Ethiopia: Updates on war against TPLF

Ethiopia: Updates on war against TPLF

Umekosea
1. Abiy ndiye aliyeanza mapigano ya kijeshi.
2.Kwa miaka 500 ya taifa la Ethiopia, watigray wametawala kwa miaka 27 tu.
3.Zenawi melesi mtigray rais aliyepita alifanikiwa kutokomeza njaa, ikumbukwe kabla ya hapo kila mwaka mamia walikufa kwa njaa
4.Chochote cha maana Ethiopia kina mkono wa tigrayans,
5.Watray wameungana na waoromo kabila la Abbiy, sababu ni chuki za Abby kwa yeyote anayehisi yupo juu take.
Viongozi na watu wenye ushawishi wa kabila la promo wamewekwa korokoni na huyo Abby, Jambo ambalo limepelekea hao waoromo kumgeuka Abby.
6. Abby. Anafanana na kiongozi flan ambaye alitaka atukuzwe na awe na influence katika kila sekta.
6.
Vibaraka wa mabeberu wapigwe tu
 
na kwa taarifa yako CCM ni chama cha kijeshi. kile chama ni tawi la kijesh kama unavyoiona jkt. hawa akina Kikwete Lowasa Jaka mwambi nk walikuwa wanajesh wa ngaz za juu tu na zaman ulikuwa huwez kuingizwa jesh kama huna Card ya ccm
Yana mwisho haya
Kukata mzizi wa fitna ni katiba Mpya!
 
Mkuu fafanua;

"4. Wa Tigray na Ahmara ni Wahabeshi wakati Waoromo ni Wakush"

Waziri Mkuu aliyepinduliwa Mengistu Haile Mariamu alikuwa kabila gani?

Mfalme aliyepinduliwa Haile Selasie alikuwa kabila gani?
 
Mkuu fafanua;

"4. Wa Tigray na Ahmara ni Wahabeshi wakati Waoromo ni Wakush"

Waziri Mkuu aliyepinduliwa Mengistu Haile Mariamu alikuwa kabila gani?

Mfalme aliyepinduliwa Haile Selasie alikuwa kabila gani?
Habesh ni jumuisho ya Makabila yenye ufanano na asilia ya Asia ya kusini kama Yemen. Ila tofauti Hawa waliunda Dola ya Kikristo ya kale sana na hawakua Arabized.

Watawala wa Ethiopia na Makabila yao.

1. Menelik II kabila lake ni Amhara
2. Haile Selassie kabila lake ni Amhara
3. Mengetsu Haile Mariam kabila lake Ahmara
4. Melez Zenawi kabila lake ni Tigray
5. Haile Mariam Deselng Kabila dogo la kusini Woylita.

6. Abiy Ahmed ni Muoromo.

Sent from my Lenovo L38111 using JamiiForums mobile app
 
Ni nani wanawafadhili hao TPLF!??
 
Jana nimelala vizuri kabisa kwa furaha maana nilikuwa nachukia sana kuona awa jamaa wanaoleta ukabila wanaendelea tu kusonga mbele.

Hakika marafiki wa kweli hapa Duniani ni Iran,Warusi na UAE + Waturuki.msaada wenu umekuwa nguzo muhimu sana kwa Watu wa Ethiopia,naimani Wa Ethiopia watawashkuru sana.pongezi zingine ziende kwa Eritrea kwa kusaidia mpaka kutoa wanajeshi japo kuna watu waliamua mpaka kukuwekea vikwazo.

Misri tulikuwa pamoja Libya ila safari hii umeniangusha sana. ujatumia akili na busara.
Misri ni kati ya nchi zinazowapa support Watigrayi kwa sababu ya Bwawa la kuzalisha umeme ambalo Abiy amelirithi kutoka utawala uliopita
 
Samahani kuuliza, huyu Mengistu Haile Mariam laiyemuua kikatili H. I. M Haile Selassie ni kabila lipi lati ya hayo tajwa?

Nadhani waethiopia walikosea kuuondoa utawala wa kizazi cha kina Menelik (Solomon Dynasty) pamoja na mapungufu yaliyokuwepo.

By then Ethiopia ilikuwa strong sana ila baada ya Mengistu kuzingua sidhani kama imewahi kuwa stable kama hapo kabla.
 
Salaam,

Kwa mahaba yangu Nitakua naweka updates za mapigano yanayoendelea huko Ethiopia Kati ya Jeshi la Serikali na Waasi wa TPLF na Jeshi lao liitwalo TDF.

