Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
Majasusi wa Mossad walivyoiba mkojo wa Rais Hafez Al-Assad wa Syria kwa kutumia choo cha bandia.
Rais wa zamani wa Syria bwana Hafez Assad (Baba yake na Bashar, rais wa sasa) alikuja kugundua ya kuwa idara ya ujasusi ya Israel (mafundi wa Mossad) walimtengenezea choo cha bandia kwa kutumia yeye tu pale alipoudhuria mazishi ya mfalme Hussein wa Jordan.
Ilikuwa si rahisi kwa walinzi wa Hafez kuweza kugundua kuwa kulikuwa na njama hiyo ya kuunda choo cha mtego baina na specialists wa mossad kwa kushirikiana na idara ya ujasusi ya Jordan.
Kilichofanya choo kile kuonekana si cha kawaida ni kwamba, bomba la kupitishia uchafu (haja kubwa na ndogo) halikuelekezewa kwenye shimo la choo bali kulikuwa na chombo maalum kama bakuli kubwa kidogo kwa ajili ya kukinga kisha kupeleka maabara kwa uchunguzi maalum.
Dakika chache baada ya rais wa Syria kutumia choo kile cha mtego, lile bakuli la kukingia lililokuwa limejaa mkojo wa Hafez lilikimbizwa chaaaaap mpaka Tel Aviv ambapo pathologists pamoja na biochemists wa Mossad walikuwa wameandaliwa kuufanyia uchunguzi wa kina.
Baada ya uchunguzi kufanyika kilichokuja kugundulika ni kuwa rais Hafez ambaye tayari alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya moyo na high blood pressure, kumbe ana magonjwa mengine zaidi ambayo ni cancer pamoja na kisukari, hivyo hatokuwa na muda mrefu sana wa kuishi.
Medical report ilionesha, mbali na magonjwa yaliyokuwa yanamsumbua Hafez, pia dawa alizokuwa akitumia ili kuweza kurefusha maisha yake.
Hafez alikuwa akikaribia ukingoni mwa maisha yake. Mtu aliyekuwa mshirika mkubwa katika mchakato wa amani ya mashariki ya kati.
Baada ya kupewa report ya mossad, waziri mkuu Ehud Barak alisisitiza diplomatic community ya Israel wakiongozwa na waziri wa mashauri ya kigeni (Huku Tanzania ni kama mzee wetu Augustine Mahiga) kuwa waingie makubaliano mapema na serikali ya Syria kabla Hafez hajafa kwa maana kwa maana hawajui ni nani atakayefuata baada ya Hafez kufariki.
Kulikuwa na dalili za kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria na Hafez ndio mtu pekee ambaye wayahudi waliweza kumuamini kutokana na msimamo wake.
Medical report iliyokuja kuandaliwa tena na specialists wa mossad pamoja na wale wa jeshini (MI) alionesha namna hali ya Hafez ilivyokuwa inazidi kuwa mbaya kiasi kwamba aliweza kufanya kazi kwa masaa machache sana kwa siku.
Report pia ikaeleza namna ambavyo Hafez alivyoahirisha ghafla safari ya kwenda Moscow pamoja na kushindwa kuhudhuria mazishi ya mfalme Hassan wa Morocco.
Specialists wa Mossad na MI wakaja kugundua ya kuwa rais Hafez alikuwa akilazwa kila baada ya miezi mi nne ili kuweza kubadilishiwa damu.
Itaendelea wiki ijayo. Stay tunned......