Wanabodi,
Mtanisamehe sana kwa kuanza huu mjadala kwa maneno makali, kuwa sisi Watanzania tulio wengi ni "ignorants!", vichwa maji kabisa!, vichwani ni weupe!, uwezo wa kufikiri, "logical thinking", ni sifuri, ndio maana hatuna uwezo wa kufanya maamuzi ya maana, "informed decisions", hali inayopelekea, tunapelekwa pelekwa tuu kama mazuzu!, kiasi kwamba, wengi wetu tunashabikia zaidi na kushupalia vitu vidogo vidogo ambavyo ni non issues, na immaterial, ambazo sio chanzo bali ni matokeo tuu, badala ya kudeal na issue zenyewe ambazo ndicho chanzo, kilizopelekea haya yatokanayo, havishungulikiwi, havizungumzwi!, haviguswi!.
Hii ignorance ya Watanzania ina cut across society yetu na ku reflect ndani ya kila sekta ya jamii yetu kuanzia ndani ya familia zetu, mitaa yetu, vitongoji vyetu, vyama vyetu, hadi ndani ya bunge letu, tuna wabunge ma ignorants mule!, tuna viongozi wetu ma ignorants hadi ndani ya cabinet yetu!, tuna viongozi wa taasisi za umma ma ignorants hadi t, tuna viongozi wetu wa vyombo vya dola ni ma ignotants, na wana jf wengi pia ni ignorants tuu, nikiwemo mimi mwana JF, Pasco wa jf, tofauti na wengi maignorants wenzetu, wanajikalia kimya, hivyo kuificha hiyo ignorance yao, lakini sisi wengine ambao kwa bahati mbaya sana, hatukujaliwa aibu, tunaionyesha hiyo ignorance yetu kwa ku speak out and expressing our minds, tatizo, ni, in so doing, tunajikuta tumewaambukiza ignorance, hata wengine ambao hawakuwa ignorants!. Sorry for this.
Ni kufuatia ignorance hii, Chama cha Mapinduzi, (CCM), kinaitumia ignorance hii ipasavyo kwa kuifanya ndio mtaji wake wa kupatia kura za ushindi, mwaka hadi mwaka, na mwakani tutaichagua tena CCM kwa kuipa ushindi wa kishindo!.
Hisia za kujiuliza, kama sisi ni ma ignorants au tumelogwa, ni kufuatia kuwa na mtazamo, ya kuwa haiwezekani, watu wenye akili zao timamu, wakafanyiwa mambo ya ajabu ajabu kama haya, lakini bado tunaichagua CCM tena na tena!.
Wakati tulipopata uhuru toka kwa mkoloni, tulikuwa na maadui wakuu watatu, ujinga, umasikini na maradhi, lakini hadi leo miaka zaidi ya 50 baada ya uhuru, sio tuu, wale maadui wakuu watatu bado wapo, bali ujinga umeongezeka mara dufu, umasikini sasa ni uliotopea, na maradhi hadi mengine ni janga, vimeongezeka afadhali ya zamani na enzi za mkoloni, bali pia, tumeongeza idadi ya maadui wakuu, wakiwemo rushwa na ufisadi, ambapo mazao yake ni pamoja na DCP, Deep Green, Meremeta, TanGold, Alex Stewart, EPA, Richimond, na sasa Escrow.
Kitu kizuri cha ajabu kuhusu sisi Watanzania ni kujifanya kupiga kelele sana as if tunauchukia umasikini, ujinga, maradhi, rushwa na ufisadi, lakini sisi wale wale, mwaka hadi mwaka, tunawachagua watu wale wale, chama kile kile, sera zile zile, tukitegemea matokeo tofauti!, hii ni nini kama sio ignorance at the highest levels?!. Keshokutwa tunawapa serikali za mitaa!, mwezi April tuna wapitishia ile "Bora Katiba" kwa kura za ndio za kutosha, na zisipotosha "zitatosheshwa!",na October, 2015, tunamalizia kazi, kwa kuirudisha CCM kwa ushindi wa kishindo!.
Ignorance hii imejidhihiri wazi kwenye huu mjadala wa Escrow unao endelea sasa, ambapo wengi wetu, tumejikita kwenye issue ya fedha za Escrow tuu, ambayo sio a very big deal!, fedha ya escrow ni matokeo tuu ya hili jinamizi linaloitwa IPTL!, na hiyo pesa iliyokuwa inawekwa kwenye account ya escrow ni capacity charges only, bado Tanesco inalipa mabilioni kwa mabilioni ya kulipia Utilities huko huko IPTL, Aggreko, Simbion, Songas!, badala ya watu kujadili chanzo, na kwa nini tumefika hapa, wao wanajadili matokeo tuu!. Hii kama sio ignorance ni nini?!.
Katika kuwabaini wahusika, watu wanafanya "cherry picking ya kumchagua huyu na yule, na kumuepusha yule na yule ili mradi tuu apatikane "mbuzi wa kafara!", na miongoni mwa wahusika, sijaisikia BOT ikitajwa tajwa, simply kwa sababu yeye ni dalali tuu!. Kama escrow ni account ya ubia kati ya serikali na IPTL, BOT ililipaje zile pesa PAP?!.
Escrow sio issue sana kivile!, escrow ni matokeo tuu, issue yenyewe haswa ni IPTL, ilikujaje, ilipitaje, ilikubalikaje kutuwekea mitambo ya mtumba, obsolete technology, ilikubalikaje kukubali kutozwa capacity charges zile?!, hii kama sio ignorance ni nini?!.
Watu wanataja taja tuu majina!, wananyooshea watu vidole!, wanawapigia kelele waliolipwa na JR tuu, waliolipwa na PAP wao wako wapi?, Walioileta IPTL wako wapi?, hii ni nini kama sio ignorance?!, au tumelogwa?!. Tunapaswa kuwatafuta responsible people tangu hili jinamizi la IPTL limekuja nchini, tuwawajibishe!, na sio kutafuta mbuzi wa kafara, au kama kawaida yetu, tufunike kombe mwanaharamu apite!".
Pasco