Kwanza Kuna vitu vya kuweka sawa

1. Vita siyo Kati ya Ethiopia na Jimbo la Tigray. Bali ni Vita ni Kati ya Ethiopia na Chama Cha TPLF. Chama hicho ndiyo kina Jeshi lake liloitwa TDF (Tigray Defence Force). Chama hiki wafuasi wake wengi ni watu wa Jimbo la Tigray ila siyo wote. Takwimu zinataja Chama kinaungwa mkono huko Tigray kwa wasitani wa asilimia 70. Hivyo kama 30 ya Watigray hawakikubali.

Chama hiki ndiyo kiliongoza mapigano ya kumpindua Waziri mkuu wa Zamani Mangisu Haille Mariam mwaka 1991. Baada ya kufanikiwa Mtigray wa kwanza akaongoza nchi hiyo Bw Meles Zenawi.

Melez ndiye alirudisha utawala wa majimbo uliokua umetokomezwa tangu 1975 baada ya mapinduzi ya mfalme Haile Selassie.

Aidha katika utawala wa Melez ndiyo Watigray walikamata fursa zote za taifa.

Baada ya kifo cha Melez na maandamano ya Waoromo na Wahmara ulifanyika uchaguzi mkuu akashinda Bw Ali Ahmed Ali mwaka 2018.

Bw Abiy kwa kabila ni Muoromo. Abiy akaanza mikakati ya kuweka usawa jeshini na kwenye taasisi nyingi nyeti za taifa. Jambo ambalo liliwaudhi Watigray.

Chuki hii ndo imefikisha taifa katika vita.

2. Napenda niweke sawa wiano wa watu Ethiopia. Nchi hiyo inamakabila mengi zaidi ya 20 ila Makabila makubwa ni matatu. La kwanza ni Oromo 34% la pili Ahmara 27%, na la tatu ni TIGRAY 06%.

3. Historia utawala wa Ethiopia ni Kati ya wa Ahmara na Tigray. Wa Oromo hawajajaliwa kutwaa kiti mara nyingi.

4. Wa Tigray na Ahmara ni Wahabeshi wakati Waoromo ni Wakush.

Mwisho wa UTANGULIZI.

Vita.
TPLF ni rafiki wa Magharib hasa US. Wakati Abiy ni rafiki wa nchi majirani hasa Eritria, Somali hadi UAE. Sababu ya hili ni moja, Watigray huwa ni vibaraka wa US, kusimamia maslahi ya US katika pembe ya AFRICA. Utakumbuka enzi za PM Melez Zenawi akiwa Waziri Mkuu wa Ethiopia. US walikua wanatumia Jeshi la Ethiopia kuwachapa Wasomali na Wa Eritria.

Sasa Waeritria hawataki Watigray watawale Ethiopia kwa hofu zama za Marekani kuwapiganisha zitarudi.
Ni sahihi kabisa
 
Marekebisho kidogo.
1: Kabila la tatu kwa ukubwa ni Somali halafu ndiyo Tigray.

2: Hili kabila la mama na mke wa Abbiy ni AMHARA sio Ahmara.

3: Abbiy alichaguliwa na bunge kama kiongozi wa mpito baada ya PM Haile Mariam Desalegn kujiuzuru kufuatia machafuko ya mauaji ya maelfu wa Oromo kabila la Abbiy. Hivyo hakuchaguliwa kwa uchaguzi mkuu.

La ziada ni kuwa japokuwa ni mahasimu wa kutupwa (Eritrea na TPLF) lakini chakustaajabisha ni kuwa Kabila kubwa Eritrea ni Tigray. Inasemekana Esayas Afwerk (Rais wa Eritrea) alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa waasi waliomuweka Zenawi madarakani lakini baadae wakahitilafiana ndiyo Afwerk akataka amegewe eneo lake na kuiasisi Eritrea.
Nyongeza murua kabisa! Ila kabila ni Tigrinya ambayo pia ni lugha inayoongelewa katika jimbo la Tigray na Eritrea.

Kwahiyo kuna watigrinya wa Ethiopia walio katika jimbo la Tigray na walioko Eritrea. Ni sawa na Wamasai ambao wako Kenya na Tanzania - ni walewale!
 
Nyongeza murua kabisa! Ila kabila ni Tigrinya ambayo pia lugha inayoongelewa katika jimbo la Tigray na Eritrea.

Kwahiyo kuna watigrinya wa Ethiopia walio katika jimbo la Tigray na walioko Eritrea. Ni sawa na Wamasai ambao wako Kenya na Tanzania - ni walewale!
Hapana,iko hivi;

1.Watigray walioko Eritrea wanaitwa TIGRINYAS

2.Watigray walioko Ethiopia wanaitwa TIGRIANS.
 
Back
Top Bottom