Wingi sio tija kaka, nimetoa mfano Wa watutsi Wa Rwanda Na Burundi ni asilimia 20 tu ya wanyarwanda lakini wanafahamika kwa kuwabagua wahutu miaka nenda rudi kule Rwanda Na Burundi mpaka kupelekea mauaji ya kimbari,
Nimekupa mfano Wa Afrika kusini wale makaburu hawazidi hata asilimia 30 ya watu wote Wa afrika kusini lakini walikuwa wabaguzi wabaya kabisa kuwahi kutokeà duniani Na mfumo wao Wa apartheid,
Na kusema kuwa hapa Tanzania hakuna makabila makubwa ndio maana hakuna ubaguzi sio kweli kaka, ubaguzi ulikuwepo ndio maana nyerere aliupiga vita sana , kwanza kulikuwa Na shule za madhehebu Na dini waliosoma huko ni waumini Wa dini hizo tu nyerere akazitaifisha zote ili kila mtu asome kuondoa ubaguzi, kulikuwa Na uwakilishi bungeni kutokana Na rangi yaani wazungu, waasia Na waafrika,
Makabila makubwa yapo kuna wasukuma ni zaidi ya milioni 10, kuna makabila yaliyowahi kupata elimu zamani na Maendeleo kama Wahaya , wachagga na wanyakyusa: kama sio juhudi za mwl nyerere ungekuta Tanzania tuna ukabila mkali sana kama ilivyo kwa Kenya makabila ya wakikuyu, wakalenji, wakaramoja, wakamba, waluo, waturkana, wakisii, wamasai,wameru nk