Ethiopia na Djibouti zaomba kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)


View: https://twitter.com/Africa_Archives/status/1722801341783765446?t=opOQCWXDUZpH9KVGR-JY_A&s=19
 
Siku Zambia na South Africa wakijiunga ndiyo nitaamini, nchi za ajabu ajabu ndiyo zinaomba kujiunga.
 
Duh, sasa kama ethiopia wanaomba, somalia, wanaomba imebaki eritrea na djibout nao watataka kujiunga umoja huo. Huo umoja unaweza kupoteza maana na kupelekea kuundwa umoja mwingine utakaojumuisha nchi nyingi kuanzia zile tatu za mwanzo, za pembe ya afrika mpaka afrika ya kati yote. Sasa ndio nini hiyo? Hao wanachama wanataka amani, wanatamani amani ya giant Tanzania. Wakaribishwe tu ila wasitamani kushea ardhi yetu.
 
Safi sana nchi hizo kujiunga na EAC Community lakini DRC hawakustahili kuwepo EAC.
Mbona mliwakaribisha Rwanda,Burundi,DRC na South Sudan nchi zenye machafuko yaliyopitiliza?Acheni chuki zisizokuwa na msingi,mimi nionavyo Afrika Mashariki ilistahili kuwa na nchi zifuatazo:Ethiopia,Djibout,Eritrea,Somalia,Sudan,Sudan Kusini,Uganda,Kenya,Tanzania,Somalia,Burundi na Rwanda.
 
ANGALIZO.Tuwe makini na Kenya inaweza kuwa na mpango wa kuongeza Wanachama ili siku moja Makao makuu ya Afrika Mashariki yakaamia kwao kwa sababu wao watakuwa katikati na kuna hatari miji kama Nairobi,Kisumu au Eldoret ikapendekezwa kuwa makao makuu ya umoja huo.
 
Ukweli ndiyo Wakenya hufikiria mbali zaidi amini usiamini.
 
Kwanza hii iliyopo hatujaona faida yoyote na bado wanataka kuongeza wengine. Kwa mipango yao leo hii tulitakiwa tuwe na sarafu ya pamoja na mipango mingi ambayo hata kuanza tu kutekelezwa haijaanza. EAC ni kijiwe cha kupigia stori tu.
 
somalia kukubaliwa kujiunga kwa kweli ni htari sana!! [al-shabaab}
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…