Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Baada ya jana wabunge wa viti maalum kuapishwa, waandishi wa habari walifanikiwa kufanya mahojiano madogo na mbunge mmojawapo, Ester Matiko huku wengine wakigoma. Yafuatayo ni maswali kutoka kwa waandishi na majibu kutoka kwa Ester Matiko.
MWANDISHI: Mmepata baraka za Chama?
MATIKO: Nadhani wote tunajua taratibu za viti maalum mpaka kuweza kufika wabunge kuteuliwa, kuna utaratibu ambao unaendelea ndani ya chama kupitia wings mbalimbali na baadae chama kinabariki na majina yanaenda kwenye tume ya Taifa ya uchaguzi, binafsi nilitaarifiwa nimeteuliwa ndio maana nimefika hapa kuja kuapa.
MWANDISHI: Ulitaarifiwa na katibu?
MATIKO: Na mamlaka husika
MWANDISHI: Lakini katibu wa chama anasema hana taarifa na hilo na watachukua hatua kali dhidi yenu, hili unalizungumziaje?
MATIKO: Sijui zaidi ya hapo, kwa uchache wetu ambao tumekuja hapa, nipende tu kuwaambia watanzania, wategemee makubwa kwetu pamoja na kwamba tuko 19. Tunajua yote yaliyojiri kwenye uchaguzi mkuu ulioisha hadi tukapata hiki kidogo katika ushindi wetu mkubwa tuliokuwa nao.
MWANDISHI: Endapo chama kikiwafuta uanachama, mmejiandaa kuchukua hatua?
MATIKO: Tupo hapa kwa sababu ya chama kwa hiyo kikiona kuna mwingine anafaa zaidi ya Ester Matiko, niko tayari.
MWANDISHI: Awali msimamo wa chama chenu ilionekana haukubaliani kuweza nyie kushiriki hapa
MATIKO: Nadhani leo jukumu kubwa ni kuapa na tumetimiza hilo, yanayojiri mengine yote yanawezwa kuzungumzwa kwa wakati muafaka. Katika neno letu la shukrani tumesema dhahiri kabisa tunakishkuru chama cha demokrasia na maendeleo kututeua sisi watu 19 kukiwakilisha katika bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuweza kuwasemea watanzania na chama chetu sasa mengine kama yalijiri yakaenda yakarudi, yatazungumzwa kwa wakati muafaka. Asante.
MWANDISHI: Ndio kusema mmesalimu amri
MATIKO: Sio msemaji wa chama, mimi ni mbunge mteule, ASANTENI SANA.