Escrow: Je, Watanzania ni ignorant au tumelogwa? Tuache cherry-picking kutafuta Mbuzi wa Kafara!

Nimenote mjadala mkubwa unaendelea baada ya Ngeleja kurejesha fedha za mgao wa escrow!, kwangu mimi huu ni muendelezo tuu wa hii hii ignorance niliyoizungumzia humu, tangu lini kupokea pesa au zawadi yoyote ikawa ni kosa?, kama wakati ukipokea, hukujua kama fedha hizo ni za wizi?.

Ila pia ignorance kubwa ni kushadadia wanaojulikana walipokea, jamani hawa ni wachache na walichopokea ni just a peanut!, wako Watanzania wenzetu, walipokea migao mikubwa ya fedha za wizi, kikiwemo chama fulani kilipokea mgao wa bilioni 40 za Kagoda, watu walipokea mgao wa Rada, Meremeta, Deep Green, Tan Gold, DCP, lakini kwa vile hawajulikani, they are OK!.

Mungu ibariki Tanzania.

Paskali.
 
Nyani Ngabu ,Reff : 2014 kama ndio Leo July 2017 unajihukumuje kuhusu kauli yako hii !? Je ujioni ulikuwa ni mmoja kati ya alicho lalamikia Pascal ataa kumwita mmbovu !? Tafakari chukua hatua kufuta ujinga Taifa liendembele .
 
nikiona alieanzisha uzi ni Pasco lazima niupitie ili niokoteokote vitu .

Labda nikuongezee kwamba Watanzania sio kichwa maji tu, bali vilevile ni kichwa cha mwendawazimu kila mtu anajifunzia kunyoa.
Wengine walishasema hili ni shamba la bibi.
Tofyo Reff: 2014 ndio leo July 2017 kwa kauli yako hii !? Ina maana ulikuwa nje ya kundi la wajinga ,jipongezee [emoji106] [emoji106] [emoji106]
 
Pascal Reff: 2014 ndio leo July 2017 kwa kauli yako hii !!?? Hongera sana na usichoke kutuaamsha wajinga lala [emoji106] [emoji106] [emoji106]
 
Kumbe ni kweli siku za mwizi ni arobaini "Things have started backfiring''
 
Hebu wataalamu wa sheria nisaidieni Mali ya wizi huwa inarudishwa?
Alichokifanya Ngeleja ni kukabidhi exhibit serikalini lakini amekabidhi sehemu isiyo sahihi, alipaswa akakabidhi kile kielelezo Takukuru.
 
Hebu wataalamu wa sheria nisaidieni Mali ya wizi huwa inarudishwa?
Alichokifanya Ngeleja ni kukabidhi exhibit serikalini lakini amekabidhi sehemu isiyo sahihi, alipaswa akakabidhi kile kielelezo Takukuru.
Mkuu Koroda, wizi ni kosa la jinai, hivyo linapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria kwa wahusika kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Lakini sisi Tanzania tulianzisha utaratibu mpya wa kushulikia wizi mkubwa kwa wezi wakubwa wa EPA kurejesha walichokwiba na kunakuwa hakuna kesi tena.

Hivyo Ngeleja is very right, kuzirejesha fedha zile kwenye safe custody ya serikali, ili ikikutikana escrow ni fedha za wizi, then he will be safe.

Kwa Tanzania, mwizi ni mwizi wa kuku na sio wa fedha nyingi.

Paskali
 
Umenikumbusha kesi ya Mwizi wa Kandambili na kibaba cha unga
 
Mayalla uko sahihi lakini ile ya EPA ni Mkuu wa Kaya wa wakati huo ndiye aliyeutangazia umma kwamba atakaerudisha pesa alizozipiga EPA basi atasamehewa na alitoa muda wa kikomo wa kurudisha Serikalini hizo pesa, na watu walirudisha kimyakimya. Hapa tu Mkuu wa Kaya alikuwa wa kwanza kuvunja sheria za Taifa analoliongoza lakini cha ajabu wanaojiita wabobezi wa sheria wa Taifa hili walishindwa hata kupaza sauti angalau kuonyesha kwamba alichokuwa anakifanya Mkuu wa Kaya ni uvunjifu wa sheria.
Nahisi hata Ngeleja amerejea ule ule utaratibu wa kuiba na kurudisha Serikalini na hakuna kesi.
Kweli hii nchi ni ya Watu wajinga na tusiojielewa.
Naunga mkono hoja yako Pascal Mayalla.
 
Pascally ndugu yangu huoni kama haya maneno yako ungeyasema kipindi mzee huyo JR anakamatwa hadi anapelekwa huko rupango yangekuwa na sauti?
P
 
Kwenye hii issue ya Escrow, tulikuwa tunatafuta mbuzi wa kafara, amepatikana ni Singa Singa Seth, na sasa mbuzi huyo kaenda kufia buchani kwa muuza supu, sasa James Rugemalila aachiwe, maisha yaendelee!.
Hiki nilichokisema humu, kimekuja kutokea kwa Mzee JR kukamatwa na kushitakiwa. Kiukweli kabisa, huyu Mzee ameshitakiwa kwa kuonewa bure, hana kosa lolote, baada ya Habinder Sing Sethi kukiri na kuachiwa huru, kinachofuatia ni Mzee JR kufutiwa kesi na kuachiwa huru bila masharti yoyote.

Wito wangu kwa Mzee JR, maadam karma imeisha washughulikia baadhi ya watesi wake, hana sababu ya kudai fidia yoyote ya kutiwa ndani kwa zaidi ya miaka 4 bila kosa lolote, hakuna kiwango chochote cha fidia kinaweza kumfidia kwenye dunia hii, hivyo aiachie karma imalizane na watesi wake wengine waliobakia.

Welcome back uraiani Mzee wetu JR.
P
 
Baada ya Mzee JR kuachiwa huru bila makosa yoyote, nayadurusu baadhi ya mabandiko yangu kuhusu kadhia hii, and I was 100% right. Bandiko hili lilikuwa linauliza kama Watanzania ni ignorants na nikasema anatafutwa mbuzi wa kafara, achinjwe, tufunike kombe mwanaharamu apite!. Ni kweli Mzee JR akakamatwa afanywe mbuzi wa kafara, watu wakisubiri siku tuu ya kuchinjwa, wafanye karamu. Bahati nzuri Mungu sii Athumani, mbuzi wa kafara hakuchinjwa na nadala yake kuna watu ya kuwakuta yamewakuta. Kuachiwa huku kunaendelea kuthibitisha jinsi tulivyo ignorant, unamshikilia mtu miaka mitano jela bila hatia yoyote kisha unamuachia!. Karma haitakuacha salama!.

Pia najua, itakuwa miongoni mwa masharti ya kuachiwa ni kutoishitaki serikali kudai fidia, lakini hata asiposhitaki, karma ya mateso yake, imeisha washughulikia baadhi ya watesi wake na waliobakia, karma yao inawasubiri.
Naendelea kusisitiza viongozi wetu tendeni haki.

Mzee JR, pole sana kwa mapito uliyopitia. Mungu ni mwema, shukuru kwa yote, karibu uraiani.

Paskali
 


Kumbe unaamini nguvu ya CCM ipo kwenye ujinga 😂
Mkuu Gichbo, karibu mitaa hii
P
 
nikiona alieanzisha uzi ni Pasco lazima niupitie ili niokoteokote vitu .

Labda nikuongezee kwamba Watanzania sio kichwa maji tu, bali vilevile ni kichwa cha mwendawazimu kila mtu anajifunzia kunyoa.
Wengine walishasema hili ni shamba la bibi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…