Open school
JF-Expert Member
- Jul 13, 2015
- 1,158
- 1,746
Serikali inatumia nusu trillion kwa mwaka kununua mashangingi tu. Kodi inatumika kuwaneemesha wachache serikalini.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
HAkuna mtu alitoa taarifa , ndo nikapata mshangaowanazima
kaza mkanda waambie na wananchi jimboni waongeze juhudi shambani msimu huu muhimu sana wa kilimo 🐒"Watanzania hawana pesa mfukoni, Watanzania hawana pesa ya kununua, watu hawawezi kuendesha maisha, wachumi watakuwa wananielewa (mimi sio mchumi) nimesoma mahali hali ya mtu kuwa na mahitaji lakini hana pesa na naliongelea kwa sababu ni Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ambayo inaratibu biashara katika Taifa letu, Mheshimiwa Mwenyekiti nikupe kwanza taswira ya hali yetu ya sasa kama Taifa, pato la Taifa linaongezeka, pato la kila mwananchi mmoja mmoja (per capital income) inaongezeka, balance of trade kati ya Tanzania na Kenya, Tanzania inauza zaidi Kenya kuliko Kenya wanavyouza Tanzania, shilingi ya Tanzania inaimarika kuliko shilingi Kenya, ni kweli zamani tulikuwa tunabadilisha shilingi ya Kenya kwa shilingi elfu 21 leo hii ni shilingi 15, ina maana shilingi yetu inaimarika licha ya uwepo wa UVIKO-19, vita vya Ukraine nk" -Shigongo
"Mheshimiwa Mwenyekiti hilo lipo kwenye vitabu, nikiwaeleza wananchi wa Buchosa kwamba per capital income imeongezeka, nikiwaeleza wananchi wa Buchosa kwamba GDP imeongezeka wananiambia GDP ndio nini wakat hawana kitu mfukoni, sina pesa mfukoni GDP ni kitu gani, tumeshindwa kushusha uchumi kutoka juu kwenda kwenye meza ya mwananchi wa kawaida, Mheshimiwa Mwenyekiti kwa nini tuko hapa?, tuko hapa kwa sababu ya vita nilizozitaja, tuko hapa kwa sababu ambazo awamu ya Tano (5) iliyafanya, awamu ya tano ilikuwa awamu ya kuthubutu, iliingia kwenye miradi mikubwa mikubwa ambayo si jambo baya, lakini hii maana yake ni kwamba mapato yakazidiwa na matumizi, certificate ya Bwawa ikiiva lazima Mwigulu achanganyikiwe" -Shigongo
"Mheshimiwa Mwenyekiti ndio hali tuliyonayo nyie wote niashahidi watu wanalalamika maisha ni magumu hawana pesa ya kununua, watu wanasitisha maisha yao kwaa sababu maisha ni magumu sana huko mtaani lakini, lakini bado magonjwa ya akili yanaongezeka, maisha yamekuwa magumu" -Shigongo
"Sekta za uchumi za nchi hii lazima zichangie pato la Taifa, hazichangii Mheshimiwa Mwenyekiti, agriculture (27%), tourisma imepanda kidogo, mining (10%), fishing (1.8%) Taifa letu ni tajiri mno sekta hazichangii, tunataka sekta za uchumi za nchi hii zichangie pato la Taifa ili mwisho wa siku kapu likijaa tupunguze hata kodi zetu, hakuna ubaya kapu likijaa tukasema VAT iwe 4% kwani shida nini, nikisema hivyo Wafanyabiashara wataenda kulipa kodi, faida zinaongezeka, Mheshimiwa Mwenyekiti watu hawalipi kodi, tax base yetu haifiki milioni sita (6) kwenye Taifa hili"
-BuschosaMbunge wa jimbo la Buchosa Erick Shigongo amezungumza hayo akiwa Bungeni, jijini Dodoma Februari 12.2024
Siku ya mwisho kila goti litapigwaKuelekea Uchaguzi mkuu wa 2025
Unataka Watawala wakugawie pesa? Sema unataka wafanyaje?Miaka Sitini 60 Sixty ya Umasikini kila siku afadhali jana huku Watawala wakiendekeza HADAA👈 na POROJO👈 Ni wakati sasa tuangalie upande wa Upinzani CHADEMA✌️👈
Kwa hiyo kule ambako Kuna feni maisha ni mepesi?ni saa tatu na nusu, nalala bila feni leo mwanao
nalowesha shuka na maji
Watekeleze majukumu yao inavyotakiwa, hali ya maisha ya mwananchi wa chini itabadilika.Unataka Watawala wakugawie pesa? Sema unataka wafanyaje?
