Erick Kabendera kupitia Kitabu chake: Ben Saanane aliuawa na Rais Magufuli na maiti yake ikatupwa Mto Rufiji

Picha ya mwangosi akipigwa bomu ziliwekwa mitandaoni na magazetini uliziona?
daah ile picha sio kabisa ilimuonesha ffu ameshika kichwa kapigwa butwaa haamini kama anachoshuhudia ni utumbo wa binadam mtu mzima umetapakaa chini yan sio poa kabisa
 
Kwamba jiwe mwenyewe ndio alimshoot Mwamba.
Damu ya mtu haiendi bure
 
Hizo za chinichini zimeanzia humu JF, nazo hazina ushahidi kama haya madai ya Kabendera.
Mpaka sasa hatuna evidence kipi kilitokea ila tutakuja kujua tu ukweli haufichiki.
 
Kabendera alikuwa anafanya kazi gani katika taasisi ipi ya serikali ya Tanzania?
Waliokuwa wanampa taarifa alizokuwa anaziuza ni wakina nani?
Kwa nini bado yuko uraiani kama haya madai ni ya kweli?
Unaposema "wenzake" akina Snowden unamaanisha Kabendera alikuwa jasusi wa serikali?
Pia hakuna ushahidi wa Marekani kuua watu wanaodaiwa kuvujisha siri za serikali ya Marekani kwa maadui zake. Huwa wanakamatwa, kufunguliwa mashitaka na kufungwa na wapo wengi mfano Robert Philip Hanssen, Jack Teixeira, Reality Winner n.k
 
wew inaelekea unajua kitu.
umenyorosha maelezo hadi raha.
safi sana.
sasa na huyu Ben mlimpeleka wapi? maana naona mnampinga mkuu kabendera?
mnatuchanganya.
 
Hiki kitabu usishangaae kikipigwa marufuku na serikali!
Na huu uzi nashangaa bado haujafutwa mpaka dakika hii!
 
Watachafuka sana , chama na serikali kwa ujumla wake
 
Kabendera ni mwandishi wa habari, akawa anaandika taarifa za kiuchunguzi na kutafuta majarida ya nje aziuze, sio asaidie. Mtofautishe na yule mwandishi aliyefariki awamu ya Mwinyi aliyeandika kuhusu Loliondo kuuzwa, huyo alitaka kusaidia nchi.

Waandishi kama Kabendera kuna wanaotuma taarifa nje, kuna wanaopewa agenda kutoka nje waziandike kwa wasomaji wa ndani na wa nje. Mfano andika agenda ya ubaya wa bwawa la umeme linalojengwa, andika ubaya wa bomba la mafuta kutoka Uganda kwamba linachafua mazingira (hii kandarasi walikuwa nayo Wakenya).

Snowden hakuwa spy, alikuwa contractor wa NSA na CIA kutokana na utaalamu wake. Akavujisha siri, akaiba data za serikali akashtakiwa, ila huwezi msikia analialia kumlalamikia Obama sababu alijua anachofanya. Kabendera yeye alijua kupokea miamala tu, kuhusu akigundulika hakutaka kujisumbua.
 
daah watu mna vichwa vigumu wkt mlichoonyeshwa apo ni paragraph moja tu ya kitabu kikubwa.

wew kanunue icho kitabu usome humo ndani uone uo ushuhuda ulivyojengwa ndo uanze hayo mabishano au vinginevo ulete ushahidi wako.
Wewe ushuhuda unao? Huna.

Kabendera kaandika tuhuma kwa mtu mfu, ambaye hawezi kujitetea. Ushahidi wake ni "both opposition and government sources I have spoken to"
 
wew inaelekea unajua kitu.
umenyorosha maelezo hadi raha.
safi sana.
sasa na huyu Ben mlimpeleka wapi? maana naona mnampinga mkuu kabendera?
mnatuchanganya.
Kabendera anadai viongozi wa upinzani na serikali alioongea nao wanajua. Ni kina nani hao?
Mwambie awataje hao kisha ndio waseme Ben yuko wapi. Simple as that. Siku nyingine mwandishi mwingine aje aseme "kaambiwa" Ben aliuwawa na Mbowe, tukubali kisa kaambiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…