Habari zenu binafsi kwa ujumla wenu;
Jana wakati napata kifunga kinywa pale kingstaa kaunta ya juu wakaja wadada wawili wanapiga stori ya mwenzao waliyetoka kumwombea azidi kulala pahala pema peponi baada ya kumaliza mwaka mmoja akiwa chini ya dongo takriban tani saba. Walikuwa wanasikitika uamuzi wa rafiki yao huyo kujiua. Kwa unasaji wangu wa habari (siyo umbea) nikalazimika kuwajoin ili waninusishe yaliyojiri.
Ni hivi:
Kulikuwa jamaa marafiki wawili bwana X na bwana Y ambao walikuwa wameoa na bahati nzuri wake zao nao pia wakatokea kuwa marafiki wazuri. Katika pilikapilika za maisha siku moja bwana X akapata ajali iliyomgharimu kutenguka kiuno na kuparalaiz kuanzia kiunoni mpaka miguuni. Maisha ya Bwana X yakahamia kitandani rasmi, na baioloji yake ikawa haina mawasiliano na jinsia ya kike.
Bwana Y kwa upendo akawa anaisaidia familia ya Bwana X kwa hali na mali (kipato cha mke wa bwana X hakikutosha kuhimili mikiki ya maisha katika hali hii ya serikali ya awamu ya nne)
Mwaka ukakatika, mke wa X akaingiwa na shetani sehemu zake za siri. Akajikuta analazimika kujipitisha na kumimina mabode langueji ya malavidavi kwa bwana Y. Bwana Y uzalendo ukamshinda akalazimika kuliamsha pepo la ngono lililolala kwenye baioloji yake. Shughuli ikaanza wakanogewa na dhambi. Wakajivinjari bila ya mgonjwa X wala mke wa Y kujua mpaka Malaika wa Mungu alipoamua kuweka mambo hadharani.
Siku moja wamepiga ulabu, bwana Y akamsindikiza mke wa X mpaka nyumbani kwa Bwana X. Pepo likawaingia wakaanza kujivinjari sebuleni. Makelele ya malavidavi, Bwana X akastuka usingizini, sijui alipata wapi nguvu akajiangusha kitandani, akajiburuza mpaka sebuleni akashuhudia rafiki yake akimla uroda mkewe
.. Akaachia yowe kwa mstuko, na Ziraili mtoa roho akaichukua roho yake kupitia njia ya mstuko wa Moyo
Haikupita muda mke wa Bwana X nadhiri ikawa ikamsuta
. akaona isiwe tabu
kwa hiyari yake tena bila ya kushauriwa wala kulazimishwa na mtu, akamwalika ziraili aje kuchukua roho yake kupitia mtaa wa sumu
. Naye akatangulia kuzimu. Yaliyojiri kwa bwana Y ni kuwa ndoa yake imekuwa historia. Na Bwana Y amekuwa kama kreze akiamini ameua watu wawili at a go! (Nadhani baioloji yake itakuwa imepata hitilafu flani)
Sasa ndugu zangu, (kina mama safari hii hebu kuweni wakweli japo kiduchu):
1.Hiki kiapo kwamba nitakuwa mwaminifu mpaka kifo kitutenganishe kinatekelezeka? Is it practical kwa wanawake? (Kwa wanaume sitii neno hapo, kwa sababu liko wazi kabisa)
2.Eti mwaweza kwenda kuliwa uroda ilhali mumeo unayempenda sana mpaka ukaamua kuhamia kwake yu kitandani hoi? Nadhiri haziwasuti? (Ningekuwa Mungu mngenitambua hakyanani)
3.Je mwaweza kuvumilia muda gani wakati mnajua kabisa huyu unayelala naye kitanda kimoja baioloji yake ishakuwa si rizki? Mwaweza kuvumilia mpaka ziraili mtoa roho afanye kazi yake? (Hapa mnaweza kuniambia kwa PM manake najua wengine mwaogopa kusema hadharani)
Babu ako konfyuzdi na ameanza kuogopa kutenguka kiuno
.Bibi bado anadai wasije wakanichakachulia kwenye hili banda nililojenga kwa pesa za mkopo;
Angalizo: Hii mada ni serious na atakayeenda Ofu Topic
.nambwenga makwenzi afu anakula BAN!