Errol Spence vs Mikey Garcia moto kuwaka.

Errol Spence vs Mikey Garcia moto kuwaka.

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Ule mpambano wa kukata na shoka kati ya Mikey Garcia na Errol Spence hatimaye umewadia.


Errol Spence anatetea mkanda wake wa IBF dhidi ya Mikey Garcia.

Mikey Garcia amepanda uzito mara mbili ili kumchallange Errol Spence , vilevile Garcia ni bingwa wa dunia mara nne katika uzito tofauti tofauti wakati Spence yeye anapigana katika uzito wa Welterweight pekee.

Garcia imepigana jumla ya mapambano 39, 30 ameshinda kwa K.O na hakuwahi kupigwa wala kutoa sare (39-0-0) ,kwa upande wa umri ana miaka 31, urefu wa mita 1.6 na uzito wa Kg 61 , ni Orthodox

Spence amepigana jumla ya mapambano 24, 21 ameshinda kwa K.O 3 ,hakuwahi kupigwa wala kutoa sare (24-0-0) , ana umri wa miaka 29, urefu wa mita 1.7, uzito wa Kg 67 yeye ni southpaw.


Sasa je nani atapoteza title ya undefeated????


Majibu yote tutayapata usiku wa leo.



teammikeygarcia-20190316-0001.jpeg
 
Errol spencer moja wa mabondio bora kabisa kwa sasa. Namkubali sana pamoja na mshaji wake Devrota hawa ndio mbadala wa Money Mywether.
Sijajua huu mpambano utapigwa mida ya saa ngapi. Mkuu kama utakuwa na uwezo tuwekee na link.

Shukrani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Errol spencer moja wa mabondio bora kabisa kwa sasa. Namkubali sana pamoja na mshaji wake Devrota hawa ndio mbadala wa Money Mywether.
Sijajua huu mpambano utapigwa mida ya saa ngapi. Mkuu kama utakuwa na uwezo tuwekee na link.

Shukrani

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio Devrota ni Gervonta .

Gervonta Davis Tank
 
Garcia ame-catch up na hajafanya kazi nzuri. Amenenepa kwa kuongeza mafuta na maji, pumzi zitakata.
Spence atavuta muda na kumdhalilisha baadae.
Pili, style ya spence ipo superior.
Mbona Floyd Mayweather ni Orthodox lakini ndiye bondia bora zaidi kuliko hata hao southpaws.
 
Mbona Floyd Mayweather ni Orthodox lakini ndiye bondia bora zaidi kuliko hata hao southpaws.
Floyd ana defence mechanism nzuri sana na pia ana nidhamu ya hali ya juu. Floyd is a genius, ni mwepesi na hujenga misuli ya mabega anayoitumia kutelezesha ngumi kutoka upande wowote.
Pili, Floyd anaeza kuinama haraka, kurudisha torso nyuma wakati miguu ipo firm, na kukuzunguka kimduara na kukuchanganya.
Garcia hayupo hivyo, huwa anaenda straight kama De La Hoya kwa sababu baba yake ndivyo alivyomfundisha.
Sababu siyo south au orthodox, bali ni style ya kupigana.
 
Back
Top Bottom