Interested Observer
JF-Expert Member
- Mar 27, 2006
- 3,384
- 4,428
Kwa mwandishi wa habari na mtu ambaye unadai umesoma sheria UDSM, sijawahi kuona mwandishi mbovu kama wewe!
Kanuni nyepesi tu za uandishi zinakushinda. Mjinga nambari moja utakuwa ni wewe.
Unaweka alama za nukuu hata pasipotakiwa. Unarudia rudia maneno yaleyale uliyoyaandika katika lugha moja na kuyaandika katika lugha ingine.
Hivi una matatizo gani wewe?
Hakuna mtu mshenzi mshenzi duniani. Yupo mjinga mjinga. Ila yupo mtu Mshenzi.
wewe hizo pesa za kwenye escrow account prof.benno ndulu ambaye ni gavana alishashtukia mchezo na alitaka executive order kutoka ofisi kuu ikulu na raisi ndiye aliyetoa executive order.jamani hamsikii hata nyaraka zinazosomwa kuna
zingine zimezuiwa ili kumlinda raisi alie juu
ambae ndie mwizi mkuu.pia account moja ya
mkombozi wamegoma kuisoma ambayo ndio
ilikuwa na mgao wa jumla. Pia stanbic bank
taarifa zake zimefichwa ni wazi raisi akitajwa
basi ni mtikisiko wa nchi.
Unataka kusemaje na wewe. Hebu potea
Kwa mwandishi wa habari na mtu ambaye unadai umesoma sheria UDSM, sijawahi kuona mwandishi mbovu kama wewe!
Kanuni nyepesi tu za uandishi zinakushinda. Mjinga nambari moja utakuwa ni wewe.
Unaweka alama za nukuu hata pasipotakiwa. Unarudia rudia maneno yaleyale uliyoyaandika katika lugha moja na kuyaandika katika lugha ingine.
Hivi una matatizo gani wewe?
Tundu Lissu alizungumzia hilo hadi akaombewa mwongozo wa eti wa 'kulitumia jina la rais kwa dhihaka!'. Soma kipande hiki kwa ajili ya rejea:... wanawapigia kelele waliolipwa na JR tuu, waliolipwa na PAP wao wako wapi?, Walioileta IPTL wako wapi?...
Hata kama tutam-criticize Pasco kwavile anaandika vitu tusivyopenda kuvisikia lakini bado ukweli upo pale pale kwamba maamuzi ya PAC yanaonesha wazi kwamba yanalinda baadhi ya watu na kuwashupalia baadhi ya watu... na mmoja wa ambao PAC imemshupalia ni Muhongo! Hata ukimsikiliza Zitto wakati anahitimisha mjadala, alitumia muda mrefu sana kumwa-attack Muhongo kuliko muda alioutumia kum-attack Werema ambae kwa maoni yangu WErema ndio muhusika namba moja katika sakata hili! Unless kama Werema alikuwa anatekeleza maagizo ya wakubwa wake, lakini nafasi ya Werema katika sakata hili ni kubwa kuliko Muhongo ambae PAC ilimkomalia... lakini hata hivyo, siwezi kushangaa kwavile Muhongo ni msema hovyo na ameshawahi kuwachana hadharani baadhi ya wajumbe wa PAC kwahiyo PAC ni kama wanalipiza kisasi na kutaka kumchinjia baharini!!
Tukirudi kwenye suala la PAC kulinda baadhi ya watu! Hivi unaiache BOT katika sakata hili? Wakati Zitto anasoma Ripoti yake alikuwa anaonesha wazi kwamba anamlinda Gavana wa BOT kwa maneno kama vile "Gavana wa BOT alijitahidi sana...." na upuuzi mwingine kama huo! This's stupid, I repeat, it's stupid kwavile hakuna chochote ambacho Zitto alikuwa anakifanya zaidi ya kumlinda Gavana!
Labda niwajuze jambo wasiofahamu taratibu za kibenki! Tunapoingia benki hizi za kawaida, mtu mwenye daraja la chini kabisa benki(apart from supporting staffs) ni Teller... narudia, staff wa daraja la chini kabisa bank ni Teller!!! Lakini ingawj Teller ndie staff wa daraja la chini kabisa; yeye ndie mwenye maamuzi ya mwisho kabisa ya kulipa au kutolipa transaction iliyopo mbele yake! Hata Branch Manager hana ubavu wa kumlazimisha Teller kulipa kitu ambacho Teller ana mashaka nacho! Hata CEO hana ubavu wa kumlazimisha Teller kulipa malipo ambayo Teller hajajiridhisha kama ni genuine payments! Kama iliyopo mbele ya desk la Teller ni Cheque... basi cheque hiyo hata iwe na mihuli ya RPC, IGP, CAG, TAKUKURU, IKULU na takataka zote unazozijua wewe, bado Teller kama anajiamini, na hajajiridhisha if the payment is genuine, anayo haki with no offense, kukataa kulipa cheki husika na humfanyi chochote kile kwa mujibu wa sheria! Pamoja na mamihuri yote hayo, Teller anayo haki ya kugoma na kumwambia yeyote asiye na mashaka juu ya transaction husika, basi na alipe yeye!!!
Sasa ikiwa ka-Teller tu kana maubavu yote haya, what about BOT? BOT walikuwa na uwezo na haki ya kukataa kufanya malipo ikiwa hawajajiridhisha hata kama ingekuwa ni maagizo kutoka kwa MoF au Ikulu! Na sitaki kuamini kwamba Ndulu haifahamu hii role yake, anaifahamu lakini aliamua kulinda kibarua chake!!!! Sasa ili mradi PAC imetumia kila nafasi kumsafisha Ndulu, ni wazi kwamba iliamua kwa makusudi uwachinjia baharini wale isiowataka na kuwalinda wale inaowataka...
Wanabodi,
Mtanisamehe sana kwa kuanza huu mjadala kwa maneno makali, kuwa sisi Watanzania tulio wengi ni "ignorants!", vichwa maji kabisa!, vichwani ni weupe!, uwezo wa kufikiri, "logical thinking", ni sifuri, ndio maana hatuna uwezo wa kufanya maamuzi ya maana, "informed decisions", hali inayopelekea, tunapelekwa pelekwa tuu kama mazuzu!, kiasi kwamba, wengi wetu tunashabikia zaidi na kushupalia vitu vidogo vidogo ambavyo ni non issues, na immaterial, ambazo sio chanzo bali ni matokeo tuu, badala ya kudeal na issue zenyewe ambazo ndicho chanzo, kilizopelekea haya yatokanayo, havishungulikiwi, havizungumzwi!, haviguswi!.
Hii ignorance ya Watanzania ina cut across society yetu na ku reflect ndani ya kila sekta ya jamii yetu kuanzia ndani ya familia zetu, mitaa yetu, vitongoji vyetu, vyama vyetu, hadi ndani ya bunge letu, tuna wabunge ma ignorants mule!, tuna viongozi wetu ma ignorants hadi ndani ya cabinet yetu!, tuna viongozi wa taasisi za umma ma ignorants hadi t, tuna viongozi wetu wa vyombo vya dola ni ma ignotants, na wana jf wengi pia ni ignorants tuu, nikiwemo mimi mwana JF, Pasco wa jf, tofauti na wengi maignorants wenzetu, wanajikalia kimya, hivyo kuificha hiyo ignorance yao, lakini sisi wengine ambao kwa bahati mbaya sana, hatukujaliwa aibu, tunaionyesha hiyo ignorance yetu kwa ku speak out and expressing our minds, tatizo, ni, in so doing, tunajikuta tumewaambukiza ignorance, hata wengine ambao hawakuwa ignorants!. Sorry for this.
Ni kufuatia ignorance hii, Chama cha Mapinduzi, (CCM), kinaitumia ignorance hii ipasavyo kwa kuifanya ndio mtaji wake wa kupatia kura za ushindi, mwaka hadi mwaka, na mwakani tutaichagua tena CCM kwa kuipa ushindi wa kishindo!.
Hisia za kujiuliza, kama sisi ni ma ignorants au tumelogwa, ni kufuatia kuwa na mtazamo, ya kuwa haiwezekani, watu wenye akili zao timamu, wakafanyiwa mambo ya ajabu ajabu kama haya, lakini bado tunaichagua CCM tena na tena!.
Wakati tulipopata uhuru toka kwa mkoloni, tulikuwa na maadui wakuu watatu, ujinga, umasikini na maradhi, lakini hadi leo miaka zaidi ya 50 baada ya uhuru, sio tuu, wale maadui wakuu watatu bado wapo, bali ujinga umeongezeka mara dufu, umasikini sasa ni uliotopea, na maradhi hadi mengine ni janga, vimeongezeka afadhali ya zamani na enzi za mkoloni, bali pia, tumeongeza idadi ya maadui wakuu, wakiwemo rushwa na ufisadi, ambapo mazao yake ni pamoja na DCP, Deep Green, Meremeta, TanGold, Alex Stewart, EPA, Richimond, na sasa Escrow.
