Ethiopia: Makundi 7 ya Waasi yaungana kupindua Serikali ya Abiy Ahmed

Ethiopia: Makundi 7 ya Waasi yaungana kupindua Serikali ya Abiy Ahmed

Historia ya Ethiopia ni tofauti mno na Tanzania
Mkuu hilo hawalijui hawa. Na hiki kinachotokea ni kama yale ya Siad Barre 1990s Somalia. Vita za ukabila zilizokuja kuzaa Alshabaab na mambo mengine Somalia.
 
Bob UKABILA unawamaliza hao. Wakushi na wasomali ni watu mafala kuwahi kutokea.
Hapo wanapigana kabila la Tigray ndio liongoze nchi.
Hawana lolote. Hawapiganii reforms bali wanapigania utawala wa kikabila.
Inaonekana hivyo lakini Jamaa anawaminya vibaya sana , acha wajitetee
 
hahaha Mussolini alivamia Ethiopia wakati wa vita kuu ya 2 ya dunia ilikuwa ni vita na siyo ukoloni wa kawaida, na ndiyo kipindi pekee ambacho ethiopia ilikaliwa na wageni kwa muda mfupi lkn vinginevyo ethiopia ndiyo nchi pekee duniani ambayo wazungu in last 200 years hawakuingia, na sababu ni hiyo kwamba Ethiopia was already Christian, ukiangalia ukoloni wote wa wazungu hawakujaribu kuingia na kutawala nchi ambzo zilikuwa htayari ni Christian ...
Vipi kuhusu Liberia
 
huwa wanadanganya ili wakubalike ni kama tu tanzagiza, ni crypto muslims, ethiopia was a Christian country, kwanza Ethiopians are one the earliest continous Christians in the world na wamekuwa under attack by muslims for centuries ...
Mama yake alikuwa mkristo ndio akachagua dini ya kikristo tangia zamani sio Leo.
 
Inaonekana hivyo lakini Jamaa anawaminya vibaya sana , acha wajitetee
Kaka mwaka jana tu sio mbali,jimbo la Amhara kukazuka ethnic cleansing ya minor groups. Hapo utasema jamaa anawaminya!??
Mwaka jana pekee kuliripotiwa zaidi ya vifo 300 vya mapigano ya kikabila hususan Oromia na Amhara.
Wana laana ya ukabila hao watu mkuu.
 
Hiyo Ndio Africa…. Nchi ikishaanza kuwa na positive outlook ya uchumi na nguvu lazima akina mangungo wa msovero wajitokeze kuimaliza

Hata kwetu wapo

Egypt ndo yuko nyuma ya upumbavu huu
 
Hiyo nchi ukabila utawamaliza. Afrika ni bara la laana na mahangaiko. Nadhani Mungu alituumba kuwa watumwa wa jamii zingine.
Kwani Ulaya hamna Ukabila? Urusi na Ukraine wanapigana kwa ajili ya Ukabila. Kwa ufupi nchi za Ulaya nyingi ni kabila moja moja hasa za Ulaya Mashariki.
 
CCM siipendi, ila nikiona chanzo cha migogoro mingi afrika naona sababu zinajirudiaga zile zile, naingiwa na ubaridi naona bora CCM iendelee kutawala tu.

hapo kwel wengi tunaona heri tubaki na zimwi tulijualo kuliko hawa wanaakarakat ambao hatujui nia yao nn
 
Makundi saba ya waasi nchini Ethiopia, yakiwemo makundi ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakipigana upande tofauti wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 2020 hadi 2022, yametangaza kuunda muungano wenye lengo la kuipindua serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed.

Muungano huo unaoitwa Ethiopian Peoples’ Forces Alliance for Survival, unayakutanisha makundi yenye asili tofauti za kikabila kutoka maeneo mbalimbali nchini humo, kuanzia Tigray kaskazini hadi Mkoa wa Somali kusini. Hata hivyo, baadhi ya makundi hayo bado yana migogoro kuhusu maeneo na masuala mengine.

Makundi mengi yameishutumu serikali kwa kujilimbikizia madaraka na kuyatenga maeneo mbalimbali nchini. Serikali kwa upande wake imesema imeanzisha mazungumzo ya kitaifa yenye lengo la kushughulikia mgawanyiko wa kisiasa na migogoro ya ndani ambayo imekuwepo kwa muda mrefu.

Muungano huo uliotangazwa Septemba 20, 2026 usiku unajumuisha Tigray People’s Liberation Front (TPLF) na Amhara Fano National Movement.

Fano, ambao ni muungano wa makundi yenye silaha kutoka eneo la Amhara, walipigana upande wa serikali ya shirikisho dhidi ya TPLF wakati wa vita vya Tigray vya mwaka 2020–2022. Vita hivyo vilisababisha vifo vya mamia ya maelfu ya watu na vilihusishwa na ukatili uliolenga makabila mbalimbali. Baadaye, Fano waliibuka dhidi ya serikali ya shirikisho, na mapigano hayo yameendelea katika eneo la Amhara tangu mwaka 2023, huku yakisababisha vifo vya maelfu ya watu.



================

Seven Ethiopian armed groups, including longstanding enemies who fought on opposite sides of a 2020-2022 civil war, said they have formed an alliance aimed at overthrowing Prime Minister Abiy Ahmed’s government.

The announcement of the Ethiopian Peoples’ Forces Alliance for Survival brought together am ethnically diverse body of groups based across the country, from Tigray in the north to Somali Region in the south. Some remain at loggerheads with other members over territory and other issues.

Abiy’s spokesperson, Billene Seyoum, said members of the alliance had been collaborating for a while with the financial backing of Ethiopia’s neighbour and historic adversary Eritrea.

“The recent announcement is only attesting (to) what the Ethiopian government has been alleging time and again,” she wrote in a text message on Monday.

Eritrea’s information minister did not immediately respond to a request for comment. Asmara has repeatedly denied similar accusations.

ALLIANCE INCLUDES FORMER FOES

The new alliance, announced late on Sunday, includes the Tigray People’s Liberation Front (TPLF) and the Amhara Fano National Movement.

Fano, a coalition of armed groups from the Amhara region, fought in support of the federal government against the TPLF during the 2020-2022 Tigray war, which resulted in hundreds of thousands of deaths and was marked by ethnically driven atrocities.

Fano subsequently rose up against the federal government in a conflict that has killed thousands in Amhara since 2023.

Many of the groups have accused the government of centralising power and marginalising the regions. The government says it has launched a national dialogue meant to address longstanding political divisions and internal conflicts.


Source: Reuters
sema kuna watu hii dunia empty mind kabisaaaaa,vikundi 7 mmeungana kuipindua serikali sasa mkishaipindua serikali what next mtabaki na muungano wenu au mtaanzana wenyewe kwa wenyewe?
 
Hiyo nchi ukabila utawamaliza. Afrika ni bara la laana na mahangaiko. Nadhani Mungu alituumba kuwa watumwa wa jamii zingine.
Siyo kweli. Fujo za Afrika ni matokeo ya Ukoloni walioweka mipaka bila kuwashirikisha wenye nchi zao. Hata Ulaya kuna Ukabila. Karibu nchi zote unazoziona Ulaya hasa Ulaya Mashariki ni nchi za Makabila. Ukabila ni jambo la asili, waalioungana kwa hiari yao huwa hawasumbui. Uliowalazimisha lazima watasumbua
 
Back
Top Bottom