Wanabodi,
Preamble
Mtu mwenye akili na mwenye busara, anapojikwaa na kuanguka, anaangalia mahali alipojikwaa, ili kuipata sababu iliyomfanya ajikwae na kuanguka, badala ya kuangalia alipoangukia tuu, anaamka na kuendelea na safari yake, hivyo huko mbele atakuja kujikwaa tena na kuanguka tena!".
Watu wanashupalia matokeo badala ya kujiuliza chanzo!. Huu ni ujinga, ignorance!.
Watanzania ni Ignorants?, yaani Sisi Watanzania ni Wajinga?.
Mtanisamehe sana kwa kuanza huu mjadala kwa maneno makali, kuwa sisi Watanzania tulio wengi ni "ma-ignorants!", yaani wengi wetu ni watupu kabisa vichwani mwetu au ni weupe tii!, ni vichwa maji kabisa!, uwezo wa kufikiri wa wengi wetu, "logical thinking", ni mdogo au sifuri, ndio maana hatuna uwezo wa kufanya maamuzi sahihi ya maana, "to make informed decisions", hali inayopelekea, tunapelekwa pelekwa tuu kama lingo'ombe au mazuzu!, kiasi kwamba, wengi wetu tunashabikia zaidi na kushupalia vitu vidogo vidogo ambavyo ni non issues, na immaterial, ambazo sio chanzo bali ni matokeo tuu, badala ya kudeal na issues zenyewe ambazo ndicho chanzo, cha haya madhila, kilizopelekea haya yatokanayo, yatokee, vyanzo haviuliziwi, havishungulikiwi, havizungumzwi!, haviguswi!, tuna deal na matokeo tuu!.
Ujinga Huu wa Watanzania, Kutojiuliza Chanzo cha Tatizo Umeanzia Wapi na Uko Wapi?.
Hii ignorance ya Watanzania ina cut across society yetu na ku reflect ndani ya kila sekta ya jamii yetu kuanzia ndani ya familia zetu, mitaa yetu, vitongoji vyetu, vyama vyetu, hadi ndani ya Bunge letu tukufu, tuna wabunge ma ignorants mule hakuna mfano!, tuna viongozi wetu wengi tuu ni ma ignorants hadi ndani ya cabinet yetu kuna mawaziri ni ma ignorants, uthibitisho ni jinsi mawaziri wetu wanavyotimuliwa from time to time!, tuna viongozi wa taasisi za umma ambao ni ma ignorants na jambo kubwa na la ajabu, tuna hadi viongozi wetu wakuu wa vyombo vya dola, nao ni ma ignorants tuu, na wana jf wengi pia ni ma ignorants tuu, nikiwemo mimi mwana JF, mwenzenu Paskali, tofauti kati yangu na baadhi ya mfano wangu, ni ma ignorants ambao tunajitambua na tunasema, wakati wengi wa ma ignorants wenzetu, hukaa kimya, hivyo kuificha hiyo ignorance yao, lakini sisi ambao kwa bahati mbaya sana, hatukujaliwa aibu ya kuogopa kuongea, tunaongea wazi wazi hivyo tunaionyesha hiyo ignorance yetu kwa uwazi kabisa kwa ku speak out our minds and expressing our opinions.
Jee Ujinga Huu ni Mtaji?.
Yes ujinga ni mtaji!. Ni kufuatia ignorance hii, Chama cha Mapinduzi, (CCM), kimekuwa kinaitumia ignorance hii ipasavyo kwa kuifanya ndio mtaji wake wa kupatia kura ubwete za ushindi, mwaka hadi mwaka, na mwakani tutaichagua tena CCM kwa kuipa ushindi wa kishindo!.
Kwa Nini Mtu Uwaite Watanzania Wenzako Kuwa ni Wajinga?.
Naomba kuweka wazi kuwa kwenye bandiko hili, sijatukana mtu, wala sijawaita watu ni wajinga, bali nimeuliza tuu swali kuwa, Jee Sisi Watanzania ni Wajinga?. Majibu ya swali hili ndiyo yatakayosema kama sisi ni ma ignorants au la!, kama ni ma ignorants, huu ujinga wetu ni ujinga wa aina gani au tumelogwa?. Maswali haya ni kufuatia kujiuliza, haiwezekani kabisa, kwa watu wenye akili zao timamu, wakafanyiwa mambo ya ovyo ya ajabu ajabu kama haya, lakini inapofikia wakati wa kuwapima hao waliowachagua, bado wakawachagua watu wale wale, chama kile kile, na baadae kuja kufanyiwa madudu yale yale!.
Jee Hali Ilikuwa Hapo Mwanzo, Ukilinganisha na Hali Ikoje Sasa?