Kitu kizuri cha ajabu kuhusu sisi Watanzania ni kujifanya kupiga kelele sana as if tunauchukia umasikini, ujinga, maradhi, rushwa na ufisadi, lakini sisi wale wale, mwaka hadi mwaka, tunawachagua watu wale wale, chama kile kile, sera zile zile, tukitegemea matokeo tofauti!, hii ni nini kama sio ignorance at the highest levels?!. Keshokutwa tunawapa serikali za mitaa!, mwezi April tuna wapitishia ile "Bora Katiba" kwa kura za ndio za kutosha, na zisipotosha "zitatosheshwa!",na October, 2015, tunamalizia kazi, kwa kuirudisha CCM kwa ushindi wa kishindo!.
Ignorance hii imejidhihiri wazi kwenye huu mjadala wa Escrow unao endelea sasa, ambapo wengi wetu, tumejikita kwenye issue ya fedha za Escrow tuu, ambayo sio a very big deal!, fedha ya escrow ni matokeo tuu ya hili jinamizi linaloitwa IPTL!, na hiyo pesa iliyokuwa inawekwa kwenye account ya escrow ni capacity charges only, bado Tanesco inalipa mabilioni kwa mabilioni ya kulipia Utilities huko huko IPTL, Aggreko, Simbion, Songas!, badala ya watu kujadili chanzo, na kwa nini tumefika hapa, wao wanajadili matokeo tuu!. Hii kama sio ignorance ni nini?!.
Katika kuwabaini wahusika, watu wanafanya "cherry picking ya kumchagua huyu na yule, na kumuepusha yule na yule ili mradi tuu apatikane "mbuzi wa kafara!", na miongoni mwa wahusika, sijaisikia BOT ikitajwa tajwa, simply kwa sababu yeye ni dalali tuu!. Kama escrow ni account ya ubia kati ya serikali na IPTL, BOT ililipaje zile pesa PAP?!.
Escrow sio issue sana kivile!, escrow ni matokeo tuu, issue yenyewe haswa ni IPTL, ilikujaje, ilipitaje, ilikubalikaje kutuwekea mitambo ya mtumba, obsolete technology, ilikubalikaje kukubali kutozwa capacity charges zile?!, hii kama sio ignorance ni nini?!.
Watu wanataja taja tuu majina!, wananyooshea watu vidole!, wanawapigia kelele waliolipwa na JR tuu, waliolipwa na PAP wao wako wapi?, Walioileta IPTL wako wapi?, hii ni nini kama sio ignorance?!, au tumelogwa?!. Tunapaswa kuwatafuta responsible people tangu hili jinamizi la IPTL limekuja nchini, tuwawajibishe!, na sio kutafuta mbuzi wa kafara, au kama kawaida yetu, tufunike kombe mwanaharamu apite!".
Pasco
Heshima mbele mkuu, mabandiko yako mengine kuhusu saga la escrow yanachanganya lakini ninaelewa wapi unataka tujiegemeze, Lisu alieleza vizuri, 1994 alienegotiate na kuitambua IPTL ni mkuu wa kaya akiwa maji, nishati na mdini, 1995 akiwa fedha, 2014 akiamuru fedha zitoke kwa ushauri wa AG, bunge hili suala wamegoma kabisa lisijadiliwe maana yake nini? Wananchi hatutaki kabisa kujiongeza? Hatuwezi kuungana na wale wachache wanaotutetea? Hebu tuamke uchunguzi mara ngapi? Tutaifishe IPTL na H.S. Seth akamatwe kama PAC ilivyoazimia kabla ya saga kuanza kujadiliwa. KWELI ITUWEKE HURU.
Hata kama tutam-criticize Pasco kwavile anaandika vitu tusivyopenda kuvisikia lakini bado ukweli upo pale pale kwamba maamuzi ya PAC yanaonesha wazi kwamba yanalinda baadhi ya watu na kuwashupalia baadhi ya watu... na mmoja wa ambao PAC imemshupalia ni Muhongo! Hata ukimsikiliza Zitto wakati anahitimisha mjadala, alitumia muda mrefu sana kumwa-attack Muhongo kuliko muda alioutumia kum-attack Werema ambae kwa maoni yangu WErema ndio muhusika namba moja katika sakata hili! Unless kama Werema alikuwa anatekeleza maagizo ya wakubwa wake, lakini nafasi ya Werema katika sakata hili ni kubwa kuliko Muhongo ambae PAC ilimkomalia... lakini hata hivyo, siwezi kushangaa kwavile Muhongo ni msema hovyo na ameshawahi kuwachana hadharani baadhi ya wajumbe wa PAC kwahiyo PAC ni kama wanalipiza kisasi na kutaka kumchinjia baharini!!
Tukirudi kwenye suala la PAC kulinda baadhi ya watu! Hivi unaiache BOT katika sakata hili? Wakati Zitto anasoma Ripoti yake alikuwa anaonesha wazi kwamba anamlinda Gavana wa BOT kwa maneno kama vile "Gavana wa BOT alijitahidi sana...." na upuuzi mwingine kama huo! This's stupid, I repeat, it's stupid kwavile hakuna chochote ambacho Zitto alikuwa anakifanya zaidi ya kumlinda Gavana!
Labda niwajuze jambo wasiofahamu taratibu za kibenki! Tunapoingia benki hizi za kawaida, mtu mwenye daraja la chini kabisa benki(apart from supporting staffs) ni Teller... narudia, staff wa daraja la chini kabisa bank ni Teller!!! Lakini ingawj Teller ndie staff wa daraja la chini kabisa; yeye ndie mwenye maamuzi ya mwisho kabisa ya kulipa au kutolipa transaction iliyopo mbele yake! Hata Branch Manager hana ubavu wa kumlazimisha Teller kulipa kitu ambacho Teller ana mashaka nacho! Hata CEO hana ubavu wa kumlazimisha Teller kulipa malipo ambayo Teller hajajiridhisha kama ni genuine payments! Kama iliyopo mbele ya desk la Teller ni Cheque... basi cheque hiyo hata iwe na mihuli ya RPC, IGP, CAG, TAKUKURU, IKULU na takataka zote unazozijua wewe, bado Teller kama anajiamini, na hajajiridhisha if the payment is genuine, anayo haki with no offense, kukataa kulipa cheki husika na humfanyi chochote kile kwa mujibu wa sheria! Pamoja na mamihuri yote hayo, Teller anayo haki ya kugoma na kumwambia yeyote asiye na mashaka juu ya transaction husika, basi na alipe yeye!!!
Sasa ikiwa ka-Teller tu kana maubavu yote haya, what about BOT? BOT walikuwa na uwezo na haki ya kukataa kufanya malipo ikiwa hawajajiridhisha hata kama ingekuwa ni maagizo kutoka kwa MoF au Ikulu! Na sitaki kuamini kwamba Ndulu haifahamu hii role yake, anaifahamu lakini aliamua kulinda kibarua chake!!!! Sasa ili mradi PAC imetumia kila nafasi kumsafisha Ndulu, ni wazi kwamba iliamua kwa makusudi uwachinjia baharini wale isiowataka na kuwalinda wale inaowataka...
Lakini si wewe unashindia kwenye mitandao kila siku kuwabeza wapinzani? Unapokosa posho za magamba unaungana na wapinzani. Wanapokupa mnofu unawabeza wapinzani. Hutabiriki. Wewe ni ndumila kuwili! Nadhani wewe ndiye mjinga namba moja!
Mkuu Maendeleo Tu, pole, sisi binadamu tunatofautiana uwezo wa kujieleza, uwasilishaji mada na kueleweka, ndio maana wengine huwa ni waliimu wa kufundisha wengine waelewe, sisi wengine ni wasema onyo, kazi yetu ni kusema chochote tunachokiona, na kuiacha kazi ya uelewa kwa wale tuu watakaoelewa, au kama hivi wachache wanaoelewa, kuwaelewesha na wengine kama hivi, anavyofanya huyu Mkuu SharkNiliposoma bila kuangalia author nilijaribu kuielewa mistari. Mwisho nilipojua ni Pasco nikabaki njia panda. Mkuu Pasco unajua hueleweki kabisa! Thread zako zinasigishana
Pasco,
Umeandika sana hapo juu! Nimejaribu kusoma neno kwa neno!!
Mwishowe nimekuja na summary au conclusion moja tu, kua SISI WATANZANIA NI WAJINGA SABABU YA KUENDELEA KUICHAGUA CCM PAMOJA NA MAPUNGUFU YAKE CHUNGU NZIMA!!