Esther Matiko: Unapoingia Segerea unavuliwa nguo zote, unaambiwa "unakaguliwa na hata kama ni Mama utaruka kichurachura"

Esther Matiko: Unapoingia Segerea unavuliwa nguo zote, unaambiwa "unakaguliwa na hata kama ni Mama utaruka kichurachura"

Sheria zote kandamizi za kikoloni tumezirithi as if tz sio taifa huru.
1. Mfano Sheria iliyotumika kuvunja nyumba za watu Kimara Mbezi Kibamba Ni Sheria ya mkoloni 1931.
2. Sheria zote kandamizi wanazotumia polisi ni za kikoloni. Kama Ile ya kumuuliza mtu kabila.
Maafisa wa magereza watu wazima na familia zao wanaona fahari kabisa kumkagua mwanamme mwenzake Tena mtu wa miaka mingi Kama yule jamaa yake singasinga sehemu za haja kubwa. Halafu jioni anamuambia mkewe anatoka kazini. Kazi ya kuangalia mik***u ya wanaume wenzake.
Pathetic.
 
Kama una akili timamu huwezi kuingia kwenye haya majeshi ya kipuuzi
Binafsi siwezi kudhalilika kwa sababu yoyote. Mtu pekee anaeweza kukagua makalio yangu ni daktari na iwe imelazimu kuna ugonjwa usipotobika labda nitahatarisha maisha yangu, vinginevyo hakuna.
 
Unaonekana umeangalia movie ya escape from sobibo, mkuu! Yale siyo maisha halisi mkuu ni maigizo mkuu, na pia ni hali zilizokua karne ya 16 na 17!
Siyo utoto wa movies naongelea kitu ambacho ninakifahamu asilimia 100%. Kwenye magereza ya wenzetu kuna A cat mpaka D cat prisons.ukiwa A cat prison lazima upitie hicho kioo.Tii sheria bila shuruti.
 
Siyo utoto wa movies naongelea kitu ambacho ninakifahamu asilimia 100%. Kwenye magereza ya wenzetu kuna A cat mpaka D cat prisons.ukiwa A cat prison lazima upitie hicho kioo.Tii sheria bila shuruti.
Black corn’s man!
 
Mbunge wa Viti Maalum, Esther Matiko, ameitaka Serikali kufunga mashine maalum kwenye Magereza ili kuondoa malalamiko ya Wafungwa kukaguliwa wakiwa uchi wa mnyama jambo ambalo ni kinyume na Haki za Binadamu.

“Unapoingia Segerea unavuliwa nguo zote, unaambiwa unakaguliwa na hata kama ni mama upo kwenye siku zako utaruka kichurachura ili waone kama kuna kitu umeficha huku chini"- Ameeleza Esther Matiko.

Tuwe na vifaa vya kisasa vya ukaguzi, kama kuna kitu ameweka tumboni kitaonekana kuliko wanavyofanya sasa hivi, ni udhalilishaji

Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema ukaguzi wa namna hiyo ni mapokeo ya kikoloni na yanaondoa Utu wa Mtu kwasababu sio sawa kwa Wanawake na hata Wanaume kukaguliwa kwa hali ya udhalilishaji.

Aidha, Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amemtaka Mbunge kuweka wazi ni wapi matukio kama hayo yanafanyika ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua.
wakati wanafanyiwa hayo huyo ndugai anayewatetea alikuwa India au alikwepo Tz
 
nakumbuka nilipelekwa gereza la Butimba Mwanza aise unavua nguo zote unaweka pembeni unabaki kama ulivozaliwa.

wakati wakuingia na wakati wa kutoka pia.

ni noma sana
 
Hakuna jela yeyeto duniani mfungwa anaingia bila kuvuliwa nguo.

Hata huko ulaya na marekani kote lazima uvuliwe nguo.


Hoja mfu kabisa,,
 
Hakuna nchi duniani ambapo mfungwa akiingia magereza havuliwi nguo zote. Huu ni utaratibu wa magereza zote duniani, unavuliwa nguo zote, unakaguliwa na kupewa uniform za wafungwa.
Kama ni mwanamke unakaguliwa na askari magereza wanawake, na wanaume wanakaguliwa na askari magereza wanaume.
Mimi sioni kama kuna udhalilishaji katika hilo. Mfano, Wanawake mnapoumwa huwa mnakwenda hospitalini na kupimwa na madaktari wanaume (gynecologist wanaume), ambao huwapima mpaka via vyenu vya uzazi, tena gynecologist wanaume ndiyo wengi kuliko wanawake, mbona hapo hamsemi mnadhalilishwa??
 
Msijali mtetezi mpya wa wanawake Mr Ndungai atalishughulikia hilo haraka sana. Mwanaharakati wa wanawake.
 
Prison is not home! ndio maana kunatisha ili watu wasitende makosa!!!!ndio maana ni laaana ya vizazi na vizazi kwa mtu anayemsingizia mtu kosa ili ampeleke pasipo hatia.

Kuna wahalifu hasa wanawake wanaweza kuingia na vitu vya hatari kwa usalama wa wanaowalinda au watuhumiwa wengine.

Yeye kama mbunge ambaye ni muhimili wa dola angetoa njia sahihi ya kupekua na siyo kulalamika.
Dah hivi jamani mabichwa ya watu wengine yakoje? Unasema atowe njia sahihi na siyo kulalamika, kwani husoma alichosema? Ameshauri wazi kabisa kuwa kuwepo na vifaa vya kisasa vya kupekuwa wafungwa lakini umeruka na comments zisizo na kichwa wala miguu!
 
Unamjua mhalifu wewe, au unasimuliwa tu!??? Imagine yule kijana A Town aliyembaka mbibi, then akamnyonga. Be serious sometimes, sawa!??? Tena nasema sheria hukoooo ziwekwe kando watu waminywe haswa hadi akili ziwakae kumkichwa.
Utakuja kwenda tu
 
Simbacha aache kuwadharau WaTz ina maana haya yote hayajui hayasomi hayatambui?
Usijiinue Mtawala machozi ya walio wengi huko magerezani ni hukumu yenu mbele ya safari
Mungu halali wala hasinzii
 
hii inatakiwa kufutwa. imagine kwamba Sugu na Msigwa nao walivuliwa nguo na kurushwa kichurachura. mdee pia na wenzake walirushwa kichurachura. kumbe kuna umuhimu wa sheria kuhusu dhamana/bail kubadilishwa. ni udhalilishaji.
 
Solution inayohitajika hapa ni ileeee ya KUWABAMIZA hao wahalifu wenzio ili wakitoka wawe na stori ya kukusimulieni nyie wahujumu wa taifa, walarushwa, mafisadi, wapiga dili na wachochezi na wavuruga-amani ya nchi. Umeelewa, umelewa, ama umeelemewa?
ungejua jela hakuna mwenyewe ,usingeongea ayo binti yangu
 
Back
Top Bottom