Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Ni kweli kabisa. Na hata India wana adhabu ya kifo kwa wahusika. Ila kwa nchi yetu kabla ya kufikia huko, basi tungeimarisha kwanza mifumo yetu ya kisheria, ambayo kimsingi inatengeneza mianya mingi ya uonevu, dhuluma, na kubambikia watu kesi kupitia baadhi ya polisi wasio waaminifu, mahakimu, nk.Ubakaji ni ukatili wa hali ya juu sana.
Kibongo bongo tukianzisha sheria za aina hii, wahanga watakuwa ni wengi sana. Mfano mdogo tu mpaka leo hakuna mwenye uhakika wa 100% iwapo Babu Seya na watoto wake walihukumiwa kihalali, au walibambikiwa ile kesi yao ya ubakaji!
Lakini pia tunaweza kudhibiti viashiria vya huo ubakaji kwa kutengeneza sheria zisizo na upendeleo! Nikupe mfano mdogo tu; kuna wale Waturuki wanaojenga reli ya mwendokasi, wanawaharibu sana watoto wadogo wa shule katika maeneo yote wanayopita kwa kuwarubuni na fedha kidogo kupitia uratibu wa baadhi ya Watanzania wenzetu wenye akili ndogo! Wamekuwa wakiwafanyia vitendo vya kikatili sana kwa kuwaingilia kinyume na maumbile, kuwalazimisha kunyonya maungo yao! Nk. Imagine watoto wa umri wa miaka 16, 17!
Umeona wamechukuliwa hatua za kisheria? Au ndiyo kusema Serikali haifahamu?