Kama majukumu yapi hayo ambayo hawajatekeleza yanapelekea maisha Yako kuwa magumu?Watekeleze majukumu yao inavyotakiwa, hali ya maisha ya mwananchi wa chini itabadilika.
Vipi unajua majukumu ya serikali?Kama unajua vizuri, basi hauwezi kumuuliza jamaa hilo swali.
Nina Kisaloni hakuna Umeme nikafunga nikanunua Bodaboda Mafuta bei juu.Unataka Watawala wakugawie pesa? Sema unataka wafanyaje?
Kama bei Juu Kwa nini wewe usioandishe bei kulingana na gharama za uendeshaji?Nina Kisaloni hakuna Umeme nikafunga nikanunua Bodaboda Mafuta bei juu.
Bei za Vyakula hazishikiki nina Familia na Watoto nasomesha nk.
Au wewe ni mnufaika wa hii System?
CHADEMA imetuahidi Watanzania kuwa itabadilisha mambo.
Hali ni ngumu msishangae kukatokea Revolt sasa hivi huku Temeke Wananchi wanashindia mlo mmoja tena wa kwato za kuku.Kama bei Juu Kwa nini wewe usioandishe bei kulingana na gharama za uendeshaji?
Ndio Mimi ni mnufaika maana nalima na wastani wa gunia la mahindi mfano ni 50,000 ,ulitaka liuzwe 30,000 Ili wewe wa mjini unufaike Mimi nife?
Sijui ni kwanini ila mimi naona hakutakuwa na mabadiliko yoyote, wote walewale. Chupi mpya tako la zamani. Viongozi wa Afrika hawatofautiani sio upinzani sio chama tawala ni vile tu hawajapata nafasi!!Labda CHADEMA kitatutoa kwenye hali hii ya DHIKI huku Viongozi wa Serikali ya CCM wakipora Nchi bila HURUMA[emoji118]
Mimi NAAMINI 👈 CHADEMA watatupatia KATIBA MPYA na TUME HURU na Watatubadilishia huu mfumo kulambano Matako (ashakum si matusi) na kupata TEUZI nina imani Watatujengea Taasisi Imara nk.Sijui ni kwanini ila mimi naona hakutakuwa na mabadiliko yoyote, wote walewale. Chupi mpya tako la zamani. Viongozi wa Afrika hawatofautiani sio upinzani sio chama tawala ni vile tu hawajapata nafasi!!
Wanafanya nini huko Temeke, warudi kijijini wakalime wapate chakula wale, ardhi ya kilimo bado ni kubwaHali ni ngumu msishangae kukatokea Revolt sasa hivi huku Temeke Wananchi wanashindia mlo mmoja tena wa kwato za kuku.
Kwato za Kuku
👆👆👆👆👆👆🤔
Ni RAHISI SANA👈 👉KUSEMA.Wanafanya nini huko Temeke, warudi kijijini wakalime wapate chakula wale, ardhi ya kilimo bado ni kubwa
Kilio changu ni sukari. Supu nazo zimepanda bei. Tunaomba gvt waliangalie sana hili swala.
[/QUOTE
Hamia kunywa supu kwa mama Hussein pale Pasua sokoni-Moshi mjini, supu aina ya mawashi washi aka nyama ghasia kwa buku, chapati mbili ni jero tu.Maji bure bila kusahau limao na ndimu.Hatufi ng'o, ttawasindikiza wao, mwendo wa kipimo jero hadi buku unatoka jasho , mishipa yote mwilini inasimama.