Esther Matiko: Wanaobaka wahasiwe

Esther Matiko: Wanaobaka wahasiwe

Ubakaji ni ukatili wa hali ya juu sana.
Ni kweli kabisa. Na hata India wana adhabu ya kifo kwa wahusika. Ila kwa nchi yetu kabla ya kufikia huko, basi tungeimarisha kwanza mifumo yetu ya kisheria, ambayo kimsingi inatengeneza mianya mingi ya uonevu, dhuluma, na kubambikia watu kesi kupitia baadhi ya polisi wasio waaminifu, mahakimu, nk.

Kibongo bongo tukianzisha sheria za aina hii, wahanga watakuwa ni wengi sana. Mfano mdogo tu mpaka leo hakuna mwenye uhakika wa 100% iwapo Babu Seya na watoto wake walihukumiwa kihalali, au walibambikiwa ile kesi yao ya ubakaji!

Lakini pia tunaweza kudhibiti viashiria vya huo ubakaji kwa kutengeneza sheria zisizo na upendeleo! Nikupe mfano mdogo tu; kuna wale Waturuki wanaojenga reli ya mwendokasi, wanawaharibu sana watoto wadogo wa shule katika maeneo yote wanayopita kwa kuwarubuni na fedha kidogo kupitia uratibu wa baadhi ya Watanzania wenzetu wenye akili ndogo! Wamekuwa wakiwafanyia vitendo vya kikatili sana kwa kuwaingilia kinyume na maumbile, kuwalazimisha kunyonya maungo yao! Nk. Imagine watoto wa umri wa miaka 16, 17!

Umeona wamechukuliwa hatua za kisheria? Au ndiyo kusema Serikali haifahamu?
 
Mbunge wa Viti Maalum, Esther Matiko akichangia leo bungeni mjini Dodoma amesema kutokana na kuibuka kwa matukio mengi ya ukatili wa watoto anafikiria kuwa wanaobainika kufanya hivyo wahasiwe ili kuifanya jamii ya kitanzania kuwa salama.

=======

Esther Matiko: Kumekuwa na matukio ya kikatili dhidi ya watoto kwenye Taifa letu ambayo yamekuwa ni muendelezo. Ntacite mifano ambayo nimeishuhudia kwa wiki moja tu hii.

Jana kwenye jimbo la Shinyanga mjini kuna mtoto wa mwaka mmoja miezi 11 amebakwa na baba wa kambo, amepelekwa hospitalini Kambarage wakamrefer kwenda Bugando, ameharibiwa ametobolewa kote, mbele nya nyuma yule mtoto, inasikitisha sana, mtoto wa mwaka mmoja na miezi 11. Mengine yamekuwa reported, mengine sio reported.

Kama Taifa huyu mtoto hata akipona ataathirika kisaikolojia, sasa wapo wangapi kama hawa kwenye Taifa letu! Tunachukua hatua gani!

Songea kuna kijana wa miaka 19 amebaka na kulawiti watoto wa shule ya msingi zaidi ya nane wadogo. Iringa watoto wamelawitiwa na kubakwa wadogo.

What are we doing, tunafanya nini kama Taifa kwani hata hizi sheria tunazoweka naona kama zinakuwa loose, at a time unafikiria hata hawa watu wawe wanahasiwa kabisa or even you remove tha part ili jamii iweze kukaa vizuri.

Inaumiza sana kama Taifa na kama mzazi naumia.

Unambakaje mtoto wa mwaka mmoja? I mean, unajua maana ya kubaka? Unajua maana ya mwaka? Unajua maana ya mmoja? How do you do it, or, how is it done?
 
Wametoka kuwaua wenye ulemavu wa ngozi kwa sababu za kishirikina sasa wamehamia kubaka watoto kwa sababu za kishirikiana.
 
She's emotional and this is understandable, but severing some random dude's gonads will not mitigate a problem...

Wabakaji wa watoto wanakera sana, lakini tatizo siyo msukumo wa kingono peke yake bali pia imani za kishirikina. Mfano, siku za hivi karibuni takwimu zinaonesha kesi za unajisi wa watoto ziko kwa wingi mkoani Iringa. Zamani ilikuwa ni sehemu za Pwani. Baada ya kufuatilia kwa undani nikafahamu kwamba imani za kishirikina zinachangia sana haya kutokea.......
Naungana na wewe kuwa ni imani za kishirikina, hiwezi sema mtoto amekuvutia mpaka umbake
 
Hivi baada ya bunge hili kuisha,yaani 2025,huyu na wenzake 18 watafanyia chama kipi kampeni?
Huo mwaka ndiyo watastaafu siasa rasmi. Au wafanye kuhamia Acti aka Fisiemu B
 
Wabunge nao wameishiwa na hoja za kuongea bungeni

Pesa za posho zinawalevywa
 
Ameshatafuta chanzo cha tatizo, kabla ya kukimbilia kwenye hitimisho?

Yaani akiwa kama msomi, badala ya kuumiza kichwa kutafuta chanzo cha haya matatizo kushamiri kwenye jamii yetu, yeye anakimbilia kutatua tatizo kwa njia ya mkato!

