Nasema nina uhakika kwa sababu hana ushahidi mwingine wa kuaminisha watu kuhusu allegation aliyoitoa kwa Magu...
Mtu mwenye akili isiyo fikiri kimantiki ni rahisi kuamini ni kweli Magufuli alimuua Ben kwa kuangalia picha ya cover tu...
Mtu kukosa ushahidi wa kuthibitisha kitu kimetokea hakukupi wewe uhakika wowote zaidi ya uhakika kuwa huyo mtu hana ushahidi.
Kutokuwepo kwa ushahidi wa kitu kuwepo si ushahidi wa kitu hicho kutokuwepo.
Rudia kusoma uelewe vizuri.
Kutokuwepo kwa ushahidi wa kitu kuwepo si ushahidi wa kitu hicho kutokuwepo.
Usichanganye mawili haya.
Mfano, Kabendera akisema Magufuki kamuua Saanane kwa mkono wake, akakosa ushahidi kuthibitisha hilo, wewe huna uhakika wowote zaidi ya kuwa huyu mtu hajatoa ushahidi.
1. Huna uhakika Magufuli kaua.
2. Huna uhakika Magufuli hajaua.
3. Huna uhakika Kabendera anadanganya, inawezekana kaghafilika tu.
4. Huna hata uhakika kuwa Kabendera hana ushahidi, inawezekana anao hajautoa tu. Kabendera kutotoa ushahidi haimaanishi hananushahidi, inawezekana ana ushahidi lakini anazuiwa na maadiki ya uandishi kutoa ushahidi. Waandishi wana miiko ya kulinda vyanzo vyao.
Inaonekana unalichukukia neno "uhakika" kirahisi sana na hulielewi.