Esther Matiko: Unapoingia Segerea unavuliwa nguo zote, unaambiwa "unakaguliwa na hata kama ni Mama utaruka kichurachura"

Esther Matiko: Unapoingia Segerea unavuliwa nguo zote, unaambiwa "unakaguliwa na hata kama ni Mama utaruka kichurachura"

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mbunge wa Viti Maalum, Esther Matiko, ameitaka Serikali kufunga mashine maalum kwenye Magereza ili kuondoa malalamiko ya Wafungwa kukaguliwa wakiwa uchi wa mnyama jambo ambalo ni kinyume na Haki za Binadamu.

“Unapoingia Segerea unavuliwa nguo zote, unaambiwa unakaguliwa na hata kama ni mama upo kwenye siku zako utaruka kichurachura ili waone kama kuna kitu umeficha huku chini"- Ameeleza Esther Matiko.

Tuwe na vifaa vya kisasa vya ukaguzi, kama kuna kitu ameweka tumboni kitaonekana kuliko wanavyofanya sasa hivi, ni udhalilishaji.

Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema ukaguzi wa namna hiyo ni mapokeo ya kikoloni na yanaondoa Utu wa Mtu kwasababu sio sawa kwa Wanawake na hata Wanaume kukaguliwa kwa hali ya udhalilishaji.

Aidha, Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amemtaka Mbunge kuweka wazi ni wapi matukio kama hayo yanafanyika ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua.

1620133705511.png

“Unapoingia Segerea unavuliwa nguo zote, unaambiwa unakaguliwa na hata kama ni mama upo kwenye siku zako utaruka kichurachura ili waone kama kuna kitu umeficha huku chini"- Ameeleza Esther Matiko

Aidha, Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amemtaka Mbunge kuweka wazi ni wapi matukio kama hayo yanafanyika ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua.

Ina maana huyu Waziri alikuwa usingizini wakati huyo Mbunge anataja Gereza la Segerea?
 
Prison is not home! Ndio maana kunatisha ili watu wasitende makosa!!!!ndio maana ni laaana ya vizazi na vizazi kwa mtu anayemsingizia mtu kosa ili ampeleke pasipo hatia.

Kuna wahalifu hasa wanawake wanaweza kuingia na vitu vya hatari kwa usalama wa wanaowalinda au watuhumiwa wengine.

Yeye kama mbunge ambaye ni muhimili wa dola angetoa njia sahihi ya kupekua na siyo kulalamika.
 
Prison is not home! Ndio maana kunatisha ili watu wasitende makosa!!!!ndio maana ni laaana ya vizazi na vizazi kwa mtu anayemsingizia mtu kosa ili ampeleke pasipo hatia.

Kuna wahalifu hasa wanawake wanaweza kuingia na vitu vya hatari kwa usalama wa wanaowalinda au watuhumiwa wengene

Yeye kama mbunge ambaye ni muhimili wa dola angetoa njia sahihi ya kupekua na siyo kulalamiks
Kwani aliposema kufungwe mashine maalum hajatoa solution ya tatizo?
 
Kwani aliposema kufungwe mashine maalum hajatoa solution ya tatizo?
Solution inayohitajika hapa ni ileeee ya KUWABAMIZA hao wahalifu wenzio ili wakitoka wawe na stori ya kukusimulieni nyie wahujumu wa taifa, walarushwa, mafisadi, wapiga dili na wachochezi na wavuruga-amani ya nchi. Umeelewa, umelewa, ama umeelemewa?
 
Ubaya wa hilo jambo au uzuri wake (Kulingana na uwezo wako wa akili) ni kwamba ipo siku hata wewe yatakakukuta.
 
Watakuwa walimfanya Mapoti!
Hapana hiyo mbn ni kawaida na ipo magereza yote Tanzania pindi mnapoingia tu mnakaba foleni mkiwa watupu aisee kama kuna kipengere kigumu jela ni hiko maana mtarushwa kichura kama dk 30 mpaka wakuone unatambaa ndo utaambiwa chukua nguo zako hapo hata kutembea shughuli wanadai eti kama ulikua na wazo la kutoloka basi hapo magoti hata kupiga hatua huwezi unakua hoi kama ulikua na tumbo la kuharaa unayamwaga mtu mzima kiufupi ni uzalilishaji
 
Prison is not home !!!! ndio maana kunatisha ili watu wasitende makosa!!!!ndio maana ni laaana ya vizazi na vizazi kwa mtu anayemsingizia mtu kosa ili ampeleke pasipo hatia...

Kuna wahalifu hasa wanawake wanaweza kuingia na vitu vya hatari kwa usalama wa wanaowalinda au watuhumiwa wengene

Yeye kama mbunge ambaye ni muhimili wa dola angetoa njia sahihi ya kupekua na siyo kulalamiks
Si amesema fungeni mashine?

Amandla...
 
Aliposema zifungwe za kisasa za ukaguzi hukuelewa au?
 
Mbunge wa Viti Maalum, Esther Matiko, ameitaka Serikali kufunga mashine maalum kwenye Magereza ili kuondoa malalamiko ya Wafungwa kukaguliwa wakiwa Uchi wa mnyama jambo ambalo ni kinyume na Haki za Binadamu

“Unapoingia Segerea unavuliwa nguo zote, unaambiwa unakaguliwa na hata kama ni mama upo kwenye siku zako utaruka kichurachura ili waone kama kuna kitu umeficha huku chini"- Ameeleza Esther Matiko

Tuwe na vifaa vya kisasa vya ukaguzi, kama kuna kitu ameweka tumboni kitaonekana kuliko wanavyofanya sasa hivi, ni udhalilishaji

Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema ukaguzi wa namna hiyo ni mapokeo ya kikoloni na yanaondoa Utu wa Mtu kwasababu sio sawa kwa Wanawake na hata Wanaume kukaguliwa kwa hali ya udhalilishaji

Aidha, Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amemtaka Mbunge kuweka wazi ni wapi matukio kama hayo yanafanyika ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua.
Kwanini waziri anauliza atajiwe ni gereza lipi ili wahusika wachukuliwe hatua?

Hatua gani atazochukua wakati huo ndio utaratibu wa magereza zote nchini?

Inawezekana huyu waziri hajawahi kuwekwa mahabusu na hatimaye gerezani ndio maana kuna umuhimu wa viongozi wa kisiasa karibu wawe wanafungwa kwanza ili wajifunze ni kwa kiwango gani raia huwa wanadhalilika gerezani.

Wanasiasa ndio watungaji wa sheria, spika kudai ni sheria za mapokeo kutoka ukoloni kwa hiyo yeye kama mkuuwa mhimili wa utungaji sheria kwanini hajawahi kuishauri serikali kurekebisha sheria hizo dhalili?
 
Kama nchi tuna mifumo ya hovyo sana sana hivi kweli Karne ya 21 Bado huo upuuzi unaendelea ni aibu kubwa sana yaani daaaaa.

Hivi mbaka hua najiuliza sie waafrika hatuna akili za kujiongeza au tunasubiri mbaka mabeberu yatoe order kwamba hebu achaneni na kicho fanyeni hivi!

Ndio sisi Kama makondoo tuwafuate Maana Kuna vitu Kama binadamu tuliokamilika hatuhitaji kujifikiria mara mbili kuvifanyia marekebisho!
 
Back
Top Bottom