Vipi ikitokea mtu akasingiziwa kubaka! Halafu akahasiwa! Halafu baadaye ikabainika, hakufanya hilo kosa! Itakuwaje?
Au lengo wanataka wabakie wenyewe, ili waishi kwa kusagana?
Pia uwakilishi huu ni kutoka wapi🤭
 
Mbunge wa Viti Maalum, Esther Matiko akichangia leo bungeni mjini Dodoma amesema kutokana na kuibuka kwa matukio mengi ya ukatili wa watoto anafikiria kuwa wanaobainika kufanya hivyo wahasiwe ili kuifanya jamii ya kitanzania kuwa salama.

=======

Esther Matiko: Kumekuwa na matukio ya kikatili dhidi ya watoto kwenye Taifa letu ambayo yamekuwa ni muendelezo. Ntacite mifano ambayo nimeishuhudia kwa wiki moja tu hii.

Jana kwenye jimbo la Shinyanga mjini kuna mtoto wa mwaka mmoja miezi 11 amebakwa na baba wa kambo, amepelekwa hospitalini Kambarage wakamrefer kwenda Bugando, ameharibiwa ametobolewa kote, mbele nya nyuma yule mtoto, inasikitisha sana, mtoto wa mwaka mmoja na miezi 11. Mengine yamekuwa reported, mengine sio reported.

Kama Taifa huyu mtoto hata akipona ataathirika kisaikolojia, sasa wapo wangapi kama hawa kwenye Taifa letu! Tunachukua hatua gani!

Songea kuna kijana wa miaka 19 amebaka na kulawiti watoto wa shule ya msingi zaidi ya nane wadogo. Iringa watoto wamelawitiwa na kubakwa wadogo.

What are we doing, tunafanya nini kama Taifa kwani hata hizi sheria tunazoweka naona kama zinakuwa loose, at a time unafikiria hata hawa watu wawe wanahasiwa kabisa or even you remove tha part ili jamii iweze kukaa vizuri.

Inaumiza sana kama Taifa na kama mzazi naumia.

WEWE ni Mbunge wa Chama gani ? Vipi na WANAWAKE WASAGAJI ?
 
Na wenyewe wabakwe then ndio wahasiwe, serikali iajiri wabakaji special kwa ajili ya wenye kesi za kubaka [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hata fiance wako au mumeo akikuingilia kwa nguvu ikaonekana anataka kukubaka utakubali ahasiwe?

Seems ubakaji mmeuchukulia kwa angle moja tu.
Si anahasiwa endapo utaenda kusema mwenyewe [emoji23][emoji23]ILA ikiuchuna tu we na fiance wako nani atajua?? Ila kama ukitaka ahasiwe mapeeeema tu unaenda kushitaki
 
Mbunge wa Viti Maalum, Esther Matiko akichangia leo bungeni mjini Dodoma amesema kutokana na kuibuka kwa matukio mengi ya ukatili wa watoto anafikiria kuwa wanaobainika kufanya hivyo wahasiwe ili kuifanya jamii ya kitanzania kuwa salama.

=======

Esther Matiko: Kumekuwa na matukio ya kikatili dhidi ya watoto kwenye Taifa letu ambayo yamekuwa ni muendelezo. Ntacite mifano ambayo nimeishuhudia kwa wiki moja tu hii.

Jana kwenye jimbo la Shinyanga mjini kuna mtoto wa mwaka mmoja miezi 11 amebakwa na baba wa kambo, amepelekwa hospitalini Kambarage wakamrefer kwenda Bugando, ameharibiwa ametobolewa kote, mbele nya nyuma yule mtoto, inasikitisha sana, mtoto wa mwaka mmoja na miezi 11. Mengine yamekuwa reported, mengine sio reported.

Kama Taifa huyu mtoto hata akipona ataathirika kisaikolojia, sasa wapo wangapi kama hawa kwenye Taifa letu! Tunachukua hatua gani!

Songea kuna kijana wa miaka 19 amebaka na kulawiti watoto wa shule ya msingi zaidi ya nane wadogo. Iringa watoto wamelawitiwa na kubakwa wadogo.

What are we doing, tunafanya nini kama Taifa kwani hata hizi sheria tunazoweka naona kama zinakuwa loose, at a time unafikiria hata hawa watu wawe wanahasiwa kabisa or even you remove tha part ili jamii iweze kukaa vizuri.

Inaumiza sana kama Taifa na kama mzazi naumia.

Hivi huyu dada ana mume/ameolewa?
 
Tatizo ni mamlaka husika kutofanya maamuzi sahihi kulishughulikia hili tatizo. Badala ya kumtafuta mganga wa kienyeji anayeeneza huo utaratibu wanamshughulikia aliyetenda peke yake. Wakati mganga anaendelea kuvuna wateja wa kutenda huo uhalifu.
Tatizo linakuja pale ambapo hao wanaotakiwa kusimamia sheria tunakutana nao wakiwa wamepanga misururu ya mashangingi yao (V8) kwa hao waganga. Bahati mbaya sana ni kwamba imani za kishirikina ni dini asilia za watanzania walio wengi. Mauaji ya Albino kanda ya ziwa, kupotea kwa watoto kule njombe na Mbeya, na ubakaji wa watoto kule Iringa ni jinai za kiimani. Hivyo tatizo kubwa liko kwenye jamii ya zetu na linahitaji mkakati wa aina yake ili kulimaliza.

Siyo kazi rahisi.......
 
Lakini inawezekana!
 
Back
Top Bottom