Wakati tulipopata uhuru toka kwa mkoloni, Tanzania tulikuwa na maadui wakuu watatu, ujinga, umasikini na maradhi, lakini hadi leo miaka zaidi ya 50 baada ya uhuru, sio tuu, bado tunao wale maadui wakuu watatu bali sasa, ujinga umeongezeka mara dufu!, umasikini sasa ni uliotopea!, na maradhi yamezidi hadi mengine ni janga la taifa kwa sababu hayana tiba!. Kila siku ni afadhali ya jana!. Wazee wa sasa wanasema, hali ilivyo sasa ni mbaya hadi kujiona zamani enzi za mkoloni ni afadhali kuliko sasa!. Kitu kibaya zaidi, ni sasa tumeongeza idadi ya maadui wakuu, wakiwemo rushwa na ufisadi, ambapo mazao yake ni pamoja na DCP, Deep Green, Meremeta, TanGold, Alex Stewart, EPA, Richimond, na sasa Escrow.
Uzuri wa Watanzania ni Upi Katika Kukumbatia Umasikini, Ujinga, Maradhi, Rushwa na Ufisadi
Kitu kizuri cha ajabu kuhusu sisi Watanzania ni kujifanya kupiga kelele sana as if tunauchukia umasikini, ujinga, maradhi, rushwa na ufisadi, lakini sisi wale wale, mwaka hadi mwaka, tunawachagua watu wale wale, chama kile kile, sera zile zile, tukitegemea matokeo tofauti!, hii ni nini kama sio ignorance at the highest levels?!. Keshokutwa tunawapa serikali za mitaa!, mwezi April tuna wapitishia ile "Bora Katiba" kwa kura za ndio za kutosha, na zisipotosha "zitatosheshwa!",na October, 2015, tunamalizia kazi, kwa kuirudisha CCM kwa ushindi wa kishindo!.
Ignorance Kwenye Mjadala wa Escrow
Ignorance hii imejidhihiri wazi kwenye huu mjadala wa Escrow unao endelea sasa, ambapo wengi wetu, tumejikita kwenye issue ya fedha za Escrow tuu, ambayo sio a very big deal!, fedha ya escrow ni matokeo tuu ya hili jinamizi linaloitwa IPTL!, hakuna anayezungumzia chanzo, na hiyo pesa iliyokuwa inawekwa kwenye hiyo account ya escrow ni fedha ndogo ya capacity charges only, bado Tanesco inalipa mabilioni kwa mabilioni ya kulipia Utilities huko huko IPTL, Aggreko, Simbion, Songas!, badala ya watu kujadili chanzo, na kwa nini tumefika hapa, wao wanajadili matokeo tuu!. Hii kama sio ignorance ni nini?!.
Kwanini Tufanye Cherry Picking Kwenye Kutafuta Mbuzi wa Kafara?!.
Katika kuwabaini wahusika, wa hili jinamizi la Esscrow, badala ya kuwatafuta wahusika wakuu waliosababisha tufike hapa, watu wanafanya "cherry picking ya kumchagua huyu na yule, na kumuepusha yule na yule ili mradi tuu apatikane "mbuzi wa kafara!", na miongoni mwa wahusika, sijaisikia kabisa BOT ikitajwa tajwa, simply kwa sababu yeye ni dalali tuu!. Kama escrow ni account ya ubia kati ya serikali na IPTL, BOT ililipaje zile pesa kwa PAP ambaye has got nothing to do with account hiyo kabla ya kwanza kujiridhisha?!.
Jee Escrow Ndio Issue Sana Kivile?, Au Issue ni IPTL?. Mbona Mnashupalia Matokeo Badala ya Chanzo?!.
Escrow sio issue sana kivile!, escrow ni matokeo tuu, issue yenyewe haswa ni IPTL, ilikujaje, ilipitaje, ilikubalikaje kutuwekea mitambo chakavu ya mtumba, inayotumia obsolete technology?, ilikubalikaje na kupitishwaje bila ripoti ya EIA?. Sisi kama Taifa, tulikubalije kutozwa capacity charges za kiasi kile kwa mitambo ile?!, hii kama sio ignorance ni nini?!.
Kwa Nini Watu Wanataja Taja Tuu Majina?, Huu Kama Sio Ujinga ni Nini?!.
Watu wanataja taja tuu majina!, wananyooshea watu vidole!, wanawapigia kelele waliolipwa na JR tuu, waliolipwa na PAP wao wako wapi?, Walioileta IPTL wako wapi?, hii ni nini kama sio ignorance?!, au tumelogwa?!. Tunapaswa kuwatafuta responsible people tangu hili jinamizi la IPTL limekuja nchini, tuwawajibishe!, na sio kutafuta mbuzi wa kafara, au kama kawaida yetu, tufunike kombe mwanaharamu apite!".
Paskali