Eti inawezekana?...UVUMILIVU MPAKA LINI?

Eti inawezekana?...UVUMILIVU MPAKA LINI?

Naamini kuwa wapo wanawake waaminifu, na ambao wanaweza hasa kujinyima chochote kwa waume zao.

Mimi kwa nnavyojiona sio mmoja wa hao (inaweza ikawa tofauti likinifika), na naamini wengi ni wa kundi hili la kutoweza kustahamili (so better kudai talaka).

Napata mshangao kuona sample ya hapa JF ni almost ni yale waaminifu watupu! ....hapo tu

Mwalimu, Mwenyezi Mungu anendelee kuwabariki na kuwaongoza
 
THIS IS VERE VERE NASHUKUR KWA KUENDELEA KUNITUNZIA MATY MDOGO MIAKA IKIFIKA INSHALLAH NITAKUJA KUGONGA MLANGO NIKIWA NA UJUMBE MZITO UTAOONGOZWA NA ASPRIN

The Following User Says Thank You to Maty For This Useful Post:

The Finest (Today)​

Hahahaaaaaaaaa lol usijali kabisa nakutunzia wewe ni mbaba peke ako humu muaminifu lol
 
Naamini kuwa wapo wanawake waaminifu, na ambao wanaweza hasa kujinyima chochote kwa waume zao.

Mimi kwa nnavyojiona sio mmoja wa hao (inaweza ikawa tofauti likinifika), na naamini wengi ni wa kundi hili la kutoweza kustahamili (so better kudai talaka).

Napata mshangao kuona sample ya hapa JF ni almost ni yale waaminifu watupu! ....hapo tu

Hahaha...mwalimu bana....

At least leo tumepata picha nyingine tofauti kidogo manake ....dah!
 
Hivi mwalimu unaamini kwamba pamoja na wanaume kusema kwao ukweli kwamba wanatoka nje ya ndoa wapo ambao hawatoki kabisa nje ya ndoa zao. Sasa kama kuna wanaume hawatoki nje ya ndoa zao unashindwaje kuamini kwamba kuna wanawake waaminifu, mimi inawezekana si muaminifu lakini naamini wapo waaminifu. Kila kitu ni kukiendekeza na kukipenda

Maty unayosema ni kweli na uaminifu upo, na sio kwamba tunasema hakuna waaminifu, la hasha! Tunataka kuthibitisha kwamba wote WANAWAKE KWA WANAUME HUTOKA NJE PASIPO KUSEMA MMOJA KAMZIDI MWENZAKE
 
Habari zenu binafsi kwa ujumla wenu;

Jana wakati napata kifunga kinywa pale kingstaa kaunta ya juu wakaja wadada wawili wanapiga stori ya mwenzao waliyetoka kumwombea azidi kulala pahala pema peponi baada ya kumaliza mwaka mmoja akiwa chini ya dongo takriban tani saba. Walikuwa wanasikitika uamuzi wa rafiki yao huyo kujiua. Kwa unasaji wangu wa habari (siyo umbea) nikalazimika kuwajoin ili waninusishe yaliyojiri.

Ni hivi:

Kulikuwa jamaa marafiki wawili bwana X na bwana Y ambao walikuwa wameoa na bahati nzuri wake zao nao pia wakatokea kuwa marafiki wazuri. Katika pilikapilika za maisha siku moja bwana X akapata ajali iliyomgharimu kutenguka kiuno na kuparalaiz kuanzia kiunoni mpaka miguuni. Maisha ya Bwana X yakahamia kitandani rasmi, na baioloji yake ikawa haina mawasiliano na jinsia ya kike.

Bwana Y kwa upendo akawa anaisaidia familia ya Bwana X kwa hali na mali (kipato cha mke wa bwana X hakikutosha kuhimili mikiki ya maisha katika hali hii ya serikali ya awamu ya nne)

Mwaka ukakatika, mke wa X akaingiwa na shetani sehemu zake za siri. Akajikuta analazimika kujipitisha na kumimina mabode langueji ya malavidavi kwa bwana Y. Bwana Y uzalendo ukamshinda akalazimika kuliamsha pepo la ngono lililolala kwenye baioloji yake. Shughuli ikaanza wakanogewa na dhambi. Wakajivinjari bila ya mgonjwa X wala mke wa Y kujua mpaka Malaika wa Mungu alipoamua kuweka mambo hadharani.

