoni yake kwenye Tume ya haki jinai na kufumua mazito sana .
Kabendera amefichua mbele ya Tume hiyo kwamba , kumbe siku zote Mahakimu huwaogopa waendesha mashitaka kiasi cha kudhulumu haki za Watuhumiwa , yaani hata kama mtuhumiwa ni dhahiri anaonewa hata akiwa Mahakamani, Mh Hakimu hawezi kumsaidia kwa vile anawaogopa waendesha mashitaka , bali hakusema sababu hasa za Mahakimu kuwatetemekea waendesha mashitaka hao .
Pamoja na hilo Kabendera anasema kwa miezi 7 aliyolundikwa gerezani hakuona mahali popote ambapo panaelekeza mtuhumiwa kutoa maoni yake kuhusu utendaji wa Jeshi la Polisi .
Amependekeza kiundwe chombo Maalum cha kupokea malalamiko ya wananchi juu ya utendaji wa Jeshi la Polisi , kumbukeni kwamba hakuna mahali popote ambapo unaweza kupeleka malalamiko ya Utendaji wa Jeshi la polisi bila koneksheni ya viongozi wa CCM.
Mwisho Kabendera ameahidi kurejea Tanzania pale atakapohakikisha kweli kwamba Usalama wake utalindwa .
Chanzo: Azam Media
PIA, SOMA:
- Mwanahabari Erick Kabendera akamatwa na Polisi nyumbani kwake; yadaiwa anaendelea na Mahojiano