Esther Matiko: Wanaobaka wahasiwe

Ubakaji ni ukatili wa hali ya juu sana.
Ni kweli kabisa. Na hata India wana adhabu ya kifo kwa wahusika. Ila kwa nchi yetu kabla ya kufikia huko, basi tungeimarisha kwanza mifumo yetu ya kisheria, ambayo kimsingi inatengeneza mianya mingi ya uonevu, dhuluma, na kubambikia watu kesi kupitia baadhi ya polisi wasio waaminifu, mahakimu, nk.

Kibongo bongo tukianzisha sheria za aina hii, wahanga watakuwa ni wengi sana. Mfano mdogo tu mpaka leo hakuna mwenye uhakika wa 100% iwapo Babu Seya na watoto wake walihukumiwa kihalali, au walibambikiwa ile kesi yao ya ubakaji!

Lakini pia tunaweza kudhibiti viashiria vya huo ubakaji kwa kutengeneza sheria zisizo na upendeleo! Nikupe mfano mdogo tu; kuna wale Waturuki wanaojenga reli ya mwendokasi, wanawaharibu sana watoto wadogo wa shule katika maeneo yote wanayopita kwa kuwarubuni na fedha kidogo kupitia uratibu wa baadhi ya Watanzania wenzetu wenye akili ndogo! Wamekuwa wakiwafanyia vitendo vya kikatili sana kwa kuwaingilia kinyume na maumbile, kuwalazimisha kunyonya maungo yao! Nk. Imagine watoto wa umri wa miaka 16, 17!

Umeona wamechukuliwa hatua za kisheria? Au ndiyo kusema Serikali haifahamu?
 
Unambakaje mtoto wa mwaka mmoja? I mean, unajua maana ya kubaka? Unajua maana ya mwaka? Unajua maana ya mmoja? How do you do it, or, how is it done?
 
Wametoka kuwaua wenye ulemavu wa ngozi kwa sababu za kishirikina sasa wamehamia kubaka watoto kwa sababu za kishirikiana.
 
Naungana na wewe kuwa ni imani za kishirikina, hiwezi sema mtoto amekuvutia mpaka umbake
 
Hivi baada ya bunge hili kuisha,yaani 2025,huyu na wenzake 18 watafanyia chama kipi kampeni?
Huo mwaka ndiyo watastaafu siasa rasmi. Au wafanye kuhamia Acti aka Fisiemu B
 
Wabunge nao wameishiwa na hoja za kuongea bungeni

Pesa za posho zinawalevywa
 
Pia uwakilishi huu ni kutoka wapi🤭
 
WEWE ni Mbunge wa Chama gani ? Vipi na WANAWAKE WASAGAJI ?
 
Na wenyewe wabakwe then ndio wahasiwe, serikali iajiri wabakaji special kwa ajili ya wenye kesi za kubaka [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hata fiance wako au mumeo akikuingilia kwa nguvu ikaonekana anataka kukubaka utakubali ahasiwe?

Seems ubakaji mmeuchukulia kwa angle moja tu.
Si anahasiwa endapo utaenda kusema mwenyewe [emoji23][emoji23]ILA ikiuchuna tu we na fiance wako nani atajua?? Ila kama ukitaka ahasiwe mapeeeema tu unaenda kushitaki
 
Hivi huyu dada ana mume/ameolewa?
 
Tatizo ni mamlaka husika kutofanya maamuzi sahihi kulishughulikia hili tatizo. Badala ya kumtafuta mganga wa kienyeji anayeeneza huo utaratibu wanamshughulikia aliyetenda peke yake. Wakati mganga anaendelea kuvuna wateja wa kutenda huo uhalifu.
Tatizo linakuja pale ambapo hao wanaotakiwa kusimamia sheria tunakutana nao wakiwa wamepanga misururu ya mashangingi yao (V8) kwa hao waganga. Bahati mbaya sana ni kwamba imani za kishirikina ni dini asilia za watanzania walio wengi. Mauaji ya Albino kanda ya ziwa, kupotea kwa watoto kule njombe na Mbeya, na ubakaji wa watoto kule Iringa ni jinai za kiimani. Hivyo tatizo kubwa liko kwenye jamii ya zetu na linahitaji mkakati wa aina yake ili kulimaliza.

Siyo kazi rahisi.......
 
Lakini inawezekana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…