Siku moja wamepiga ulabu, bwana Y akamsindikiza mke wa X mpaka nyumbani kwa Bwana X. Pepo likawaingia wakaanza kujivinjari sebuleni. Makelele ya malavidavi, Bwana X akastuka usingizini, sijui alipata wapi nguvu akajiangusha kitandani, akajiburuza mpaka sebuleni akashuhudia rafiki yake akimla uroda mkewe….. Akaachia yowe kwa mstuko, na Ziraili mtoa roho akaichukua roho yake kupitia njia ya mstuko wa Moyo…

Haikupita muda mke wa Bwana X nadhiri ikawa ikamsuta…. akaona isiwe tabu…… kwa hiyari yake tena bila ya kushauriwa wala kulazimishwa na mtu, akamwalika ziraili aje kuchukua roho yake kupitia mtaa wa sumu……. Naye akatangulia kuzimu. Yaliyojiri kwa bwana Y ni kuwa ndoa yake imekuwa historia. Na Bwana Y amekuwa kama kreze akiamini ameua watu wawili at a go! (Nadhani baioloji yake itakuwa imepata hitilafu flani)

Sasa ndugu zangu, (kina mama safari hii hebu kuweni wakweli japo kiduchu):

1.Hiki kiapo kwamba “nitakuwa mwaminifu mpaka kifo kitutenganishe” kinatekelezeka? Is it practical kwa wanawake? (Kwa wanaume sitii neno hapo, kwa sababu liko wazi kabisa)

2.Eti mwaweza kwenda kuliwa uroda ilhali mumeo unayempenda sana mpaka ukaamua kuhamia kwake yu kitandani hoi? Nadhiri haziwasuti? (Ningekuwa Mungu mngenitambua hakyanani)

3.Je mwaweza kuvumilia muda gani wakati mnajua kabisa huyu unayelala naye kitanda kimoja baioloji yake ishakuwa si rizki? Mwaweza kuvumilia mpaka ziraili mtoa roho afanye kazi yake? (Hapa mnaweza kuniambia kwa PM manake najua wengine mwaogopa kusema hadharani)

Babu ako konfyuzdi na ameanza kuogopa kutenguka kiuno….Bibi bado anadai wasije wakanichakachulia kwenye hili banda nililojenga kwa pesa za mkopo;

Angalizo: Hii mada ni serious na atakayeenda Ofu Topic….nambwenga makwenzi afu anakula BAN!
seriously contradicting indeed, i need to learn why walifanyia nyumbani kwa jamaa, hiyo haitakua mara ya kwanza
 
Hahahaha...uliza kina mama hao...watakujibu wanawavumilia kwa MSAADA WA MUNGU.......wizi mtupu!

nitashukuru kama wakijibu. Kuna observation moja kwamba kwenye familia ambayo baba ana ugonjwa huo huwa kuna kijana wa kazi mtanashati sana au ndugu wa baba anayeishi hapo homu. Au extreme cases, huyo baba anaye rafiki yake (kama asprin) ambaye ni family friend wa karibu sana.
 
seriously contradicting indeed, i need to learn why walifanyia nyumbani kwa jamaa, hiyo haitakua mara ya kwanza

Lile pepo likiwakolea kisawasawa ni kama kipindupindu!
 
Sasa jamaa ameshatenguka kiuno na mkewe anahitaji mambo anategemea angevumiliwa mpaka kifo? mazingira ya tukio la kujivinjari hayakuwa mazuri kiukweli nikimaanisha jamaa kuugulia ndani halafu mke kuja na mtu sebuleni.

Uvumilivu una mwisho!
 
nitashukuru kama wakijibu. Kuna observation moja kwamba kwenye familia ambayo baba ana ugonjwa huo huwa kuna kijana wa kazi mtanashati sana au ndugu wa baba anayeishi hapo homu. Au extreme cases, huyo baba anaye rafiki yake (kama asprin) ambaye ni family friend wa karibu sana.

Aisee Muhosni utatufukuzia wachangiaji wa kike hapa.......... hiyo ni ngumu 'kumesa' kwao asee
 
Naamini kuwa wapo wanawake waaminifu, na ambao wanaweza hasa kujinyima chochote kwa waume zao.

Mimi kwa nnavyojiona sio mmoja wa hao (inaweza ikawa tofauti likinifika), na naamini wengi ni wa kundi hili la kutoweza kustahamili (so better kudai talaka).

Napata mshangao kuona sample ya hapa JF ni almost ni yale waaminifu watupu! ....hapo tu

Asante mwalimu kwa majibu yako mazuri pekundu hapo wapo watu waaminifu tusibishe, bluu hapo umejiamulia mwenyewe kwamba huwezi ishi bila hiyo makitu uko sawa sawa kila hata mungu ndio maana kamshusha shetani na yesu/mtume kila mtu ajichagulie wa kumtumikia so kila kitu ni kukipenda tu na kukihusudu
 
Hivi mwalimu unaamini kwamba pamoja na wanaume kusema kwao ukweli kwamba wanatoka nje ya ndoa wapo ambao hawatoki kabisa nje ya ndoa zao. Sasa kama kuna wanaume hawatoki nje ya ndoa zao unashindwaje kuamini kwamba kuna wanawake waaminifu, mimi inawezekana si muaminifu lakini naamini wapo waaminifu. Kila kitu ni kukiendekeza na kukipenda

Maty si kwamba hakuna wanawake waaminifu wapo sana tena wengi tu lakini wapo ambao si waaminifu pia na wanakuwa na sababu za "MSINGI" si za "NYONGEZA"

Ukiona mama aliyeolewa anatoka nje ya ndoa ujue kuna sababu kubwa mnoooooo tena sana kwanini nasema hivyo "Wanawake wanapenda kutoka rohoni" Wanaume wanapenda kwa macho" Ndo maana wao ni rahisi sana kutoka nje kuliko wakina mama.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom