Ernesto Valverde kocha mpya Barcelona, amrithi Luis Enrique

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Anachukua mikoba ya Luis Enrique alikua kocha wa Atl Bilbao.

Karibu Catalunya Ernesto Valverde.
=====


Kocha Ernesto Valverde ametangazwa rasmi na uongozi wa Barcelona kuwa ndiye mrithi wa Luis Enrique.

Kocha huyo mpya kutoka klabu ya Athletic Bilbao, alisema kwamba kukabidhiwa mikoba kuinoa Barcelona ni jambo kubwa na gumu hata hivyo amejipanga vyema kwa ajili ya kukisuka kikosi hicho ili kuongeza makali msimu ujao.

Alisema kwa kuanza atahakikisha wanafanya usajili ambao utasaidia timu hiyo kufanya vyema kwenye La Liga msimu ujao na mashindano ya Ulaya.

Rais wa Barcelona Josep Bartomeu alisema, “Nimeongea na Varverde na kumweleza uamuzi wetu, naye ameupokea kwa moyo mkunjufu.”

“Alisema amefurahia uamuzi huo na yupo tayari kukabiliana na changamoto zote zinazohusiana na kuwa kocha mkuu wa klabu kubwa kama Barcelona.

‘Tuna muda mwingi wa kuzungumza naye, tumejirdhisha kutoka na uwezo wake mkubwa pamoja na elimu yake pia ana uzoefu wa kutosha.”

Kocha huyo amekuwa akipenda zaidi soka la vijana ikiwa ni pamoja na kuwa na mtindo wake wa kipekee ambao hata hivyo unaelekeana na mambo mengi yanayofanyika Barcelona.

Ververde alihamia Athletic Bilbao na kuwa kocha timu ya vijana mwaka 2002, kabla ya kupandishwa kuwa kocha mkuu msimu uliofuata.

Pia amewahi kuzifundisha Espanyol, Olympiacos, Villarreal na Valencia kabla ya kurudi tena Athletic mwaka 2013.

Kocha huyo mwenye miaka 53 alitangaza uamuzi wake wa kujiunga na Barcelona baada ya kuitumikia timu yake ya zamani kwa miaka minne.


Luis Enrique akinyanyua kombe la Copa Del Rey enzi zake akiwa Barcelona ambayo anaachana nayo rasmi.​
 
bola karibu bwana rire rijjammaa llilikua mamruki
 
Jamaa chaguo lake la Kwanza Herrera sijui atamtoa OT??
 
Anatokea wapi huyu??
*Ernesto Valvarde ateuliwa kuwa kocha mpya Barca, ni nani huyu?*


Ernesto ni mzaliwa wa nchini Hispania ambako alizaliwa miaka 53 iliyopita nchini Hispania na amewahi kuichezea timu yake ya taifa huku pia akipita katika vilabu mbalimbali nchini Hispania.

Ernesto Valverde amevichezea vilabu vya Alaves, Sestao, Espanyol,Atletic Bilbao lakini pia alikuwepo katika kikosi cha Barcelona kilichoshinda kombe la Cup Winners Cup na Copa Del Rey chini ya Johan Cruyf.

Mwaka 1997 ndipo Valverde aliamua kuacha kucheza soka na kuanza kujihusisha na masula ya soka ambapo alifundisha timu kama vile Espanyol,Olympiakos,Villareal,Valencia na hatimaye Bilbao.

Uwezo wa Ernesto Valrade ulionekana mkubwa sana haswa walipochukua kombe la Super Cup mwaka 2014 baada ya kuifunga Barcelona mabao 4 kwa nunge hapo ndipo alianza kufahamika sana.

Lakini pia Valvarde sio mgeni sana wa makombe kwani alipokuwa akiinoa Olympiakos alifanikiwa kubeba makombe matano ya michuano mbali mbali nchini Ugiriki.

Valvarde anakwenda kuchukua kazi ya Luis Enrique aliyeamua kustaafu, lakini atakuwa na kibarua kigumu kuirudishia Barca ubingwa wa La Liga na Champions league ambayo yote msimu huu wameikosa.
 
Barca wanahitaji miaka 5 mengine ya transformation kutoka kizazi cha kina Inesta,Xazi,Pique na kuleta damu mpya ASA za LA masia nadhani bodi imeliona ilo maana jamaa ni muumink wa soka LA vijana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…