*UHALISIA TARIME: MLINZI WA ESTHER MATIKO ALIYEKAMATWA NI JAMBAZI SUGU AMBAYE AMEKUWA AKITAFUTWA NA POLISI SIKU NYINGI*.
• Alikamatwa akiwa na Esther Matiko katika Hotel ya Blue Sky – Tarime.
• Esther alijaribu kuzuia Polisi kumkamata muhalifu, kwa kisingizio ni Mlinzi wake.
• Wasingizia amekamatwa katika ofisi yao wakati kakamatwa Hotelini.
• Sababu ya hali yao kuwa mbaya waamua kutumia majambazi ili kutengeneza kikosi cha kudhuru wana CCM.
• Jambazi mmoja anayemiliki bunduki mbili kiharamu wamefanikiwa kumtorosha lakini Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka.
Tukio la kukamatwa kwa mtuhumiwa wa ujambazi jana tarehe 14/10/2020, katika Hotel ya Blue Sky katika mji wa Tarime limegeuzwa kuwa propaganda ya kutafuta kura za huruma kwa Chadema katika Jimbo la Tarime Mjini.
Mtuhumiwa huyo wa ujambazi ambaye ni mmoja wa walinzi wa Esther ambaye kwa muda mrefu amekuwa akitafutwa na Jeshi la Polisi alikamatwa baada ya raia wema kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kuhusu mahali alipo.
Polisi walifika katika Hotel ya Blue Sky, na ukiona katika video wanayosambaza Esther alikuwa na Walinzi wengi ila huyo mmoja ndio alijaribu kukimbia na Polisi kumfukuza na kumkamata ndani ya Hotel hiyo.
Esther amejaribu kulialia kuwa wao wanaonewa sababu ya jambazi huyo kukamatwa, na alijaribu kutumia nguvu kuwazuia Polisi kufanya kazi yake ili baadae aje kulalamika anaonewa.
Kama mtu sio muhalifu kwa nini akimbie mara awaonapo Polisi? Mbona alikuwa na walinzi wengi na aliyekamatwa ni mmoja peke yake? Sababu ni kuwa wao wameamua kutumia wahalifu kwani wana uzoefu wa kudhuru watu.
Hata wiki iliyopita Polisi walikamata wahalifu wengine anaowatumia John Heche kama kikosi kazi cha kudhuru wana CCM, ambapo tayari walikuwa wametekeleza tukio la kumkata mapanga kijana mmoja wa CCM alipokuwa anatoka kwenye mkutano wa kampeni wa Chama Cha Mapinduzi.
Hivyo tunawashauri Chadema kwanza wakubaliane na hali kuwa mwaka huu hawana chao katika majimbo ya Tarime, pili wajiepushe na uhalifu ili kuutumia kutafuta kura za huruma, wameingia kwenye ushindani wakubali kuna kushinda na kushindwa. N a uhalifu hauna Chama, hata ukiwa mwanachama wa CCM ukafanya uhalifu utakamatwa tu. Kuwa Upinzani sio kinga dhidi ya uhalifu. Hakuna Chama chenye malaika pekee, hivyo wajiepushe na propaganda mfu, sisi tutakuwa tunazijibu na kuwaumbua, OVA.