Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mbunge wa Viti Maalum, Esther Matiko, ameitaka Serikali kufunga mashine maalum kwenye Magereza ili kuondoa malalamiko ya Wafungwa kukaguliwa wakiwa uchi wa mnyama jambo ambalo ni kinyume na Haki za Binadamu.
“Unapoingia Segerea unavuliwa nguo zote, unaambiwa unakaguliwa na hata kama ni mama upo kwenye siku zako utaruka kichurachura ili waone kama kuna kitu umeficha huku chini"- Ameeleza Esther Matiko.
Tuwe na vifaa vya kisasa vya ukaguzi, kama kuna kitu ameweka tumboni kitaonekana kuliko wanavyofanya sasa hivi, ni udhalilishaji.
Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema ukaguzi wa namna hiyo ni mapokeo ya kikoloni na yanaondoa Utu wa Mtu kwasababu sio sawa kwa Wanawake na hata Wanaume kukaguliwa kwa hali ya udhalilishaji.
Aidha, Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amemtaka Mbunge kuweka wazi ni wapi matukio kama hayo yanafanyika ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua.